Katiba mpya,wananchi na wadau tuangalie maeneo haya kwa kina - Tanzania kwanza

Katiba mpya,wananchi na wadau tuangalie maeneo haya kwa kina - Tanzania kwanza

Joined
Feb 25, 2012
Posts
419
Reaction score
2,169
Other things Remain Constant,
Vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba TUISOME RASIMU, TUTAFAKARI, TUJADILI, TUTOE MAONI KWA KUITANGULIZA TANZANIA MIOYONI MWETU. SIO KULENGA KULIKOMOA KUNDI FULANI AU UPANDE FULANI WA NCHI.
Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:

A) Ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... ktk maeneo yao.

Pili ibara ya 227(1) kutakuwa na Jeshi la Polisi la jamuhuri ya muungano litakuwa na jukumu la ulinzi wa wa watu wao, Ibara ya 232 inaongelea vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao Pia 233 (1) kutakuwa na idara ya usalama wa Taifa wa jamuhuri ya muungano ... Ibara 235 inasema bila kuathiri masharti ya katiba hii, nchi washirika wanaweza kuanzisha idara za usalama.

Analysis, swala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo nirahisi vikosi vya muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa.

B) ibara ya 217(1) kutakuwa na benki kuu ya jamhuri ya muungano na majukumu yameainishwa...... ibara ya 218 serikali washirika zitakuwa na BENKI ZAO zakusimamia sera za kifedha na kibenki
Analysis; hakuna namna unaweza kuwa na monetary policy tatu ktk nchi moja ukafikia malengo. Ni kama gari kuwa na sukani tatu na madreva wa tatu at per, the will miss the right direction.

C) ibara ya 1(1), 1(2) na 57(1) zinazungumzia shirikisho, nionavyo mimi ni makosa. Jamhuri ya muungano ni nchi sio shirikisho. Kupata shirikisho ni sharti kwanza nchi washirika tupige kura kama tunataka kujiunga na shirikisho au laa kama tulivyokataa la afrika mashariki.

Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia bila kuangalia mungano wa serikali mbili kuwa ni msimamo wa CCM. TANZANIA BARA ITAKUWA NA SERIKALI MBILI YAANI YA BARA NA YA MUUNGANO ambayo haitahusika na maisha ya watanzania bara kupitia mambo yenye mguso wa moja kwa moja. NITAWALETEA SIKU NYINGINE IMPLICATION ZAKE KIUCHUMI KWA TAKWIMU NA JINSI KODI ITAKAVYOPANDA KUKIDHI NYONGEZA YA SERIKALI. BE BLESSED

Ha ha ha! Kwa mamlaka mliyo nayo kama "chama tawala" hamasisheni watanzania wakubali mfumo wa serikali moja hapo nitawaona wa maana. Otherwise, Serikali Mbili (kama ilivyo sasa) ni usanii uliopindukia. Kama Serikali tatu haziwezekani then bora Muungano uvunjike kuliko kuendelea na huu usanii uliopo. By the way, inaeleweka ni kwanini CCM inang'ang'ania sana huu muundo uliopo.

OMBI KWA MODS: Tunaomba kile kitufe cha "dislike" kirudi; hii mada inatia kichefu chefu ukizingatia nia ovu ya chama cha mleta mada kuhusu suala la Muungano na Katiba kwa ujumla wake.
 
Huyu Pimbi, mbona leo kuna vikosi kule Zanzibar na hatujapigana , am hujui kuwa kuna KMKM, na vingine? Kamtoe Ludovick magereza kwanza.
 
Kama unavyosema ni kweli hatuwezi kuwa na monetary policy tatu... Hapa mpango mzima ni Serikali moja tu

kama wale wa Zenji hawawezi tunasema let Zanzibar go, sitaki serikali tatu, Gari itakuwa vipi na misikanio mitatu!?

Mpango mzima ni Tanzania moja...
 
Tunaisoma rasimu hii ya katiba na kuitolea maoni japokuwa kuna watu wameshaanza kukaririshwa kwa rasimu mbadala mfn katika baraza la katiba wilaya ya tarime leo trh8.7.2013 ndio ilikuwa tarehe ya kuanza kuchambua rasimu/kutoa maoni mbaya zaidi imeahilishwa bila sababu za msingi matokeo wale wajumbe wote wanaotokana na chama tawala wameitwa na kupewa maelekezo ya chama sanjari na rasimu yao waisome na hii ndio itawapa dira hasa katika kuijadili rasimu ya tume kitu ambacho kinaweza kuathili mchakato mzima wa rasimu hapa wilayani
 
Mimi ni TANGANYIKA KWANZA mengine baadae.

