Katiba mpya ni muhimu kwa maendeleo na mstakabali wa vizazi vya sasa na vijavyo

Heri ya X Mass.

Tunamshukuru Mungu kwa siku kuu ya leo,na kwa namna ya kipekee kabisa nawapongeza waKristo wote Tanzania na Duniani.

Wakati bado tunaendelea kusheherekea siku hii muhimu naomba tuwarejeshe katika mjadala wa mchakato wa KATIBA MPYA.

Ni hakika KATIBA ya sasa ina mapungufu mengi na tena imepitwa na wakati.
Ukitazama STRUCTURE ya Katiba utaona imejikita katika KUMSIKILIZA,KUMTII,KUMWABUDU,KUMSIFU,KUMNYENYEKEA RAIS wa JMT.

Si vibaya RAIS wa JMT akatengenezewa utaratibu wa kiMungu Mungu tatizo kubwa ni kwamba RAIS wa JMT ni mwanadamu mwenye mapungufu mengi.Akitumia vibaya katiba watu wengi wataumia sana tena sana.Hakuna mahali pa kupinga maamuzi mabaya ya RAIS.Akiamu kutuingiza katika vita tutaingia,akiamua kukwapua fedha za wananchi nje ya utaratibu wa sheria atakwapua hakuna wa kumzuia,akiamua kuingiza jeshi mtaani kutandika wananchi asiowapenda hakuna wa kumkatalia.Viongozi wote wanaapishwa kumtii Raia na si katiba.

Hakuna tatizo iwapo Rais atakuwa malaika lakini kama ni hawa watawala mapenda madaraka hakika sioni Tanzania ikipiga hatua za maana.

KATIBA MPYA ni muhimu sasa kuliko wakati wowote Mwl alituachia katiba mbaya ni wajibu wetu wote kuhakikisha KATIBA MPYA itakayopunguza madaraka makubwa ya RAIS.Itakayo hakikisha uhuru wa Mahakama,Bunge na tume ya uchaguzi.

Ngongo kwasasa KIBANDA MAITI.
Mh mbona uvccm wanasema eti katiba mpya itamsaidia nn bibi alieko kijijin 🤣🤣🤣🤣
 
Hili mbona lilielezwa sana na Jaji Warioba na Wajumbe wake wakati wanakusanya maoni kwa ajili ya kuandaa Rasimu ya Katiba ya Warioba,AU ulikuwa bado MDOGO?

Kukusaidia tafuta nakala ya Katiba hii ya 1977 na Rasimu ya Katiba ya Warioba,ujione mapungufu ya katiba hii ya KALE

Kumbe ww unafata mkumbo na hubanwi na chochote wala lolote Kwa katiba ya sasa!
 
Katiba mpya bila elimu ni sawa na kazi bure.

Ujinga bado ni mwingi sana vichwani mwa watu.
 
Heri ya X Mass.

Tunamshukuru Mungu kwa siku kuu ya leo,na kwa namna ya kipekee kabisa nawapongeza waKristo wote Tanzania na Duniani.

Wakati bado tunaendelea kusheherekea siku hii muhimu naomba tuwarejeshe katika mjadala wa mchakato wa KATIBA MPYA.

Ni hakika KATIBA ya sasa ina mapungufu mengi na tena imepitwa na wakati.
Ukitazama STRUCTURE ya Katiba utaona imejikita katika KUMSIKILIZA,KUMTII,KUMWABUDU,KUMSIFU,KUMNYENYEKEA RAIS wa JMT.

Si vibaya RAIS wa JMT akatengenezewa utaratibu wa kiMungu Mungu tatizo kubwa ni kwamba RAIS wa JMT ni mwanadamu mwenye mapungufu mengi.Akitumia vibaya katiba watu wengi wataumia sana tena sana.Hakuna mahali pa kupinga maamuzi mabaya ya RAIS.Akiamu kutuingiza katika vita tutaingia,akiamua kukwapua fedha za wananchi nje ya utaratibu wa sheria atakwapua hakuna wa kumzuia,akiamua kuingiza jeshi mtaani kutandika wananchi asiowapenda hakuna wa kumkatalia.Viongozi wote wanaapishwa kumtii Raia na si katiba.

Hakuna tatizo iwapo Rais atakuwa malaika lakini kama ni hawa watawala mapenda madaraka hakika sioni Tanzania ikipiga hatua za maana.

KATIBA MPYA ni muhimu sasa kuliko wakati wowote Mwl alituachia katiba mbaya ni wajibu wetu wote kuhakikisha KATIBA MPYA itakayopunguza madaraka makubwa ya RAIS.Itakayo hakikisha uhuru wa Mahakama,Bunge na tume ya uchaguzi.

