Ndugu wanabodi,
Assalaam alaykum.
Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.
Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.
Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.
Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.
Wakatabahu,
HK.
Mi naomba hoja ya kiswahili kutumika kama lugha ya Taifa litazamwe vizuri na ikibidi libadilishwe. Katika Mazingira ya sasa siamini kuwa lugha ya kiswahili ina nafasi ya kutuvusha kutoka hapa tulipo kimaendeleo kwenda tunakotaka.Tuachane na Utaifa na Pride isiyokuwa ya msingi na tuseme kwa pamoja kwamba kiswahili kitaendelea kubaki kama lugha yetu mama inayotuunganisha wote lakini haiwezi kuwa official language kinaturudisha nyuma kwa sababu zifuatazo:
i)Watoto wa walalahoi kuwa victims: Wakati wanasiasa wanapitisha kiswahili kuwa lugha rasmi watoto wao wanawasomesha international schools na nje ya nchi, Ulaya na Marekani.Wakirudi kwenye soko la ajira mtoto wa mlala hoi hana nafasi,siku zote atakuwa chini sababu hawezi kuongea kingereza, chukulia mfano kazi za EAC community, AU, UN, Makampuni ya kigeni nk
ii)Kutengeneza makundi katika jamii; kama nilivyosema hapo juu, kundi la watoto wa makabwela waliosomea shule za kizalendo wasioweza kuimudu lugha ya Kiingereza who are looked down upon in the employment market vs watoto wa vigogo na matajiri waliosomeshwa nje ya nchi/English medium schools wanaoimudu kiingereza, hivyo wanaofikiriwa kwanza katika soko la ajira, wenye confidence, exposure
iii)Matumizi mabaya ya rasilimali:Nasema ni matumizi mabaya ya rasimilimali kufikiria kubadilisha mfumo kuwa wa kiswahili, mfumo ambao umetushinda kubadilisha tokea miaka 50 tulipopata uhuru ni kujidangaya kufikria kuwa tutaubadilisha leo.Kwa maana nyingine ni kutanguliza uzalendo upofu(blind patriotism) au Utaifa upofu(blind nationalism) Usiokuwa wa msingi.Hii tulitakiwa tufanye na tufanikishe right after independence kama walivyofanya nchi za asia, china,korea, japan nk lakini sio sasa.Huu ni muda wa kufocus on global integration so as to match the technological pace the world is today.We need to abandon Swahili very quick and fast in order to focus on English as a national language and medium of communication.That is the only way we can match up the pace, kiswahili is a big backwardness towards those goals.
iv)Low Self esteem problem:Ni ukweli usiopingika kuwa kutokumudu kiingereza vizuri kinachangia sana katika hili sana sana katika soko la ajira la dunia.Tumeona jinsi ambavyo watanzania wanapewa second priority kwenye makampuni ya kigeni kulinganisha na wakenya, waganda, wagana nk. Simaanishi kuwa hakuna wataanzania wanaobahatika kupata ajira nzuri katika makampuni ya kigheni lakini ni wachache na kikwazo kikubwa ni very low self esteem we posses due to our inability to express our-self well in English.Let's say enough with politics and pride,let's be realistic. English is the solution!!...Kusisitiza matumizi ya kiswahilili wakati watoto wao wanasoma ulaya na marekani ni ufisadi mwingine wa kimfumo.Be ware!!