Katiba Mpya Tanzania: Je, Tatizo Liko Kwenye Katiba au Kwenye Watu Wanaoiendesha?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,530
Reaction score
3,422
Tanzania imekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

Wapo wanaoamini kuwa baadhi ya changamoto za kisiasa, uwajibikaji na mgawanyo wa madaraka zinatokana na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa.

Lakini wengine wana hoja kwamba hata Katiba nzuri zaidi inaweza kushindwa kama viongozi na wananchi hawatazingatia misingi ya utawala bora, haki na uwajibikaji.

Swali la mjadala:

Kama Tanzania ikipata Katiba mpya kesho, je maisha ya mwananchi wa kawaida yatabadilika kwa kiasi kikubwa? Au tatizo kubwa ni namna watu wanavyotumia mamlaka yaliyopo?​
 
Katiba ya sasa ina loopholes nyingi sana zinazomgeuza kiongozi kuwa mungu mtu, na viongozi wetu nao wakiona hizo nafasi wanazitumia to the maximum.

Katiba mbovu inazaa viongozi wabaya, na viongozi wabaya wanailinda Katiba mbovu ili waendelee kula kujinufaisha.
 
Exactly, leo unanifuriasha sana na ndio maana lile pendekezo langu linaingia kuziba loopholes hizo kwa namna ya kipekee kabisa.

Kwanza kabisa Muundo wa dola wenye mihimili miine, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa (mlinzi wa misingi yote ya taifa, mtoa tathmini ya hali za kitaifa na mtoa muongozo au amri pale "Kanuni ya ulinganifu wa nguvu za kikatiba zilizowekwa kwenye katiba hiyo na sheria ya usimamizi wa taifa inapooingia" ni nini hicho Kanuni za ulinganifu wa nguvu za kikatiba, ni kama mzani wa nguvu za kikatiba kulingana na hali ya taifa, mfano Pale usalama wa taifa unapolindwa kisha hapo hapo demokrasia ya kisiasa inachukuliwa, na maadui wa njee utumia jukwaa hilo hili kudhoofisha usalama wa nchi, hapa nguvu ya kikatiba italiweka kwamba Demokrasia ya kisiasa iendelee isipokuwa usalama wa taifa utawekwa mbele zaidi hili tuqe salama then turudi kwenye msingi wetu, naomba niseme wazi hapa kwamba maadui utumia njia nyingi kudhoofisha taifa fulani hivyo swala si kudhibi kile kilichokuwa ni miongoni mwa miaingi ya taifa swala ni kutambua kuwa mpaka ni huu pale hili linapotomea.

Pia naomba nisemw kwamba kwenye ibara zinazohusu usalama wa taifa imewekwa falsafa kwamba "Haki za msingi za kibinadamu si tishio kwa usalama wa taifa na kinyume chake tishio la usalama wa taifa linaqeza kufichwa chini au nyuma ya haki hizo hivyo basi TISS na kwa kuzingatia Tathmini ya Baraza kupitia ofisi yake ya Tathmini ya usalama wa taifa wana wajibu kutenganisha kwa umakini kile kinachoitwa haki a kile kinachoitwa tishio na hapo ndipo tishio litadhibitiwa na haki za msingi za kibinadamu kutokuvunjwa wala kudhoofishwa."

2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania ( ni serikali moja tu ya pamoja, yenye jukumu la utekelezqji wa sera za serikali na uendelwvu wa taifa)

3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania (lenye jukumu la uwakilishi wa wananchi, Kutunga sheria, kupitisha bajeti na mijadala ya uendelevu wa taifa ambapo katika dhamiri mbali mbali za wananchi na maoni yao ya namna taifa liende na dhamiri itakayopata kipaumbele zaidi kwa ndiyo itakayo tawala, "hapa maana yake dhamiri ni maoni ya nda kile ana amini kuwa ndio njia bora ya uendelwvu wa taifa hivyo wananvhi kuweka wawakilishi wao wa kibunge ni kwaajili ya kutafuta dhamiri itakayokuwa na hoja nzito za kupewa kipaumbele".