Ngongo kwasasa KIBANDA MAITI.

Hivi tatizo letu kubwa ni kuwa na katiba mpyaaa au kutokuwa na desturi ya kuiheshimu katibaaa??
Maana watu wanapenda kuongelea kuhusu katiba, huku wakisahau kuhusu utamaduni wa kuitii katiba. Kitu ambacho ni cha muhimu sana.
Mfano, katiba hii ambayo inaonekana kupitwa na wakati na isiyokidhi mahitaji ya sasa, haiheshimiwi. Maeneo ni mengi sana katika katiba hii ambayo hayazingatiwi, lkn hayapewi uzito sana. Binafsi nafikiria, pamoja na msukumo wa katiba mpya, hili la utii wa katiba bila shuruti lizingatiwe. Hili ni muhimu, kuliko katiba.
 
Mpaka hapo umeongea mambo ya kufikirika Tu na mambo ya kisiasa

Turudi kwako personal, Tangu umezaliwa mpaka sasa na umri huo uliona, ulishawahi kupata changamoto yoyote ambayo ilibidi kuishitaki serikali?

Hapo kwenye tume ya uchaguzi, unataka kuwe na maroboti? Au wakina mbowe ndio wakawe wasimamizi wa uchaguzi?

Hata watumishi wa tume wakichaguliwa na wanainchi Kwa kupiga kura still hakuna Jambo litabadilika

Tume inakuwa mzuri vyama pinzani vikishinda ila tume inakuwa mbaya mkishindwa
Nilikuwa na nia ya kuishtaki Halmashaurifulani baada ya kukamilisha kazi na kutokulipwa fedha zangu.Nilipoanza hatua ya kufungua kesi nikakumbana na hizo sheria zinazopitishwa na wabunge wagonga meza.

Usisahau nilichukua mkopo kugharamia mradi na nilipewa certificate zote lakini fedha sikupewa.Kilichofuata ilikuwa kubembeleza na si kudai.Naelewa sana ni kwanini kampuni za nje zinakimbilia katika mahakama za usuluhishi ni kwasababu sheria zetu ni mbovu na hii imesababishwa na katiba mbaya.

Kuhusu tume ya uchaguzi.Nakumbuka sana uchaguzi wa 2020 nilikwnda kupiga kura saa mbili na dakika 17 nilikuta mabox yote yamejaa kura na hapakuwa na watu wengi wala misururu ya kupiga kura.Nakumbuka sana kura yangu nilifanya kuisokomeza kwa kalamu niliyotumia kupiga kura.Ukiweza kuniambia saa 2 na dakika 17 masanduku ya kuhifadhi kura ya Rais,Mbunge na Diwani yalikuwa yamejaa full na wapiga kura ndio kwanza walikuwa wakitoka majumbani nitakuheshimu sana.WaTanzania wanataka kura zao zihesabiwe na kuheshimiwa.

Tunataka matokeo ya Urais yahojiwe Mahakamani na wakurugenzi wasisimamie uchaguzi wowote.
 
Naunga mkono hoja, bila Katiba mpya itakayoundwa itakayoendana na mfumo wa vyama vingi, hatutoboa Hadi mwisho wa Dunia!
Hata ikiwa chama kimoja ila inayowapa raia nafasi ya kuwajibisha na kuwadhibiti viongozi wao ni sawa
 
Hivi tatizo letu kubwa ni kuwa na katiba mpyaaa au kutokuwa na desturi ya kuiheshimu katibaaa??
Maana watu wanapenda kuongelea kuhusu katiba, huku wakisahau kuhusu utamaduni wa kuitii katiba. Kitu ambacho ni cha muhimu sana.
Mfano, katiba hii ambayo inaonekana kupitwa na wakati na isiyokidhi mahitaji ya sasa, haiheshimiwi. Maeneo ni mengi sana katika katiba hii ambayo hayazingatiwi, lkn hayapewi uzito sana. Binafsi nafikiria, pamoja na msukumo wa katiba mpya, hili la utii wa katiba bila shuruti lizingatiwe. Hili ni muhimu, kuliko katiba.
Vyote viwili...
 
Kwanza tuambie katiba ya sasa inatunyima vitu gani Kwa Maisha ya mtanzania mmoja mmoja?

Tuanze na Maisha yako ww, katiba ya sasa inakunyima nn?
Katiba ya sasa inamnyima mtanzania fursa ya kuchagua na kuwawajibisha viongozi muhimu wanaowatawala. Raia hawawachagui na pia hawawezi kuwawajibisha DED, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, RAS, DAS ambao ndio wahusika wakuu katika matumizi ya kodi zao na kutekeleza sheria za nchi.

