Katiba Mpya tutumie ile ya Warioba badala ya kuteketeza pesa

Tunahitaji katiba mpya haraka la sivyo matrilioni yataendelea kupotea kama ilivyooneshwa kwenye ripoti ya CAG.
Wanaoyakwapua nao wanataka kazi iendelee. Msigishano uko hapo. Kupata katiba mpya yenye tuyatakayo hakuwezi kuwa Kwa lelemama.
 
Tunza posts zako unapoendelea kusubiria dodo kwenye mnazi
Niliiona KATIBA mpya Tanzania kabla Yako. 2026 itakamilika mchakato.

Na ndicho kilichonileta JF Kwa mara ingine.

Tusubiri.
 
Unayemuwazia Hana term mbili ni Moja.

Rudi tena kufikiri sahihi.
Kwa katiba iliyopo aliyepo kutoka madarakani labda aamue mwenyewe.

Wewe unamwona ana nia ya kuachia ngazi kwa hiari yake au kwa wito wa Mdude?
 
Kwa katiba iliyopo aliyepo kutoka madarakani labda aamue mwenyewe.

Wewe unamwona ana nia ya kuachia ngazi kwa hiari yake au kwa wito wa Mdude?
Nimekwambia Rudi nyuma Anza UPYA calculations.

Unadhani ni coincidence kikosi KAZI kuyeyuka?
 
Nimekwambia Rudi nyuma Anza UPYA calculations.

Unadhani ni coincidence kikosi KAZI kuyeyuka?

Kkikosi kazi ulikisoma au ilikuwa kukisikia tu?

Your browser is not able to display this video.

KIkosi kazi kilifanya kazi yake ambayo pia si mama au CCM waliyoipenda.
 
Kuna mambo mengi ya kuboreshwa kwenye rasimu ya warioba. Ile ikipitishwa kama ilivyo, itatuletea migogoro mingine baada ya muda mfupi.
 
Yaani Tume ya Warioba ilishamaliza kazi. Ila tuna shida! Kuuza uta wa mtu ni sawa na ushoga tu.
 
Yaani Tume ya Warioba ilishamaliza kazi. Ila tuna shida! Kuuza uta wa mtu ni sawa na ushoga tu.

Matumizi ya fedha za umama kibadhirifu huitwa kulamba asali. Kwenye kulamba asali wabunge wote ccmna upinzani ni baba mmoja mama mmoja. Nyerere akiita maji ga nyanja!

Kwani uliwahi kuwasikia wapinzani au CCM wapi mwaka Gani bungeni wakiongelea kupunguzwa maslahi yao binafsi kupunguzwa?

Kwenye hoja ya kulamba asali wabunge wa vyama vyote huungana pamoja. Hoja ya maslahi yao ni muhimu zaidinya maslahi ya taifa.

Hii nchi kama ni ukombozi bado sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…