KATIBA MPYA: Wananchi wajipanga kuanzisha Kikosi kazi chao kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kabla ya 2025

Ushauri wako umepokelewa , japo mwenendo wa Rais wa awamu ya 5 ulifunua karibu kila Mtanzania kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya
 
Mngejua watu wana kiu ya pesa uku mtaani msingeangaika na katiba.

Katiba inaletaje maisha mazuri kwa mtanzania wa hali ya chini??

Success story ya katiba iliyoleta maisha mazuri ni nchi gani? Dubai? Singapore? Qatar?
Katiba Mpya ndio itakayokuja kukufungulia njia uanze kufaidi matunda ya utanzania wako, uifaidi keki ya taifa lako, sio kama sasa keki ya taifa inaliwa na kikundi kidogo cha watu.

Mfano.

Katiba Mpya ikaruhusu nafasi za ajira serikalini kama DED na nyinginezo kuombwa na wenye vigezo kupewa nafasi hizo itatuondolea ukiritimba wa sasa ambao nafasi hizo nyingi hupewa watoto wa waliowahi kuwa viongozi wa serikali miaka ya nyuma, kwa kujuana, huku wengine wakiendelea kuhangaika na bahasha za kaki miaka yote bila nafuu licha ya degree au ngazi nyingine ya elimu uliyofikia

Lakini pia, Katiba Mpya ikija italeta mgawanyo mzuri na usimamizi mzuri wa mapato yanayotokana na rasilimali za taifa letu, mfano, madini na vivutio vingine vya utalii kama mbuga za wanyama nk.

Mapato hayo yakipata usimamizi mzuri kwa wahusika kuyasimamia kwa kufuata sheria zitakazowekwa na Katiba Mpya yataleta nafuu kwa watanzania wengi, mfano vikundi vya vijana na kinamama, watapata mikopo nafuu ya uhakika hii itawasaidia kuanzisha biashara zao na kuweza kujikimu mahitaji yao na kuondokana na umaskini wa kipato.

Tofauti na sasa mapato ya madini na mengineyo yanapotelea kwenye mikono ya viongozi walafi wasiochoka kuliibia taifa wanaolindwa na chama kinacholiongoza taifa, matokeo yake umaskini kwa wengi unazidi kuongezeka kila kukicha, huku wanufaika wakiwa wachache tu.

Hivyo nikushauri ndugu, Katiba Mpya [ Rasimu ya Warioba ] itakuja kulifungua taifa letu kwa namna itakayomgusa kila mmoja wetu popote pale alipo kiuchumi na kijamii, wakati ndio huu tuanze kuipigania sasa.
 
Wajiandae tu kukamatwa na kutupwa Mwabe Pande, Mama si anashauriwa na Kikwete kwa kila kitu, subirini tu mtaona maana huu ndiyo ulikuwa mchezo wa Kikwete katika utawala wake.
 
Jiwe aliweka vitisho akaondoka , wewe ni nani wa kututisha ?
Bado hawatambui kwamba vitisho havina nafasi tena Tanzania, hawa watu sijui akili zao zikoje.

Wametishia Ugaidi, wakaona watu hawatikisiki.

Hii ni mikiki ya mwisho mwisho, ndiyo maana unaona Maza Mizinguo anachanganyikiwa kabisa hajui afuate lipi. Iliyobaki sasa ni kuachia tu.

CHADEMA ni lazima wakazie hapo hapo. Hii ajenda ya Katiba Mpya wamepewa kama zawadi kwao.
Wasikose kuitumia ipasavyo.
 
Na usisahau kwamba 'Maza Mizinguo' alikuwa ni Makamu Mwenyekiti kwenye hiyo "iliyochakachuliwa". Leo hii anang'aka hajui kwamba wananchi wa Tanzania wanataka katiba mpya!
 
