Katiba mpya,wananchi na wadau tuangalie maeneo haya kwa kina - Tanzania kwanza

Katiba mpya,wananchi na wadau tuangalie maeneo haya kwa kina - Tanzania kwanza

huu muundo wa serikali na muungano kwa ujumla unahitaji utulivu kuuamua ili kuondoa makelele ya mda mrefu mfano kusema kuwe na polisi ya muungano na washirika hapa utatokea mgongano hasa kiutendaji na kimamlaka.
 
Mie Tanganyika kwanza vinginevyo ibaki hivi hivi serikali mbili maana wengine tulishajizoelea na muundo huu kutokana na watu wa bara kumezwa na serikali ya muungani wakati wenzetu upande wa pili wana serikali yao pia ni beneficiary wa serikali ya muungano, mistake ilishafanyika tukawa na serikali mbili badala ya moja.

Kama serikali mbili imetushinda tujaribu serikali moja vinginevyo tujikatae mapema na sie tuwe na Tanganyika yenu na zanzibar ibaki kivyao maana serikali tatu ni uzushi tu wakati huo huo bado tena tupo kwenye shirikisho la Afrika mashariki. Kwani kama la serikali mbili au moja limeshindikana tukivunja muungano kuna shida gani hasa ukizingatia zanzibar na Tanganyika tuna uhusiano wenu wa kiasili hata kama tutakuwa nchi tofauti bado tunaweza tukaendeleza uhusiano wetu, mbona Kenya watu wanaingia na wanafanya tu shughuli zao kama kawa kama vile upo Dar tofauti ni kwamba unaingia na passport tu na bado hotel unalipa kwa rate zile zile (hapa kuna tofauti gani na mtu ambae anaishi Mwanza akaenda kwa shughuli binafsi Dar akafikia hotel akafanya yaliyompeleka na kurudi zake ndivyo hivyo na Zenji itakavyokuwa)
 
Jadiri hoja siyo sura za watu kama huwezi unaweza ukawa mjumbe msomaji wa mabandiko.

mkuu kunamajitu ya ajabu yenyewe kila kitu ni kejeli na matusi sijui wanamalezi gani lakini huu ni wakati wa kuungalia vema huu muungano na muundo wake kwani umekuwa ni kelo kwa mda mwingi ukiangalia rasimu nayo imekuja na mitihani mingi zaidi unawezaje kuwa na idara za usalama mbili kwenye nchi moja na majeshi mawili ya polisi ya polisi kwenye nchi moja hizo watafanyaje,
 
Kwa usalama wa ID yangu iwe active naomba kuachana na mjadala huu na sipendi kuchangia post yoyote ya Mwigulu, hata kama umeandika point nzuri kiasi gani ndani ya roho yangu nimekuweka kwenye kundi moja na Lucifer. Thats it i hate you.
 
mkuu kunamajitu ya ajabu yenyewe kila kitu ni kejeli na matusi sijui wanamalezi gani lakini huu ni wakati wa kuungalia vema huu muungano na muundo wake kwani umekuwa ni kelo kwa mda mwingi ukiangalia rasimu nayo imekuja na mitihani mingi zaidi unawezaje kuwa na idara za usalama mbili kwenye nchi moja na majeshi mawili ya polisi ya polisi kwenye nchi moja hizo watafanyaje,
Ni vizuri mkimueleza pia jinsi Ludovic alivyokuwa analia pale Mahakamani leo baada ya kukosa mtu wa kumdhamini, si vyema kumtelekeza mtoto wa watu baada ya kumtumia.
HAMY-D Njoo uongee na bosi wako hapa hii si tabia njema kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hii analysis yako iko verry poor, ukizingatia lengo na madhumuni yako.

Kwanza Mchakato wa kuanzisha Katiba mpya mlikuwa hamuutaki kwa sababu itapunguza ulaji na mapango yenu yote ya kufanya uhalifu pamoja na ufisadi...

Ninauhakika nyinyi mnahofu kubwa sana ya kuwa na katiba mpya yenye vyombo vya sheria, ulinzi, Usalama na Uchaguzi huru kwani kufanya hivyo ninauhakika mtashindwa kupendelewa na hatimaye kufikishwa mahakamani na pengine kufungwa kwa sababu ya uovu mnaoufanya.

Wanganyika wanachotaka ni Tanganyika yao na Zanzibar wanachotaka no Zanzibar yao yenye mamlaka kamili nyinyi manataka serikali mbili ambayo imekuwepo tangu 1964 mpaka leo na mnataka kuendelea nayo kivipi???

Nyinyi hamna nia njema na Katiba mpya kwa sababu hamna uchungu na waTZ mko tu kwa ajili maslahi yenu tu na watanzania hawako tayari kudanganyika safari hii.

kweli kabisa!
 
Tahira ww, kichaa mkubwa wewe, ukawa danganye wala punda wenzako wanyiramba kule singida, ww subiri uone udhalimu unao watenda watz hauta onja mauti kabla ya kuyaona malipo uaji wote uliopanga kwa uroho wa siasa na ccm yako,
shame upon you.
watz lazima wapate tanganyika yao, peleka ujinga wako kwa wauaji wenzako wa ccm
 
Tahira ww, kichaa mkubwa wewe, ukawa danganye wala punda wenzako wanyiramba kule singida, ww subiri uone udhalimu unao watenda watz hauta onja mauti kabla ya kuyaona malipo uaji wote uliopanga kwa uroho wa siasa na ccm yako,
shame upon you.
watu lazima wapate tanganyika yao, peleka utahira wako kwa wauaji wenzako wa ccm



Other things Remain Constant,
Vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba TUISOME RASIMU, TUTAFAKARI, TUJADILI, TUTOE MAONI KWA KUITANGULIZA TANZANIA MIOYONI MWETU. SIO KULENGA KULIKOMOA KUNDI FULANI AU UPANDE FULANI WA NCHI.
Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:

A) Ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... ktk maeneo yao.

