Katiba Mpya ni muhimu kwa sasa

Katiba Mpya ni muhimu kwa sasa

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Ukisema hatA kama ulikuwa ni CCM kindakindaki, unakuwa mpinzani. Unatakiwa uwe mnafiki kusifia kila kitu
Hivi;-

Kuonyesha nyala za serikali ndio kuifungua Nchi

- Kuonyesha hazina yako ndo kuvutia wawekezaji tutaibiwa mpaka tukome na hiyo faida tunayoitegemea itatupa majuto. Mungu ibariki Loyal tour film.

Tulipofikia bila kumunginya maneno KATIBA MPYA NI MUHIMU tunawaambia watumishi mnaofurahia mseleleko kuleni lakini hiyo ni pelemende ya danganya toto.

KATIBA NI YA MUHIMU SANA KWA SASA
 
1653252859853.png

Mkono ni wa mwanamke ambae ana dhamana na kuku aliye mezani. Bangili za mwanamke huyu ni za kijani na kipande cha kuku amepewa mpiga kelele. Ni wazi kuwa hawezi kupiga kelele akiwa na kipande cha nyama mdomoni.
 
Katiba si suruhisho la matatizo nchini, suruhisho ni viongozi kufuata sheria na kuitii katiba iliyopo, kama hii wameshindwa tii hata hiyo mnayopigia kelele hawawez kutii, kwanza wengi mnaodai katiba wenyewe hamjui kwann mnadai, tukiwauliza hii ya sasa inamapungufu gan hamjui zaidi ya kufuata mkumbo wa hao wachumia tumbo wenu wanaotamani kuingia ikulu....
 
Hakuna misingi inayowalazimisha viongozi kutii sheria. Nayo ni katiba. Kama una kataa katoba bora na wakati huo huo unataka utawala bora basi unajidanganya.

Mahakama haiko huru uhuru wake unaanzia kwenye katiba.

IGP hayuko huru. Uhuru wake unaanzia kwenye katiba. Bunge haliko Huru Uhuru wake unaanzia kwenye katiba. Sasa hao viongozi unaosema watafata sheria na katiba iliyopo wataanzia wapi?
 
Kutii sheria sio swala la katiba ni utawala bora ni swala la mtu, na ndio sababu kuna jela na mahakama hata kwa hizo nchi zinazobadili katiba kila siku
 
Back
Top Bottom