Pamoja na kwamba pendekezo lako unaweza kuwa umelitoa kwa nia njema, lakini hili unalopendekeza haliwezekani, na pendekezo hili ndilo linaloweza kugeuzwa na hao wasiopenda uwepo wa katiba mpya kuchelewesha mchakato mzima wa kuendelea na mipango ya katiba mpya haraka iwezekanavyo, kabla ya 2025.

Wananchi wanaotaka kujuwa ubaya na uzuri wa katiba iliyopo, tayari wapo wengi sana, hasa ukichukulia kwamba hii siyo mara ya kwanza kATIBA mPYA KUDAIWA.
Mchakato wa kuandaa katiba mpya tayari ulishafanyika, tokea wananchi waliposhirikishwa kutoa maonikatika Tume ya Warioba. Hapajabadilika chochote toka wakati huo na sasa kiasi kwamba watu wasijue uhitaji wa katiba mpya. Labda useme tu kwamba wakumbushwe, kazi ambayo itakuwa ikifanyika wakati wa mchakato wa Katiba mpya ukiendelea.

Kwa kifupi.
Ninakubaliana na wewe, kuna haja ya wanaharakati, hasa hizi taasisi tulizonazo zisizo za kiserikali kuanza kufanya kazi ya kukumbusha wananchi umuhimu na uhitaji wa uwepo wa Katiba Mpya, kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Sioni sababu ya kusimamisha zoezi la kuanza maandalizi ya kupata katiba mpya eti kwa sababu wananchi hawana elimu kuhusu katiba iliyopo. Hii itakuwa ni kupoteza muda, ambao ni mfupi sana.

Natumaini Erythocyte ataiona habari hii.
 
Hiki ndicho kilichobakia
Kuna wachache wanataka kujimilikisha nchi...
Mabango ya Katiba yawe mengiiiii wakereke

Katiba ni ya Wananchi sio kikosi kazi (kuwatisha watu eti kikosi kazi ndio nini)
Yule mwenye kujidai na muziki wa bacongo akose usingizi
 
Hizi ni ndoto za uongo punguzeni kuota mchana.
 
Umelima mahindi yako halafu Serikali inakunapangia bei na soko, hapo utapataje hiyo pesa? KATIBA MPYA ni muarobaini wa UHALIFU wote wa CCM, umeelewa sasa we kilaza?
Wewe ndio kilaza na mamako na babako, haujui hata maswala ya kikatiba ni yapi. Kwa hiyo ndio mnavyodanganywa katiba itakuja kucontrol soko?
 

Hii ndiyo njia muafaka ya kupata katiba mpya. Liwalo na liwe.
 
Mama Samia anajua kwamba Maoni ya wananchi yalishakusanywa na Tume ya Warioba , yeye mwenyewe alikuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba.

Haya ya kusema wananchi hawana uelewa katunga tu ili asogeze muda malengo yatimie .

Ni kosa kubwa sana kudharau wananchi
 
Mngejua watu wana kiu ya pesa uku mtaani msingeangaika na katiba.

Katiba inaletaje maisha mazuri kwa mtanzania wa hali ya chini??

Success story ya katiba iliyoleta maisha mazuri ni nchi gani? Dubai? Singapore? Qatar?
Huyo mnamtegemea awaletee pesa mtaani mawazo yake yapo kwenye uchaguzi wa 2025 na anavyoonekana kua na uroho wa madaraka msishangae akangangania aongoze milele
 
Huyo mnamtegemea awaletee pesa mtaani mawazo yake yapo kwenye uchaguzi wa 2025 na anavyoonekana kua na uroho wa madaraka msishangae akangangania aongoze milele
Hatari sana !
 
Dogo, hili lilishafanywa kikamilifu wakati wa Rasimu ya Warioba..
 
Yanabana lakini yataachia tu.Katiba mpya ni lazima,huwezi kuzuia hitaji la wenye nchi yao🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
 

Safi sana kiongozi madarasa kama haya anatakiwa yasambazwe zaidi ili watu wapate kuelewa kuhusu hii katiba mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…