Pili ibara ya 227(1) kutakuwa na Jeshi la Polisi la jamuhuri ya muungano litakuwa na jukumu la ulinzi wa wa watu wao, Ibara ya 232 inaongelea vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao Pia 233 (1) kutakuwa na idara ya usalama wa Taifa wa jamuhuri ya muungano ... Ibara 235 inasema bila kuathiri masharti ya katiba hii, nchi washirika wanaweza kuanzisha idara za usalama.

Analysis, swala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo nirahisi vikosi vya muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa.

B) ibara ya 217(1) kutakuwa na benki kuu ya jamhuri ya muungano na majukumu yameainishwa...... ibara ya 218 serikali washirika zitakuwa na BENKI ZAO zakusimamia sera za kifedha na kibenki
Analysis; hakuna namna unaweza kuwa na monetary policy tatu ktk nchi moja ukafikia malengo. Ni kama gari kuwa na sukani tatu na madreva wa tatu at per, the will miss the right direction.

C) ibara ya 1(1), 1(2) na 57(1) zinazungumzia shirikisho, nionavyo mimi ni makosa. Jamhuri ya muungano ni nchi sio shirikisho. Kupata shirikisho ni sharti kwanza nchi washirika tupige kura kama tunataka kujiunga na shirikisho au laa kama tulivyokataa la afrika mashariki.

Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia bila kuangalia mungano wa serikali mbili kuwa ni msimamo wa CCM. TANZANIA BARA ITAKUWA NA SERIKALI MBILI YAANI YA BARA NA YA MUUNGANO ambayo haitahusika na maisha ya watanzania bara kupitia mambo yenye mguso wa moja kwa moja. NITAWALETEA SIKU NYINGINE IMPLICATION ZAKE KIUCHUMI KWA TAKWIMU NA JINSI KODI ITAKAVYOPANDA KUKIDHI NYONGEZA YA SERIKALI. BE BLESSED

 
kama Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 Tukapata Tanzania. baada ya miaka50 ya majaribio tulitegemea huu muungano ukomae na kuwa serikali moja, ili tutamke kwa jeuri kuwa kuna nchi moja, Taifa moja, serikali moja, bunge moja, na dola moja. kwa hiyo ifikapo 26/4/2013 tungeizika zanzibar rasmi kama tulivyoizika tanganyika miaka hamsini iliyopita. Kama tutarudi kwenye serikali tatu au kuendelea na serikali mbili, mimi naona hakuna haja ya muungano, hapo ndoa imeshindikana hapo kila mmoja arejee kwa wazazi wake.

naunga mkono hoja!
 
Mimi ni TANGANYIKA KWANZA mengine baadae.

Lakini kwa jinsi inmavyoonekana Tanzania inaweza kuwa na majeshi ya ulinzi matatu, hapo ndio matatizo yatakapoanzia kwa sababu kila mtu ataiona ana comand upande wake.

Mimi nadhani ni vyema kila nchi ijetegemee kivyake na tubaki marafiki kama kenya na sie . ... Mbona EAST AFRICA ilivunjika?
Mbona Sudan imegawanyika?

Hizi ndoa zenye manung'uniko kila kukicha ndio matokeo yake siku moja unakuta mzazi mmoja kwatilia sumu familia nzima ili wote wakose.

TANGANYIKA KWANZA!

Huwa unaonekana kama Chizi. Anyway leo navunja mwiko, namgongea "mwendawazimu" like!
 
Today you want to be patriot after killing people in Arusha, U will still remain the most brainless person I have ever seen
 
Serikali tatu au mbili kwa Muungano wetu siyo tiba kabisa. Na hili hata Pinda aliongea lakini akashambuliwa akakana!. Huwezi kuwa na Serikali tatu halafu utegemee ufanisi wakati hata serikali mbili zimeshindwa.

Solution ni serikali moja au kuachana na huu Muungano!
 
Mimi ni TANGANYIKA KWANZA mengine baadae.

Lakini kwa jinsi inmavyoonekana Tanzania inaweza kuwa na majeshi ya ulinzi matatu, hapo ndio matatizo yatakapoanzia kwa sababu kila mtu ataiona ana comand upande wake.

Mimi nadhani ni vyema kila nchi ijetegemee kivyake na tubaki marafiki kama kenya na sie . ... Mbona EAST AFRICA ilivunjika?
Mbona Sudan imegawanyika?

Hizi ndoa zenye manung'uniko kila kukicha ndio matokeo yake siku moja unakuta mzazi mmoja kwatilia sumu familia nzima ili wote wakose.

TANGANYIKA KWANZA!



Tehteh!
Umeingia chakike,
kwa hizo sera zako watakutimua sasa hivi.,
Ama sivyo ukubaliane na sera zao.
 
Unajua nimeshtuka sana! Nilidhani Savimbi kafufukia humu JF, kumbe ni Mwigulu Mzee wa kuchamba! Katika hoja zako, hiyo ya kuendelea na serikali mbili haikubaliki kamwe! Tunataka sasa serikali tatu, tunataka Tanganyika yetu mliyoiua CCM.
 
Back
Top Bottom