4. Mahakam ya jamhuri ya muungano wa tanzania (yenye jukumu la kutafasiri katiba na sheria za nchi, kutoa uhamuzi wa migogoro ya kikatiba na kisheria, na kutoa hukumu zote zinaloitaji mamlaka ya Mahakama,

muundo huu unafunga mianya yote ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma na mengineyo na hapo ndipo uadilifu, uwazi na uwajibikaji utakapoibuka kwa asilimia zaidi ya 90%

Rasimu ya katiba yenye muundo uliotajwa hapo juu inapatikana katika tovuti ya www.katibampya.com

Tembelea tovuti tajwa, soma pendekezo hilo hasa ibara ya 98 mbaka 116 ilizozungumzia kuhush baraza la uaimamizi wa taifa kiundani kuanzia muundo, mamlaka yake, mipaka na mengineyo, kisha njoo na hoja za kina kama ni kuunga mkono pendekezo hilo la katiba au kukosoa.
 
Tanzania imekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

Wapo wanaoamini kuwa baadhi ya changamoto za kisiasa, uwajibikaji na mgawanyo wa madaraka zinatokana na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa.

Lakini wengine wana hoja kwamba hata Katiba nzuri zaidi inaweza kushindwa kama viongozi na wananchi hawatazingatia misingi ya utawala bora, haki na uwajibikaji.

Swali la mjadala:

Kama Tanzania ikipata Katiba mpya kesho, je maisha ya mwananchi wa kawaida yatabadilika kwa kiasi kikubwa? Au tatizo kubwa ni namna watu wanavyotumia mamlaka yaliyopo?​
Katiba hii inaweza.
Tembelea www.katibampya.com
 
Pamoja na katiba ya sasa kuwa na mapungufu, tatizo kubwa lipo kwa watu (viongozi na wananchi wanaoongozwa).
Viongozi hutokana na wananchi, hivyo ujinga wa wananchi huzalisha viongozi wajinga au wa hovyo.
Kiongozi mpuuzi hawezi kuvumiliwa na wananchi wanaojielewa
 
Kama hatuta kuwa na utamaduni wa uwajibikaji hata ije katiba mpya mambo ni yale yale tuu
Alafu hivi kwan lazima tuwe na katiba ya maandishi
Katiba inaweza kuweka nidhamu kama sehemu yake miwingi ya taifa, hivyo maadili ya taifa yanakuwa si jambo la ahadi au hamu ya kiongozi binafsi bali ni jambo la lazima, ndio maana pendekezo langu la katiba linaingia kutoa jibu la hoja yako kwa asilimia zaidi ya 75%

Najua unajua wapi inapatikana rasimu hiyo ya katiba, kwaiyo nakukalibisha kwa hoja pale utakapoona ibara fulani haijatoa jibu la kina kwenye hoja zako nami nitakujibu kulingana na rasimu yenyewe itamkavyo.
 
Hivi kwani ni lazm kuwa na katiba ya maandishi
 
Haihitaji maelezo mengi zaidi ya ukweli kuwa takwa la kuandika katiba upya ni la msingi na linahitajika sasa.

Katiba inatakiwa kuandikwa upya kwa kuzingatia mahitaji ya sasa baada ya miaka sitini, Mchakato unatakiwa uwe na kazi ya kuichambua Katiba iliyopo na kuboresha pale inapopwaya, kuichambua upya ile rasimu ya Warioba kuingiza yale maoni ya wananchi yaliyokwisha kutolewa na kuandika mapya yaliyojitokeza.

Ile Katiba pendekezwa iliyochakachuliwa na chama tawala isitumike kama mfano wa katiba tunayoitaka, kwa sababu ina wigo wa kulinda makundi yanayoogopa mabadiliko.
 
