Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,319
wacha kuweka upuuzi wako..hapa kwa heading kubwa bila ya source ya habari yenyewe.
kuwangangania kwa chuki waislam ...tutabaki hivyo hivyo mambo muhimu yanayoleta umaskini nchii hayataondoka kwa kushabikia udini.
waislam kama walivo wakristo na wengineo wanayo haki ya kuchangia upatikanaji wa katiba mpya.
kila kundi lina mlengo yake lakini mwisho wa yote lengo ni kupatikana katiba ambayo lengo kubwa litakuwa
kuna mengi ambayo waislam wamesema ili katiba ilinde haki za raia wake na kutoa fursa sawa basi yanapaswa kuwemo ndani ya katiba mfano
- kulinda haki za raia wote bila ya kubagua kwa misingi ya dini,ukabila,ukanda ama rangi au jinsia.na kuwa serikali itakuwa mwajiri wa bila ya ubaguzi
- haki ya kuabudu italindwa ndani ya katiba na mengineyo
ama sula la OIC hili sio suala la katiba ni suala uamuzi tu wa serikali...kama kuna umuhimi wa kujinga ama la..na kama zanzibar wajiunge ama la hili ni suala ambalo pia litaamuliwa na katiba kwani Tanganyika wanakataa kwa mashinikizo lakini katiba hio hio basi itambue imeungana na zanzibar amabyo ina waislam wengi hivyo ina maslahi na jumuia za waislam dunian, hii lazima ndani ya katiba iepo na lazima ipewe haki hii ya kujiunga na jumuiya kama hizi.
- suala la kurejesha mahkama ya kadhi -suala hili linahusu ndoa za waislam inajulikana wazi waislam wana sheria zao za ndoa na ilii mashauri yao ndoa na mirathi yapate uhalali wa kisheria basi ni lazima kuwepo na mahakama inayotambiliwa kisheria sio suala la udini.ni kustahamiliana katika jamii hii ambayo makundi haya mawili yanakurubiana kwa wingi na maingiliano.wengi ya makundi ya wakristo waliobatizwa miaka ya 60 na 70 basi familia zao ni mchanganyiko wa dini hizi..
- suala la kadhi lina kuzwa sana na viongozi wa makanisa kuliko uhalisia wake..hili kwa vile ni lazima katika maisha ya muislam basi tustahamiliane na hili sio lazima liwemondani ya katiba lakini sheria inaweza kutongwa kuanzisha mahakama hii. na ukweli halihusu watu wengine bali kazi yake ni mashauri ya ndoa ya kiislam.
- kama katiba lengo lake ni kuleta usawa basi sheria zote kandamizi au zile sheria ambazo zimeletwa kwetu kwa malengo maaulum ya kuwa kandamiza makundi fulani ndani ya nchi..mfano wa hapa ni sheria ya Ugaidi...hii sheria imeletwa kwa lengo la kuwakandamiza waislam.ndani ya katiba mpya hii lazima iondoke
- japo serikali haina dini lakini itambue raia wake ni waumin wa dini tofauti , hivyo kama serikali inasaidia kwa namna yoyote ile makudi ya dini au taasisi ya dini basi iwekwe fumula maalum ya usawa kabisa kwamba ni kiasi gani.kuliko sasa hivo misaada ya serikali inalenga zaid upande mmoja
- ama suala lingine ni kutambua kuwa tanzania ni nchi huru hivyo haifungamani na nchi yoyote duniani kiitikadi ama kimsimamo
- rasilimali zote ni mali ya watanzania hivyo mikataba yote iwe ya uwazi na taifa lifaidi zaidi kwa mkataba wowte wa madini na mafuta
- kuwe na bunge tafauti la muungano ambalo litajumiasha wawakilishi na wabunge wa Tanganyika (kama ni 100 basi kila upande uwe 50) hili ndio lipitishe sheria za muungano.sio kama sasa hivi wabunge wa znz wanapiga kura kupitisha bajeti ya magufuli ..hhaaaaa mpaka unaona kinyaaa ...watu kama hawaoni ukweli hivi magufuli na wizara yake inahusu nini na mbunge wa michweni pemba? hivyo bunge la muungano liwe tofauti kujadili mambo ya muungano na yale ya kina magufuli basi yajadiliwe na wabunge wa Tanganyika..ima hili nalo litategemea Hali ya mungano baada ya katiba mpya
ama kuhusu vyama vya dini sijasikia madai hayo ila hii ni yale matongo tongo aliyonayo mleta mada....
lakini hapa katiba lazima ikataze na ipige marufuku vyama vyote vya kidini ama kikanda ama kikabila ...na lazima katiba za vyama uongozi wao uwe wa kitaifa usiwe wa kimkoa
mwisho mleta hoja wacha chuki kwa waislam ....
Umejitahidi sana kutoa maelezo yako,lakini nashindwa elewa tatizo lako liko wapi? Mahakama ya kadhi ni swala la ibada kwa waislam,kama imamu huchaguliwa na waislam kwanini kadhi asichaguliwe na waislam wenyewe na aendeshe hukumu ziwahusuzo waislam hadi serikali iwaanzishie hiyo mahakama,kuna nini hadi iwe lazima mahakama ya kadhi ianzishwe na serikali ?
OIC, Organization of Islamic ... kama sijakosea, kama ni organization ya Islamic ... TZ sio Isramic, kwa nini ijiunge kama nchi ? malengo na madhumuni ya OIC yanahusu uendelezaji wa UISLAM, serikali ya TZ isiyo na dini inahusikaje na uendelezaji wa UIslam ? hata kama kuna baadhi ya malengo yasiyohusu dini kama misaada au lah,hiyo haitoshi kuifanya nchi isiyo ya kiislam kujiunga na taasisi ambayo ni ya kidini per se.
Misaada ya serikali hailengi upande mmoja kama unavyojaribu kudanganya ndugu,serikali inatoa ruzuku kwenye mahospitali yanayoendeshwa na makanisa kwa makubaliano ya kutoa huduma kwa niaba ya serikali,na si kwa wakristo tu,imesemwa taasisi ya agha khan inanufaika nayo ni ya kikristo ?
Bado serikali haijawanyima ruzuku waislam kama wanaweza endesha taasisi kama hospital,unajua kuwa hilo si moja ya malengo ya Uislam,kama serikali ingekuwa inatoa fedha kuendeshea sunday school,naamini na waislam wangepata za kuendeshea madrasa. Lakini sivyo,serikali inafadhili miradi kusaidia jamii kiafya inayoendeshwa na taasisi za kidini sio kikristo tu