Nikikosa maji, umeme, hospitali au barabara nzuri nalalamika na kumlaani waziri ambaye yuko huko Dodoma badala ya kwenda kuwadai viongozi wa serikali walio karibu nawe zaidi. Na sababu kubwa haiwezekani kuwadai hawa walio karibu ni kwa sababu hawajawachaguliwa na wananchi.
Hili ni moja tu.
 
Heri ya X Mass.
Mwl alituachia katiba mbaya ni wajibu wetu wote kuhakikisha KATIBA MPYA itakayopunguza madaraka makubwa ya RAIS.Itakayo hakikisha uhuru wa Mahakama,Bunge na tume ya uchaguzi.
Heshima kitu cha bure, katiba ya Mwalimu ilikuwa better 100% kuliko hii iliuokuja kufinyangwa finyangwa!.

Watanzania tunahitaji sana elimu ya katiba, ujue Mwalimu aliacha nini, nini kilikuja kifanyika na kwanini

P
 
Heri ya X Mass.

Tunamshukuru Mungu kwa siku kuu ya leo,na kwa namna ya kipekee kabisa nawapongeza waKristo wote Tanzania na Duniani.

Wakati bado tunaendelea kusheherekea siku hii muhimu naomba tuwarejeshe katika mjadala wa mchakato wa KATIBA MPYA.

Ni hakika KATIBA ya sasa ina mapungufu mengi na tena imepitwa na wakati.
Ukitazama STRUCTURE ya Katiba utaona imejikita katika KUMSIKILIZA,KUMTII,KUMWABUDU,KUMSIFU,KUMNYENYEKEA RAIS wa JMT.

Si vibaya RAIS wa JMT akatengenezewa utaratibu wa kiMungu Mungu tatizo kubwa ni kwamba RAIS wa JMT ni mwanadamu mwenye mapungufu mengi.Akitumia vibaya katiba watu wengi wataumia sana tena sana.Hakuna mahali pa kupinga maamuzi mabaya ya RAIS.Akiamu kutuingiza katika vita tutaingia,akiamua kukwapua fedha za wananchi nje ya utaratibu wa sheria atakwapua hakuna wa kumzuia,akiamua kuingiza jeshi mtaani kutandika wananchi asiowapenda hakuna wa kumkatalia.Viongozi wote wanaapishwa kumtii Raia na si katiba.

Hakuna tatizo iwapo Rais atakuwa malaika lakini kama ni hawa watawala mapenda madaraka hakika sioni Tanzania ikipiga hatua za maana.

KATIBA MPYA ni muhimu sasa kuliko wakati wowote Mwl alituachia katiba mbaya ni wajibu wetu wote kuhakikisha KATIBA MPYA itakayopunguza madaraka makubwa ya RAIS.Itakayo hakikisha uhuru wa Mahakama,Bunge na tume ya uchaguzi.

Ngongo kwasasa KIBANDA MAITI.
Well
 
Naunga mkono hoja na nasisitiza, Katiba Mpya ni hitaji la kila raia hata mafisadi ili waendelee kufaidi pesa walizozichuma!
 
Katiba ya sasa inamnyima mtanzania fursa ya kuchagua na kuwawajibisha viongozi muhimu wanaowatawala. Raia hawawachagui na pia hawawezi kuwawajibisha DED, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, RAS, DAS ambao ndio wahusika wakuu katika matumizi ya kodi zao na kutekeleza sheria za nchi.

Nikikosa maji, umeme, hospitali au barabara nzuri nalalamika na kumlaani waziri ambaye yuko huko Dodoma badala ya kwenda kuwadai viongozi wa serikali walio karibu nawe zaidi. Na sababu kubwa haiwezekani kuwadai hawa walio karibu ni kwa sababu hawajawachaguliwa na wananchi.
Hili ni moja tu.

Hayo mnayoyataka sasa inchi itakuwa haitawaliki kwamba kama maji hakuna ww raia uwe na uwezo wa kumfukuza kazi Mkurugenzi hahaha

Ishu ya uchaguzi ni utashi wa watu Tu, hata kukiwa na katiba mpya kama watu sio wazalendo watachukua ela za watu na watafanya cheating Tu,

Coz katiba mpya haiwez kutoa rushwa wala haiwez kufanya vipato vyetu viwe sawa

So mwenyewe pesa atashinda uchaguzi tu

Remember tuko Africa
 
Back
Top Bottom