katiba mpya ni" collection" ya "madesa" bila "thinking behind"

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
kimsingi utawala wa nchi ni mihili mitatu, lakini kwa mujibu wa katiba ya sasa na katiba inayopendekezwa kwa kuangalia mazingira ya tanzania tuna mihimili mitatu kinadharia lakini kivitendo tuna mhimili mmoja tu.

sababu za kuwa na mhimili mmoja kuu ni mbili

1. huwezi kuwa na bunge ambalo ni sehemu ya serikali na ukawa na mahakama inayoteuliwa na serikali ukawa na mihimili mitatu inayoweza kusimamiana katika utendaji.

2. ni kosa kubwa kuwa na mihimili mitatu alafu ukachukua nguvu za jamii zote zikawekwa katika mhimili mmoja. mfano serikali ndio mhimili unaomiliki majeshi na fedha na hizi ni nguvu ambazo zinaifanya serikali kujenga kiburi kwa mihimiri mingine kwa maana hata wafanye maamuzi hawa wengine je serikali isipotekeleza watafanya nini? sababu hii inawafanya mahakama na bunge kuchukua ushauri wa adui usiyeweza kumsinda ungana naye hivyo badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi kusimamia utendaji wa serikali ni kuungana na serikali kuwa kitu kimoja.

kosa kubwa jingine tulilolifanya ni kutengeneza kijiwe cha kahawa eti kusimamia serikali.
mfumo wa bunge tulioutengeneza ni kijiwe cha kahawa hakina utaalamu wala mfumo wa kusimamia na kushauri serikali. tunatumia fedha nyingi kuendesha chombo kisichokuwa na tija kutokana na chombo kutokutumia utaalamu wala utaratibu kufanya kazi.

kwa nini baraza la madiwani na bunge kisiwe chombo kimoja lakini watu hawa wanafanya kazi kwa takwimu. diwani kazi yake ni kufuatilia utendaji wa serikali katika kata. kama ni utendaji katika shule, vituo vya afya, ujenzi wa miradi ya maendeleo na katika halmashauri wanakutana katika ofisi ya mbunge kujumuisha takwimu na kuzichambua. ofisi ya mbunge ina wataalamu wa kufuatilia utendaji wa halmashauri na yeye wakati wote yuko jimboni ndiye mtendaji mkuu. ripoti za madiwani katika jimbo pamoja na taarifa za utendaji wa halmaushauri zinajadiliwa na madiwani na kutengeneza ripoti ya mbunge kupeleka bungeni ikiwa ndio utendaji wa serikali.

mwananchi yeyote akiombwa rushwa, kudharauriwa, kunyanyaswa katika ofisi yoyote ya umma anakimbilia ofisi ya mbunge kutoa taarifa.

lakini eti mtu yuko kwenye biashara zake akitoka huko anaenda kujadili utendaji wa serikali kwa hisia tu hivi kweli hiki si kijiwe cha kahawa? tunapolaumu utendaji wa serikali je bunge si ndio linatakiwa kubeba lawama likiwa la kwanza maana msimamiaji yuko wapi?

kuwachukua wanasiasa eti wanapita katika mashirika kukagua hesabu sijui kufanya nini nadhani tunafanya mchezo, kwanini chombo hiki kisiajiri wataalamu waliobobea kufanya kazi hiyo na hawa wawakilishi wa wananchi wanajadili mapendekezo yao.

nadhani bunge letu ni kituko namba moja lakini haya tunaweza kuyarekebisha kupitia katiba.

sasa kiukweli sijui tunafanya nini lakini matokeo ya kutokuwa na mifumo ni kila anayekabidhiwa kitengo akiona kina maslahi ni kujinufaisha mwenyewe maana hakuna mifumo ya kijamii kusimamia.

binafsi nimejiuliza kama katiba hii tumeitunga kwa kuangalia matatizo yetu na kutafuta jinsi ya kuyatatua au tumekusanya materials na kuweka pamoja bila kureflect matatizo yetu kwa maana matatizo mengi tunayolalamikia ya mfumo yanatokana na udhaifu katika mihimili mitatu ya juu au kukosa mihimili mitatu na kuwa na mhimili mmoja.
 
