You are missing the point dude!
Tatizo sio kuwepo au kutokuwepo kwa kipengele.
Tatizo ni utaratibu unaotumika kuingiza na kutoa vipengele pamoja na kauli za UONGO zinazotolewa na viongozi waandamizi wa chama kulaghai watu juu ya utaratibu huo.
Kuna busara moja ya Kiingereza nitaitafsiri kwa Kiswahili ieleweke. Inasema "Si kila jambo sahihi ni zuri. Ni busara sahihi kumpatia chakula mtu mwenye njaa kali, lakini chakula hicho kinaweza kumuua kwa vile tumbo likiwa tupu linapaswa kupewa mlo kwa hatua eg kwanza anywe uji wa moto kabla ya mlo..Kwahiyo japo ni sahihi kumpatia mlo mtu mwenye njaa kali, kufanya hivyo kunaweza kuleta matokeo mabaya, yaani kifo cha mwenye njaa kali."
Kwa kuzingatia busara hiyo ya Waingereza, na kwa kupuuzia maajabu ya CCM kusumbuliwa na ukomo wa uongozi,si katika chama chenu, bali Chadema, as long as viongozi waliopo sasa wana-deliver, who gives a sh*t about ukomo wa uongozi wao? Ndio sheria na kanuni ni muhimu lakini what if sheria na kanuni hizo hazitomsaidia Mtanzania kuondokana na CCM? Do you seriously think Chadema wakiamua kufuata demokrasia halisi na hatimaye wakapata Mwenyekiti na mgombea urais John Shibuda kutakuwa na haja ya kufanya uchaguzi mkuu kwa matarajio ya Chadema kuing'oa madarakani CCM?
Mtu hahitaji kuielewa vema taaluma ya siasa kubaini kuwa CCM wangependa sana kuona Chadema sio tu inadhoofika bali pia inakufa kabisa. Pamoja na hujuma kubwa zinazofanywa dhidi ya chama hicho kikuu cha upinzani kwa kutumia vyombo vya dola na mamluki waliopandikizwa Chadema, moja ya matamanio makubwa ya CCM ni kuiona Chadema ikifa kifo cha asili eg iweke ukomo wa uongozi mahiri uliopo madarakani hivi sasa kisha waingie kila Dick,Tom na Harry na hatimaye CCM iiendeshe Chadema kwa remote control.
Ukomo wa uongozi katika taasisi yoyote ile ni maamuzi na maridhiano ndani ya taasisi husika. Kwa hapa Uingereza, taasisi muhimu kabisa ni monarchy. Na tukiamini kuwa Uingereza ni miongoni mwa mataifa yanayoaminika kwa demokrasia duniani,kwanini basi monarchy haina ukomo? Jibu jepesi ni kwamba monarchy inaonekana kuwa na manufaa makubwa kwa taifa hili kuliko hiyo 'demokrasia' ya kila muda flani ya kuwabadili Labour na Conservatives.
Ni upunguani kwa CCM kuhangaika na ukomo wa uongozi huko Chadema ilhali mnashindwa kuleta ukomo wa umasikini wa Mtanzania. Ni uendawazimu kwa CCM kuhangaika na 'matatizo' ya Chadema ilhali Mwenyekiti wenu kishawatahadharisha kuwa mnaweza kung'oka madarakani mwaka 2015.
Sote watafahamu kuwa 'adui mwombee njaa' na unafiki wenu wa kuonyesha mnakerwa na 'kutokuwepo kwa ukomo wa uongozi ndani ya Chadema' au 'kuchakachuliwa kwa katiba ya Chadema' ni desperation tu. Ndio two wrongs dfon't make a right, lakini kama suala ni uchakachuaji basi babu la uchakachuaji ni CCM, na si kwa masuala yake ya ndani tu bali hata kwa taifa kwa ujumla.Hivi sio ninyi mliobadili rushwa na kuiita takrima?
Ukomo wa uongozi katika Chadema or not, katiba iliyochakachuliwa or not, as long as Dkt Slaa na timu yake wanawezxa kuikomboa Tanzania kutoka katika nira ya ufisadi, who gives a damn?
You guys need to get a life!