Katiba na Siasa za Tanzania - Tuwekane sawa

Katiba na Siasa za Tanzania - Tuwekane sawa

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Kiwango kilichofikiwa kinafikirisha.

1. Kufanya siasa kwenye ubora wa elimu ilikuwa mkakati wa muda mrefu uliobuniwa na utawala wa awamu ya pili ili kuwa na taifa la watu wasiojielewa kusudi waburuzwe, AU ilitokea coincidently tu kulingana na uelewa wa kiongozi wa nchi juu ya maana na umuhim wa elimu kwa taifa?

Kuna ulazima wa kurejesha Elimu ya nchi katika ubora ili tuwe na competent and valuable human capital, ambayo ni muhimu sana kuweka taifa katika mwelekeo sahihi. Nashauri serikali chini ya rais, i deploy consultant service kutoka "UINGEREZA", ifanye kazi na team ya team ya wataalam mchanganyiko (Si wizara ya elimu iliyoshindwa), kuratibu upya elimu yetu kwa kutuonyesha pia wapi tuliangukia), lakini watoe pia mwongozo wa utekelezaji wa mpango huo na washiriki katika kuusimamia japo kwa miaka kadhaa ya awali. La sivyo tumekwisha!.

2. Nini kifanyike kuirejesha nchi katika orbit sahihi ambayo kwa mjibu wa katiba inaonekana ni mali ya watu wachache, na wanaweza kufanya watakayo bila kuhjiwa wala kuwajibishwa? Mfano, sasa hatuna Bunge, na wananchi kwa sababu ya namba 1, hapo juu wanashangilia. Kwa msingi huo huo, watu wanashangilia hata pale Mahakama inapoonyesha rangi ya kudhoofishwa na kufanya kazi kisiasa. Hili ni muhimu la sivyo hakuna aliyesalama.

3. Utendaji kazi uliochini ya viwango wa vyombo vya serikali, na kutokujali shida za wanyonge, wasio na elimu sahihi, wala mahala pa kulilia ni bomu kubwa kwa hatma ya nchi. Mamlaka kuu nchini zinapocompromise standards bila woga si tu ni mfano mbaya sana bali ni dharau na dhihaka kwa Watanzania japo ndiyo wamefanywa misukule kwa kunyimwa elimu sahihi. Mfano Wizi uliyonyamaziwa wa wizara ya fedha, huku wananchi wakiumizwa na tozo, huku Waziri wa fedha akiwafanya wapumbavu kwakmba madeni yanayokopwa yatalipwa na Serikali si wananchi, kukithiri kwa rushwa na ukikukwaji wa haki za binadamu mara kwa mara, haviashiriii afya njema.

Nina mifano mingi. mmoja wapo, ni "Spika wa bunge kutokujua taratibu za kuacha kazi ni dalili kwamba kansa ya kukosa viwango, imeenea ktka nchi". Ni jambo lisiolomithilika spika wa Bunge kuandika barua ya kujiuzuru nafani yake ya spika kwa katibu wa CCm, na kumpa nakala mwajiri wake. Ni kweli hii? Katibu wa Bunge anasubiri maelekezo kutoka kwa katibu wa ccm ili a effect hiyo barua? Ccm ndiyo mwajiri wa spika na bunge ni mtendaji wa ccm?
Hii ni nini hii?

Ni huzuni sana. Pamoja na mifano mingi ambayo sijaitaja, tunahitaji kufanya kitu. Nini kifanyike?
 
Nikuulize swali mkuu, Je Katibu wa bunge anaweza kumfukuza kazi Speaker? Tuanzie hapo. Maana aliyekuwa nafasi uliyonayo ndiye mwenye uwezo wa kukufukuza au kukuwajibisha.
 
Nikuulize swali mkuu, Je Katibu wa bunge anaweza kumfukuza kazi Speaker? Tuanzie hapo.
Katibu wa Bunge ni mtendaji wa Bunge anayetuliwa na Rais, kwa mujibu wa katiba ya JMT. Spika anaweza kufukuzwa kazi ya uspika kwa maazimio ya Bunge na katibu wa bunge akatekeleza kama mtendaji mkuu wa ofisi za Bunge.

Katibu mkuu wa Ccm anahusika nini na shughuli za bunge? Sheria gani inampa mamlaka ya kutoa maelekezo kwa katibu wa Bunge? Huoni kama kuna kitu kibaya sana hapa? Kwamba spika anaandika barua ya kuresign nafasi ya uspika kwa katibu wa ccm halafu mwajiri wake anampa nakala!. Mwajiri wake anakiri kwmba anasubiri kwanza katibu wa ccm aseme, ndipo yeye atende!.



Ni kitu gani hiki lakini?
 
Hii ni Tanzania mkuu,mahali ambapo katibu wa tawi wa chama chetu anaweza kumpiga mkwara mkurugenzi wa halmashauri akanywea kabisa.
 
Back
Top Bottom