Heeeee ndugu hebu pisha huko usituvuruge na uongo wako humu, umeandika maneno kibao na hata hapo najua hujamaliza una haki ya kutoa ya moyoni na yale ambayo hujayatoa subiri nimalize uandike tena, hakuna unachokiongea hapa na hujaisoma katiba pendekezwa maana ungeelewa tu, miaka kibao umeishi Tanzania labda niwe nazungumza na non -Tanzanian lakini kama wewe ni Mtanzania utanielewa, hoja ya kuwa tuna mihimili 3 kinadharia na si kivitendo sijui umeiokota wapi? nashindwa kukuelewa hata hujui majukumu ya mahakama, Bunge na Serikali, na hata umeshindwa kuelewa kabisa mihimili hii inafanya kazi pamoja kwa manufaa ya watanzania? Rudi darasani usipotoshe na uache siasa katika masuala yaliyolifikisha taifa la Tanzania hapa. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
 
unauma usichoweza kutafuna, jambo hili nadhani liko juu ya uwezo wa akili yako waachie wenye uwezo wa kufikiri walitafakari kwa maana kama ungeangalia sababu za kutokuwa na mihimili mitatu usingekurupuka.

bunge linatakiwa kusimamia serikali kwa maana kuangalia yale serikali inayoyafanya kama ndiyo wananchi wanayotaka sasa serikali ni sehemu ya bunge kwa maana mawaziri ni wabunge na serikali inateua watumishi mbalimbali kutoka bungeni. katika mazingira hayo wabunge hawasimami kuikosoa serikali bali wanajadili hoja za serikali kwa kujitengenezea mazingira ya kuteuliwa.

hata kama serikali imekosea mbunge hajali kazi ya bunge ni nini bali anasimama kutetea. lakini kama bunge lisingekuwa na muingiliano wowote na serikali wabunge wangukuwa wanawafanyia kazi wananchi waliowatuma tu bila kujadili hoja kwa kujitengenezea mazingira ya kuteuliwa.

mahakama zetu majaji wanatoka wapi? niambie kama uteuzi wa watumishi katika nchi yetu uko huru? huu ni mfumo tulioujenga hebu niambie siku raisi akivunja katiba utampeleka mahakama gani ambayo inaweza kusimama kusema huyu mtu ambaye ameleta kesi ambaye ni "no body" anachokidai ni sahihi dhidi ya huyu raisi aliyeniteua na mwenye mamlaka ya kutengua uteuzi wangu wakati wowote.

tukisema uwepo wa mihimili mitatu ni kuwa na vyombo hivyo vikisimamiana kwanza, serikali ikifanya makosa lipo bunge kukemea na kukosoa ua kuwajibisha, serikali ikifanya makosa ipo mahakama kutoa hukumu juu ya hayo. lakini kama bunge na mahakama haviwezi kufanya lolote juu ya makosa ambayo serikali inatenda basi inakuwa mihimili hiyi haipo bali mfumo wetu umeviingiza vyombo hivyo ndani ya serikali na kuwa sehemu ya serikali na vikashindwa kufanya kazi.

lengo ni kuangalia ni kwa vipi tunaweza kuwa na mihimili mitatu inayosimamiana katika kufanya kazi.

EGO kubali kuambiwa ukweli, mbona unakuwa mbishi tena unatumia maneno ya uongo hivyo? alichokisema jamaa hapo juu ni right kabisaa kuwa umesahau mambo muhimu hasa majukumu ya mahakama, BUNGE NA sRERIKALI NA JINSI INAVYOFANYA KAZI.
 