Lakini kwa jinsi inmavyoonekana Tanzania inaweza kuwa na majeshi ya ulinzi matatu, hapo ndio matatizo yatakapoanzia kwa sababu kila mtu ataiona ana comand upande wake.

Mimi nadhani ni vyema kila nchi ijetegemee kivyake na tubaki marafiki kama kenya na sie . ... Mbona EAST AFRICA ilivunjika?
Mbona Sudan imegawanyika?

Hizi ndoa zenye manung'uniko kila kukicha ndio matokeo yake siku moja unakuta mzazi mmoja kwatilia sumu familia nzima ili wote wakose.

TANGANYIKA KWANZA!
 
Huyu bwana Mwigulu Nchemba kila ninaposoma post zake akili yangu inanipeleka Arusha kwa wale watoto na akina mama waliokufa kwa lile bomu mkutano wa Chadema. Hivi anadhani watu tutasahau?

Watu wengine wana roho ngumu kweli kweli, wamesingizia watu innocent kedi za ugaidi na kuwalaza mahabusu miezi zaidi ya mitatu at the cost ya familia zao na watoto wao, wameua watu na na kuvuruga maisha ya wazazi na wengine kufanywa yatima, vilema na kuwa mzigo kwa familia zao milele halafu unakuja na distractions za katiba mpya.

Ujasiri watu hawa wanautoa wapi?
 
other things remain constant,
vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba tuisome rasimu, tutafakari, tujadili, tutoe maoni kwa kuitanguliza tanzania mioyoni mwetu. Sio kulenga kulikomoa kundi fulani au upande fulani wa nchi.
Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:

A) ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na jeshi la wananchi wa tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... Ktk maeneo yao.

Pili ibara ya 227(1) kutakuwa na jeshi la polisi la jamuhuri ya muungano litakuwa na jukumu la ulinzi wa wa watu wao, ibara ya 232 inaongelea vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao pia 233 (1) kutakuwa na idara ya usalama wa taifa wa jamuhuri ya muungano ... Ibara 235 inasema bila kuathiri masharti ya katiba hii, nchi washirika wanaweza kuanzisha idara za usalama.

Analysis, swala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo nirahisi vikosi vya muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa.

B) ibara ya 217(1) kutakuwa na benki kuu ya jamhuri ya muungano na majukumu yameainishwa...... Ibara ya 218 serikali washirika zitakuwa na benki zao zakusimamia sera za kifedha na kibenki
analysis; hakuna namna unaweza kuwa na monetary policy tatu ktk nchi moja ukafikia malengo. Ni kama gari kuwa na sukani tatu na madreva wa tatu at per, the will miss the right direction.

C) ibara ya 1(1), 1(2) na 57(1) zinazungumzia shirikisho, nionavyo mimi ni makosa. Jamhuri ya muungano ni nchi sio shirikisho. Kupata shirikisho ni sharti kwanza nchi washirika tupige kura kama tunataka kujiunga na shirikisho au laa kama tulivyokataa la afrika mashariki.

Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia bila kuangalia mungano wa serikali mbili kuwa ni msimamo wa ccm. Tanzania bara itakuwa na serikali mbili yaani ya bara na ya muungano ambayo haitahusika na maisha ya watanzania bara kupitia mambo yenye mguso wa moja kwa moja. Nitawaletea siku nyingine implication zake kiuchumi kwa takwimu na jinsi kodi itakavyopanda kukidhi nyongeza ya serikali. Be blessed

yaani kwa matendo yako mayu hata maadishi yako huwa sisomi!
Kuna siku utayalipa tu tena duniani !
 
Other things Remain Constant,
Vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba TUISOME RASIMU, TUTAFAKARI, TUJADILI, TUTOE MAONI KWA KUITANGULIZA TANZANIA MIOYONI MWETU. SIO KULENGA KULIKOMOA KUNDI FULANI AU UPANDE FULANI WA NCHI.
Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:

A) Ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... ktk maeneo yao.

Pili ibara ya 227(1) kutakuwa na Jeshi la Polisi la jamuhuri ya muungano litakuwa na jukumu la ulinzi wa wa watu wao, Ibara ya 232 inaongelea vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao Pia 233 (1) kutakuwa na idara ya usalama wa Taifa wa jamuhuri ya muungano ... Ibara 235 inasema bila kuathiri masharti ya katiba hii, nchi washirika wanaweza kuanzisha idara za usalama.

Analysis, swala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo nirahisi vikosi vya muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa.