Katiba ya sasa ina loopholes nyingi sana zinazomgeuza kiongozi kuwa mungu mtu, na viongozi wetu nao wakiona hizo nafasi wanazitumia to the maximum.

Katiba mbovu inazaa viongozi wabaya, na viongozi wabaya wanailinda Katiba mbovu ili waendelee kula kujinufaisha.
Uko sahihi
 
US wana katiba nzuri, lakini sasa hivi kuna vilio kila kona wakilalamikia utendaji wa ICE kwa madai ya ukiukwaji wa katiba.

Trump, kama hawa wakwetu, anaipuuza katiba.
Kama jamii haina utamaduni wa uwajibikaji na kujituma kuleta maendeleo hata ije katiba ni kazi bure

Maendeleo hayana chama - RIP JIWE
 
Haihitaji maelezo mengi zaidi ya ukweli kuwa takwa la kuandika katiba upya ni la msingi na linahitajika sasa.

Katiba inatakiwa kuandikwa upya kwa kuzingatia mahitaji ya sasa baada ya miaka sitini, Mchakato unatakiwa uwe na kazi ya kuichambua Katiba iliyopo na kuboresha pale inapopwaya, kuichambua upya ile rasimu ya Warioba kuingiza yale maoni ya wananchi yaliyokwisha kutolewa na kuandika mapya yaliyojitokeza.

Ile Katiba pendekezwa iliyochakachuliwa na chama tawala isitumike kama mfano wa katiba tunayoitaka, kwa sababu ina wigo wa kulinda makundi yanayoogopa mabadiliko.
Sawa kabisa, tuweke na nyongeza ya elimu kwa watu ili wahakikishe katiba inapata utii wa juu kwa kuwashughulikia wanaoivunja.
 
Tanzania imekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

Wapo wanaoamini kuwa baadhi ya changamoto za kisiasa, uwajibikaji na mgawanyo wa madaraka zinatokana na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa.

Lakini wengine wana hoja kwamba hata Katiba nzuri zaidi inaweza kushindwa kama viongozi na wananchi hawatazingatia misingi ya utawala bora, haki na uwajibikaji.

Swali la mjadala:

Kama Tanzania ikipata Katiba mpya kesho, je maisha ya mwananchi wa kawaida yatabadilika kwa kiasi kikubwa? Au tatizo kubwa ni namna watu wanavyotumia mamlaka yaliyopo?​
Kuna katiba bora sana ilikuwa ya chadema ila mbowe iliibaka akaitumia kama taulo na hapa lisu ataitumia vilevile

USSR
 
Tanzania imekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

Wapo wanaoamini kuwa baadhi ya changamoto za kisiasa, uwajibikaji na mgawanyo wa madaraka zinatokana na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa.

Lakini wengine wana hoja kwamba hata Katiba nzuri zaidi inaweza kushindwa kama viongozi na wananchi hawatazingatia misingi ya utawala bora, haki na uwajibikaji.

Swali la mjadala:

Kama Tanzania ikipata Katiba mpya kesho, je maisha ya mwananchi wa kawaida yatabadilika kwa kiasi kikubwa? Au tatizo kubwa ni namna watu wanavyotumia mamlaka yaliyopo?​
Cha kwanza ni katiba, maana katiba ndiyo inampa rais nguvu ambayo inafanya awe juu ya mihimili mingine yote hivyo kwa kujiona hawajibishwi kikatiba anakuwa na nguvu ya kuamua chochote yeye na genge lake ambalo linatembelea mgongo wa huyu anaye lindwa na katiba
 
Embu tupe hoja zako za taifa bila katiba ya maandishi hili tuelewe unamaana gani...?
Sitaki kukukosoa kwa sasa nasubiri hoja zako ndipo nione je, napaswa kuziunga mkono au kuzikosoa.
Katiba kama ya UK
KIjikitabu hawana wana ongozwa na mila desturi etc
 
Back
Top Bottom