Usipoteze muda mwingi kufukuza upepo usiojua unakoelekea,unatamani sana majaji uwe unawateua wewe eee!!! hapo ndo utaelewa mwenyewe hujui Serikali ni nini? Mahakama ni nini? na Bunge ni nini? hata hujui mamlaka ya Rais, ungefahamu haya usingepoteza muda wako hapa na wala hujui kuwa katiba pendekezwa inataja wazi Mamlaka ya wananchi, kwenye Ibara ya 7, hujui mimi, wewe na wananchi wengine ndio tuanatoa mamlaka kwa Serikali iliyoko madarakani? acha kuchangia kwa hisia hapa naomba uisome vizuri tena na tena acha kukurupuka.
 
hapa si swala la propaganda la kusema kubali hiki au kataa hiki bila sababu hoja ni hivi watendaji walioko katika serikali wanawezaje kufanya kazi wakijua kuna vyombo ambavyo viko ulingo mmoja mmoja na wao ambavyo viko macho kuangalia na vina mamlaka ya kuingilia.

tatizo tuna watu wanokalili wanaokwenda katika mahakama jukumu lake ni nini na utaratibu wake ni nini lakini lazima mtambue mahakama kuwa ndani ya serikali inaifanya mahakama kutokuwa ulingo mmoja na serikali na watabaki kutoa maamuzi yanayohusu wananchi wa chini lakini jambo lolote linahusu utendaji wa juu watabaki kimya.

bunge kuwa sehemu ya serikali ni uzaifu mkubwa. nitamshangaa mtu anayesema eti anatambua jinsi bunge linavyotakiwa kufanya kazi alafu anasapoti kuletwa mswada wa madini bungeni wanajadili wakina nani? wanajadili kwa kutaja viji vyao na kupigiana makofi lakini mwisho katika utekelezaji wanalalamika hatupati fedha kutoka katika madini wakati miswada wanapitisha wao.

hapa tunaweza kuwa tunajadili mambo haya kwa staili ileile ya watu kujadili si kwa kuangalia kuielekeza jamii vizuri bali pengine kwa kuangalia kusapoti au kupinga ili kujitengenezea mazingira fulani lakini jamii inaouelewa wa kutosha kuchambua kile ambacho wanaona kinawafaa.

la kusikitisha wengi wameshakuwa mashabiki ambao hawaelewi wanachikifanya.

EGO kubali kuambiwa ukweli, mbona unakuwa mbishi tena unatumia maneno ya uongo hivyo? alichokisema jamaa hapo juu ni right kabisaa kuwa umesahau mambo muhimu hasa majukumu ya mahakama, BUNGE NA sRERIKALI NA JINSI INAVYOFANYA KAZI.
 
kila kitu kina maslahi isipokuwa kwa nani ndio swali la msingi

Usipoteze muda mwingi kufukuza upepo usiojua unakoelekea,unatamani sana majaji uwe unawateua wewe eee!!! hapo ndo utaelewa mwenyewe hujui Serikali ni nini? Mahakama ni nini? na Bunge ni nini? hata hujui mamlaka ya Rais, ungefahamu haya usingepoteza muda wako hapa na wala hujui kuwa katiba pendekezwa inataja wazi Mamlaka ya wananchi, kwenye Ibara ya 7, hujui mimi, wewe na wananchi wengine ndio tuanatoa mamlaka kwa Serikali iliyoko madarakani? acha kuchangia kwa hisia hapa naomba uisome vizuri tena na tena acha kukurupuka.
 
mh nahisi kuna tatizo somewhere.... naona ID mpya humu zikipigia chapuo katiba pendekezwa kwa vioja na sio hoja, au ndo mshakodiwa?
 
Mkuu ego kimsingi, tulichotakiwa kufanya ni kuamua je, tunafuata mfumo upi? Presidential republic, semi presidential au full presidential?
Kwa sababu serikali inaweza ikawa derived from parliament lakini bado ikadeliver mazuri, case in point ni nchi za ulaya France, UK etc
Hii hybrid system yetu ambayo haieleweki ni disaster waiting to happen!
 
