KATIBA MPYA: Wananchi wajipanga kuanzisha Kikosi kazi chao kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kabla ya 2025

KATIBA MPYA: Wananchi wajipanga kuanzisha Kikosi kazi chao kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kabla ya 2025

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio taarifa inayotembea mitandaoni kwa sasa, hasa baada ya kikosi kazi cha serikali kinachoongozwa na Profesa Mukandala kusoma mapendekezo ambayo hayafahamiki yalikookotwa.

Mukandala huku akitetemeka (Ishara ya uongo), amependekeza kwamba mchakato wa Katiba mpya uanze baada ya Uchaguzi mkuu wa 2025, bado wananchi wanajiuliza ni wapi alikopata maoni hayo na ni nani waliohojiwa na kinachoitwa Kikosi kazi kilicho chini yake kilichojaa Mamluki wachumia tumbo.

Bali sasa Wananchi wa Tanzania kwa umoja wao wanapanga wiki ijayo kutangaza Kikosi kazi chao kitakachosimamia mchakato wa Katiba Mpya, inayopaswa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025, gharama zote zitalipwa na Wananchi Wenyewe.

KATIBA MPYA NI SASA, SIYO BAADA YA 2025

%23KatibaMpyaNiSasa.jpg
 
Dogo lala tena uote ,jaribuni kuwa watu wa maana Kila mtu anataka katia lakini lazima tufuate utaratibu sio lazima upete katiba ukiwa na chongo

USSR
 
Mngejua watu wana kiu ya pesa uku mtaani msingeangaika na katiba.

Katiba inaletaje maisha mazuri kwa mtanzania wa hali ya chini??

Success story ya katiba iliyoleta maisha mazuri ni nchi gani? Dubai? Singapore? Qatar?
 
Mngejua watu wana kiu ya pesa uku mtaani msingeangaika na katiba.

Katiba inaletaje maisha mazuri kwa mtanzania wa hali ya chini??

Success story ya katiba iliyoleta maisha mazuri ni nchi gani? Dubai? Singapore? Qatar?
Umelima mahindi yako halafu Serikali inakunapangia bei na soko, hapo utapataje hiyo pesa? KATIBA MPYA ni muarobaini wa UHALIFU wote wa CCM, umeelewa sasa we kilaza?
 
Umelima mahindi yako halafu Serikali inakunapangia bei na soko, hapo utapataje hiyo pesa? KATIBA MPYA ni muarobaini wa UHALIFU wote wa CCM, umeelewa sasa we kilaza?
swadakta
 
  • Thanks
Reactions: Mu7
Kuhusu Katiba mpya,Ni kwamba Serikali ina-buy time tuu,kuunda vikosi kazi ambavyo Ni vya Serikali yenyewe.KWA NINI ,Kama kweli Serikali iko serious kuwapa wananchi wake Katiba mpya,KWA NINI ISIANZE NA KIKOSI KAZI KILICHO SERIOUS,Wakaanzia kwenye Ile Forum ya maoni ya wananchi aliyokusanya Warioba ? Ikianzia Hapo,kwa vyovyote Katiba mpya kupatikana kwake haiwezi kuzidi Miaka mi-3.TATIZO SERIKALI INAZUGA tuu haipo serious.NA Katiba yoyote nje ya maoni ya wananchi aliyokusanya Warioba Sio Katiba ya Wananchi(Itakuwa Ni Katiba ya kuwalinda viongozi na chama kinachotawala kwa Sasa).KAMA ILE KATIBA ALIYOCHAKACHUA MAREHEMU Sitta na Bunge lake la CCM la Katiba,Ile siyo Katiba pendekezwa ya Wananchi.Hao Akina mkandala na viongozi mamluki wa vyama vidogovidogo ambavyo havina hata mbunge mmoja Bungeni "Kama Akina HAMADI RASHIDI,Shibuda n.k.Ni kwa vipi Hawa jamaa ni wawakilishi wa wananchi ?SERIKALI YETU TAFADHALI,TUNAWAOMBA MUWE SERIOUS KWENYE MAMBO SERIOUS Na MAKINI YA WANANCHI.MSILETE UTANI KAZINI.Mkumbuke wananchi ndio waajiri wenu.Msijaribu kuwaamsha Hawa Watanzania ambao kwa Sasa wamelala,msije mkalala nyie.
 
Hapa ndipo yale maneno"ameonja asali kaamua kuchonga mzinga"
Mama katupiga na kitu kizito kichwani
Kajitengenezea tume kama ile ya Warioba kinamna fulani
Hivyo kawahakikishia kina Zito maVx na mafuta posho mpaka 2030
Mama muogope Muumba asikupige kipapai ukamalizia maisha kwa taabu na mateso mwenzako alichomolewa bila mateso
 
Mnaanza tena??? Sasa sijui tutawaomba viongozi wa dini tena wakamuombe mama tena. Jamani, tafuteni hoja za msingi msimchokoze Rais.
 
Hii ndio taarifa inayotembea mitandaoni kwa sasa , hasa baada ya kikosi kazi cha serikali kinachoongozwa na Profesa Mukandala kusoma mapendekezo ambayo hayafahamiki yalikookotwa .

Mukandala huku akitetemeka (Ishara ya uongo) , amependekeza kwamba mchakato wa Katiba mpya uanze baada ya Uchaguzi mkuu wa 2025 , bado wananchi wanajiuliza ni wapi alikopata maoni hayo na ni nani waliohojiwa na kinachoitwa Kikosi kazi kilicho chini yake kilichojaa Mamluki wachumia tumbo .

Bali sasa Wananchi wa Tanzania kwa umoja wao wanapanga wiki ijayo kutangaza Kikosi kazi chao kitakachosimamia mchakato wa Katiba Mpya , inayopaswa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 , gharama zote zitalipwa na Wananchi Wenyewe .

KATIBA MPYA NI SASA , SIYO BAADA YA 2025

View attachment 2159876
Uzi mzuri sana lakini nilikuwa napenda kushauri kitu kidogo hapa Kwanini wanaharakati wanao dai kuitaji katiba mpya wasifanye kuanda majukwa yatakayo saidia kuelewesha wananchi kusu katiba hii iliopo kwanza ili watu waweze kufahamu kuwa nini kilichopo kwenye katiba hii baada ya hapo watu pia waweze kujuwa ubora wa katiba hii ya sasa na wapi katiba hii ilipo kuwa dhaifu ndipo ipatikane nguvu kubwa itakayo weza kuamua je katiba ibadilishwe au laa.

Maana kwa mfumo wa taifa letu ni watu wachache walio weza kusoma katiba na kuelewa na kutambuwa ni wapi pakuboshera na wap si pakuboresha.

Huu ni mtazamo wangu ingepunguza mivutano inayo endelea mitandaoni kuusu madai ya katiba mpya. Siyo vijana wengi waliopo katika mitandao ya kijami kama vile twitter pamoja na JF wanao fatilia mambo ya kimsingi, na wengi wao pia waliopo kwene mitandao hii sio wanaifahamu kusu katiba utakuta tu ni wanatembea na kasi pamoja na mwelekeo wa upepo unvyo kwenda.
 
Back
Top Bottom