B) ibara ya 217(1) kutakuwa na benki kuu ya jamhuri ya muungano na majukumu yameainishwa...... ibara ya 218 serikali washirika zitakuwa na BENKI ZAO zakusimamia sera za kifedha na kibenki
Analysis; hakuna namna unaweza kuwa na monetary policy tatu ktk nchi moja ukafikia malengo. Ni kama gari kuwa na sukani tatu na madreva wa tatu at per, the will miss the right direction.

C) ibara ya 1(1), 1(2) na 57(1) zinazungumzia shirikisho, nionavyo mimi ni makosa. Jamhuri ya muungano ni nchi sio shirikisho. Kupata shirikisho ni sharti kwanza nchi washirika tupige kura kama tunataka kujiunga na shirikisho au laa kama tulivyokataa la afrika mashariki.

Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia bila kuangalia mungano wa serikali mbili kuwa ni msimamo wa CCM. TANZANIA BARA ITAKUWA NA SERIKALI MBILI YAANI YA BARA NA YA MUUNGANO ambayo haitahusika na maisha ya watanzania bara kupitia mambo yenye mguso wa moja kwa moja. NITAWALETEA SIKU NYINGINE IMPLICATION ZAKE KIUCHUMI KWA TAKWIMU NA JINSI KODI ITAKAVYOPANDA KUKIDHI NYONGEZA YA SERIKALI. BE BLESSED

Hii analysis yako iko verry poor, ukizingatia lengo na madhumuni yako.

Kwanza Mchakato wa kuanzisha Katiba mpya mlikuwa hamuutaki kwa sababu itapunguza ulaji na mapango yenu yote ya kufanya uhalifu pamoja na ufisadi...

Ninauhakika nyinyi mnahofu kubwa sana ya kuwa na katiba mpya yenye vyombo vya sheria, ulinzi, Usalama na Uchaguzi huru kwani kufanya hivyo ninauhakika mtashindwa kupendelewa na hatimaye kufikishwa mahakamani na pengine kufungwa kwa sababu ya uovu mnaoufanya.

Wanganyika wanachotaka ni Tanganyika yao na Zanzibar wanachotaka no Zanzibar yao yenye mamlaka kamili nyinyi manataka serikali mbili ambayo imekuwepo tangu 1964 mpaka leo na mnataka kuendelea nayo kivipi???

Nyinyi hamna nia njema na Katiba mpya kwa sababu hamna uchungu na waTZ mko tu kwa ajili maslahi yenu tu na watanzania hawako tayari kudanganyika safari hii.
 
Ha ha ha! Kwa mamlaka mliyo nayo kama "chama tawala" hamasisheni watanzania wakubali mfumo wa serikali moja hapo nitawaona wa maana. Otherwise, Serikali Mbili (kama ilivyo sasa) ni usanii uliopindukia. Kama Serikali tatu haziwezekani then bora Muungano uvunjike kuliko kuendelea na huu usanii uliopo. By the way, inaeleweka ni kwanini CCM inang'ang'ania sana huu muundo uliopo.

OMBI KWA MODS: Tunaomba kile kitufe cha "dislike" kirudi; hii mada inatia kichefu chefu ukizingatia nia ovu ya chama cha mleta mada kuhusu suala la Muungano na Katiba kwa ujumla wake.

Kami ni kichefuchefu usingechangia. Ushabiki wa kidiasa unakufanya kuwa poyoyo
 
kama Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 Tukapata Tanzania. baada ya miaka50 ya majaribio tulitegemea huu muungano ukomae na kuwa serikali moja, ili tutamke kwa jeuri kuwa kuna nchi moja, Taifa moja, serikali moja, bunge moja, na dola moja. kwa hiyo ifikapo 26/4/2013 tungeizika zanzibar rasmi kama tulivyoizika tanganyika miaka hamsini iliyopita. Kama tutarudi kwenye serikali tatu au kuendelea na serikali mbili, mimi naona hakuna haja ya muungano, hapo ndoa imeshindikana hapo kila mmoja arejee kwa wazazi wake.
 
Huyu bwana Mwigulu Nchemba kila ninaposoma post zake akili yangu inanipeleka Arusha kwa wale watoto na akina mama waliokufa kwa lile bomu mkutano wa Chadema. Hivi anadhani watu tutasahau?

Watu wengine wana roho ngumu kweli kweli, wamesingizia watu innocent kedi za ugaidi na kuwalaza mahabusu miezi zaidi ya mitatu at the cost ya familia zao na watoto wao, wameua watu na na kuvuruga maisha ya wazazi na wengine kufanywa yatima, vilema na kuwa mzigo kwa familia zao milele halafu unakuja na distractions za katiba mpya.