Last edited by a moderator:
Umeishiwa hoja sasa unaanza kusema kila linalokujia. Au nawe umekodiwa kama unavyohisi wengine. Lete hoja tukujibu. Lakini wakiuliza waliochangia nawe utakuwa miongoni mwao. Hongera kwa kujitokeza.
 
dhana ya kuwa na mihimili mitatu lazima tujiulize ni nini?

hii imetokana na ukweli kuwa jamii ambayo inamiliki mali haiwezi kusimamia moja kwa moja hivyo wanaweka mfumo wa uongozi ambao unajisimamia wenyewe. unamchukua huyu unampa madara haya, unamchukua yule unampa madaraka yale na yule wote wanakuwa wanawajibika kwako na wanafanya kazi kwa kusimamiana.

lakini ukiunda mfumo ambao umetengeneza mifumo isimamiane alafu ukamchukua mmoja yeye ndiye mwenye nguvu zote na ndiye anayewateua wengine hapo ni moja kwa moja kuwa hawa wengine wanatoka kutumikia jamii na wanaanza kumtumikia huyu anayewateua.

ile dhana ya kufanya kazi kwa kusimamiana unakuwa huwezi kuipata maana wote wakishaungana na kuanza kufanya kazi kama kitu kimoja ni sawa na kuwa na taasisi moja isiyosimamiwa.

matokeo ya hilo ni kutokuwepo na yeyote wa kumfunga paka kengele na jambo lolote linalohusu uwajibikaji mpaka wakubaliane wote ndio mifumo inaanza kufanya kazi.

wenzetu mifumo hiyo inaweza kufanya kazi kutokana na mazingira yao kwa maana kumteua mtu kule yawezekana huwezi kumkontrol eti kwa sababu umemteua.

lakini huku kwetu ni tofauti na kama tunataka kutoka katika umasikini ni lazima tufanye mfumo ambao mahakam watakaa wakijua kuna serikali, kuna bunge wanaona tunayoyafanya, serikali watakaa wanajua kuna mahakama kuna bunge wanaangalia tunachokifanya, bunge watakaa wanajua kuna serikali kuna mahakama wanaaangalia tunachokifanya.

kuangalia si lazima kwa maana ya msimamizi moja kwa moja lakini kama taasisi ikijua tukifanya kosa hili basi mtu anaweza kwenda katika taasisi fulani na hawa wakafanya maamuzi tutapunguza makosa ya kiuzembe, tutapunguza makosa ya kimaadili, tutapunguza makosa ya kutotumia maarifa.

tuanzie kwenye kelele zinazopigwa na wananchi na tujiulize kwa system zilivyo kweli ni kiongozi gani anaweza kuja kusukuma watu wote waende kama anavyotaka yeye? kimsingi haiwezekani hivyo suluhisho ni kuzifanya taasisi kusimamiana.

sasa je hilo tumelifanya au tumebadili maneno lakini maana imebaki ile ile?

Mkuu ego kimsingi, tulichotakiwa kufanya ni kuamua je, tunafuata mfumo upi? Presidential republic, semi presidential au full presidential?
Kwa sababu serikali inaweza ikawa derived from parliament lakini bado ikadeliver mazuri, case in point ni nchi za ulaya France, UK etc
Hii hybrid system yetu ambayo haieleweki ni disaster waiting to happen!
 
mh nahisi kuna tatizo somewhere.... naona ID mpya humu zikipigia chapuo katiba pendekezwa kwa vioja na sio hoja, au ndo mshakodiwa?

Wewe una matatizo sana na ni mbinafsi na unashindwa kuelewa kuwa kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake kwa uhuru,Eti unahisi kuna tatizo somewhere kuona ID mpya nyie ndio mafashist wenyewe msiopenda mabadiliko na mnawaza forum hii ni yenu peke yenu na mna hati miliki huo ni upuuzi na ubinafsi uliokithiri ambao watanzania hawana tabia hii ninaanza kuwa na mashaka na wewe na kititle chako cha JF Senior Expert Member afu mbinafsi usiyetaka mabadiliko kuona wenzio wakichangia au unataka kuona michango yako ikiprevail humu bila kupingwa?
 
dhana ya kuwa na mihimili mitatu lazima tujiulize ni nini?

hii imetokana na ukweli kuwa jamii ambayo inamiliki mali haiwezi kusimamia moja kwa moja hivyo wanaweka mfumo wa uongozi ambao unajisimamia wenyewe. unamchukua huyu unampa madara haya, unamchukua yule unampa madaraka yale na yule wote wanakuwa wanawajibika kwako na wanafanya kazi kwa kusimamiana.

lakini ukiunda mfumo ambao umetengeneza mifumo isimamiane alafu ukamchukua mmoja yeye ndiye mwenye nguvu zote na ndiye anayewateua wengine hapo ni moja kwa moja kuwa hawa wengine wanatoka kutumikia jamii na wanaanza kumtumikia huyu anayewateua.

ile dhana ya kufanya kazi kwa kusimamiana unakuwa huwezi kuipata maana wote wakishaungana na kuanza kufanya kazi kama kitu kimoja ni sawa na kuwa na taasisi moja isiyosimamiwa.

matokeo ya hilo ni kutokuwepo na yeyote wa kumfunga paka kengele na jambo lolote linalohusu uwajibikaji mpaka wakubaliane wote ndio mifumo inaanza kufanya kazi.

wenzetu mifumo hiyo inaweza kufanya kazi kutokana na mazingira yao kwa maana kumteua mtu kule yawezekana huwezi kumkontrol eti kwa sababu umemteua.

lakini huku kwetu ni tofauti na kama tunataka kutoka katika umasikini ni lazima tufanye mfumo ambao mahakam watakaa wakijua kuna serikali, kuna bunge wanaona tunayoyafanya, serikali watakaa wanajua kuna mahakama kuna bunge wanaangalia tunachokifanya, bunge watakaa wanajua kuna serikali kuna mahakama wanaaangalia tunachokifanya.

kuangalia si lazima kwa maana ya msimamizi moja kwa moja lakini kama taasisi ikijua tukifanya kosa hili basi mtu anaweza kwenda katika taasisi fulani na hawa wakafanya maamuzi tutapunguza makosa ya kiuzembe, tutapunguza makosa ya kimaadili, tutapunguza makosa ya kutotumia maarifa.

tuanzie kwenye kelele zinazopigwa na wananchi na tujiulize kwa system zilivyo kweli ni kiongozi gani anaweza kuja kusukuma watu wote waende kama anavyotaka yeye? kimsingi haiwezekani hivyo suluhisho ni kuzifanya taasisi kusimamiana.

sasa je hilo tumelifanya au tumebadili maneno lakini maana imebaki ile ile?
Mkuu,
Katika parliamentary system parliament (bunge) ndicho chombo kikuu cha dola; Mahakama na serikali (executive) zinakuwa derived from it. Hii inakuwa na faida zake. Haiwezekani serikali kucontrol bunge, if anything inakuwa the other way round (bunge ndilo linacontrol serikali). Hii inasaidia kuincrease accountability ya serikali.
Tatizo letu ni kwamba mfumo wetu wa sasa una chembe za parliamentary system (wabunge kuwa mawaziri) lakini pia presidential (rais anakuwa head of state AND government). Kuwa na rais powerful hivi ndicho chanzo cha matatizo ya mfumo wetu; unakuta rais anasign mikataba bila kulishirikisha bunge, anateua watu anaowataka yeye nk.
Huko nje (parliamentary systems), unakuta Rais anakuwa head of state then waziri mkuu anakuwa head of government. Rais, ambaye ndiye mkuu wa nchi anachaguliwa na wananchi lakini waziri mkuu ambaye ndiye kiongozi wa serikali anachaguliwa na bunge na anakuwa answerable to bunge. Bunge lina mamlaka ya kuifuta serikali nzima kwa kupiga vote of no confidence in the Prime Minister, kitu ambacho ni rahisi kuliko kumuondoa Rais wa nchi.
Udhaifu wa hii system utakuja kuonekana bayana endapo itawai kutokea Rais mteule ni wa chama A lakini chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B. Kitakachofuata hapo ni what wazungu wanaita 'political gridlock'!
 
nadhani uko sahihi kabisa kwa maana katika mihimili mitatu ule mhimili ambao ndio wawakilishi wa wananchi ndio mhimili mkuu na wananchi wamekasimu mamlaka yao baadhi kwa chombo hiki ili kifanye kazi ya kufuatilia utendaji wa serikali.

lakini kwa mfumo wetu jinsi ulivyo sasa bunge halina nguvu wanabaki kuongea tu na kulalamika kuwa sisi wabunge kila siku tunaongea lakini serikali haitekelezi?

lakini kwa mfumo wetu wa bunge wa sasa ambapo hakuna mfumo ni vijembe na fitina na understanding ya mtu binafsi huwezi kuliweka bunge juu ya serikali ni kutengeneza confusion kwa wataalamu.

lazima tulielekeze bunge cha kufanya.

mfano kama serikali itapanga bajeti na ikaenda kutekelezwa na tukaenda na mfumo wa kukusanya takwimu.

mfano diwani anakusanya takwimu katika kata, idadi ya walimu, mahudhurio yao, takwimu za masomo waliyojifunza wanafunzi darasi, performance ya shule katika mitihani ya kikanda na kitaifa, takwimu katika vituo vya afya, ujenzi wa barabaram, utendaji wa viongozi wa vijiji au kata.

takwimu hizi wanatengeneza reporti moja katika ofisi ya mbunge na repoti hiyo ndiyo ya kuhoji halmashauri ili itolee ufafanuzi na majumuisho baadae. mtitiriko huu ndio unaokwenda bungeni kwa bunge kukusanya takwimu za kila wizara nchi nzima na kutengeneza repoti ya utendaji wa wizara.

repoti hii wanapewa wizara kuandaa majibu na waziri anakuja na timu yake ya wataalamu wanajibu hoja za bunge.

bunge la kufanya kazi kwa mfumo kama huu tunaweza kuliweka juu ya serikali kwa maana wanafanya kazi kwa hoja na si fitina.

lakini huu mfumo wa sasa ni holela mno kiasi ambacho tunaweza kuwapongeza wezi na kuwajibisha wachapakazi kutokana na fitina za kisiasa.

katiba yetu inamuweka waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za serikali lakini katika hali halisi hapa kwetu waziri mkuu ni kama waziri wa kawaida. waziri mkuu hana maamuzi yoyote kwa mawaziri bali likitokea kosa katika wizara waziri mkuu badala ya kumuagiza waziri husika basi anaagiza au kuwajibisha watendaji wa chini moja kwa moja.

tatizo haliko kwa waziri mkuu tu bali chukua mfano shirika lolote. shirika liko chini ya wizara na waziri kateuliwa na raisi, mkurugenzi wa shirika kateuliwa na raisi, mwenyekiti wa bodi kateliwa na raisi na wajumbe wa bodi wameteuliwa na waziri. ni confusion tupu kwa maana shirika linaposhindwa kufanya kazi nani amuwajibishe nani?

ki msingi kinadharia linawezekana lakini kivitendo ni gumu. kwa nini raisi asiteue waziri, waziri ateue bodi na bodi itafute mkurugenzi. kama shirika halifanyi kazi bodi ni kujiangalia na mkurugenzi wao. waziri yeye katika shirika chake ni bodi hivyo kama halifanyi kazi ni kuwajibisha bodi na kama hafanyi lolote raisi au bunge wao wanawajibisha waziri.

tukiondoa mifumo ya zigzag katika uwajibikaji ambao unawachanganya wasimamiaji na kuwafanya wazembe wakapata vichaka vya kujificha na kusingizia uwezekano wa kupiga tambo ndefu kimaendeleo upo.

Back
Top Bottom