Ujasiri watu hawa wanautoa wapi?

Katiba mpya ndiyo mada iliyoko mezani. Anzisha thread yako kwa hayo unayoyasema.
 
yaani kwa matendo yako mayu hata maadishi yako huwa sisomi!
Kuna siku utayalipa tu tena duniani !

Akili yako ni ndogo sanaaa na tena ni mbovu kama huwa husomi unacomment nini. Acha tabia za kike..
 
akili yako ni ndogo sanaaa na tena ni mbovu kama huwa husomi unacomment nini. Acha tabia za kike..
umejuaje !ni kweli nini akili kama za mama yako yule mnaye fananaye naye! Aisee una akili sana ,hata sauti nafanana na dadako yule wa 0713! Msalimie sana nchemba!
 
CCM huiba kura sana Zanzibar,wanajua sasa watazikosa za urais wa bara.Na yaliyotolewa ktk rasimu hawakutegemea kama yatakua na mapendekezo hayo.Ndugai hana kazi tena labda awe mbunge tuu.
 
Michango yetu tutatoa ktk mabaraza si hapa JF kuna utaratibu wa kufanya hayo.
 
Mwigulu, kwanza niungane na wewe kuhusu wasi wasi ulionao!
  1. Ni jambo la hatari sana kuwa na jeshi la ulinzi la jamuhuri ya muungano na kuwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya washirika. Wasi wasi wangu katika hili ni kuwa kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na uchumi wa Tanganyika, serikali ya Tanganyika inaweza ikawa na vikosi vyenye nguvu sawa na jeshi la muungano na hivyo kumfanya Rais wa Tanganyika asijitofautishe sana na Rais wa Jamuhuri! Kwa sasa jambo hilo halina athari kwa kuwa vikosi vya Zanzibar ni vidogo visivyo na silaha za kutisha!
  2. Hali kadhalika kwa jeshi la polisi! Rais wa Tanganyika anaweza asiruhusu polisi wa jamuhuri kufanya kazi katika eneo la Tanganyika kwa kuamini kuwa polisi wake wanatosha!
  3. Kuhusu maswala ya fedha, hapa ndipo penye vurugu kubwa za kiuchumi! Zanzibar kwa kudhani kuwa wana rasilimali nyingi kulingana na idadi ya watu wake itaona haina maana kuwa na sarafu moja na badala yake itaanzisha sarafu yake! Kitendo cha Zanzibar kuwa na sarafu yake kutadhoofisha muungano kwa kiwango kikubwa na kupeleka muungano kuvunjika!
  4. Neno "Shirikisho" nalo ni kizungumkuti! Tumekuwa na muungano kwa takribani miaka 50! Sasa kuanzisha shirikisho ni kurudi nyuma hatua kadha kwani kilichotegewa ni kuwa na muungano wa serikali moja! Hata hivyo kwa kuzingatia maoni ya baadhi ya wanasiasa wa Zanzibar na kwa namna wanavyowahamasisha wafuasi wao, itakuwa vigumu kuwa na serikali moja, mbili wala hizo tatu! Kwa kifupi ni vema tukaamua kuvunja muungano kwani kuendelea kuwa nao kutazua kero ambazo kamwe hazitaondolewa! Tutaendelea kujadili kero badala ya maendeleo ya nchi zetu! Hivyo kwa maoni yangu tusione aibu kuwaambia wenzetu wa Zanzibar kuwa sasa imetosha!
 
Mwigulu Nchemba, sijui ni kwa nini umelitazama suala la kuwa na majeshi matatu kwa mtazamo hasi zaidi. Ebu badili mawazo na kulitazama kwa mtazamo chanya; je hauwezi kuona uwezekano wa 'complemetarity'? Kwamba majeshi haya matatu, kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu, wanaweza kujijengea uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na hatari zozote zitakaziwakabili kama mmoja mmoja na kama wamoja?
Siku zote si tunasema kuwa umoja ni nguvu? Sasa kwa nini leo kuwe na woga kwamba majeshi matatu yanaweza kuleya mvurugano? Kwa nini tusiyaone kuwa ni umoja wenye nguvu?
Ndio, kuna suala la unyeti katika masuala ya ulinzi na usalama, lakini mbona hivi sasa tunashirikiana na majeshi ya nchi nyingine kufanya masuala ya ulinzi na usalama kwa pamoja bila matatizo. Kama inawezekana hivyo kwa nchi nyingine, nini kiutatufanya tushindwe kwenye nchi moja?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom