Katiba ya Kenya: Kesi zinaendeshwa live, huku itatuchukua miaka 200 kufika

Katiba ya Kenya: Kesi zinaendeshwa live, huku itatuchukua miaka 200 kufika

Kabla ya kuwasifia wakenya tujiulize walifikaje hapo... hao majirani wamemwaga damu nyingi kufikia hapo walipo. Udikteta wa enzi za Moi ulikuwa ni mkubwa na viongozi wengi waliompinga walipitia msoto na wengine kuuwawa. Mwaka 2008 tunaukumbuka kwa machafuko ya wao kwa wao na kupelekea vifo vingi sana. Tanzania tupo tayari kupita njia waliyopita? Kuhusu uchumi mnaosema kwamba wako mbali ni stori za Alinacha. Huo uchumi mzuri ni kwa tabaka la wachache nchini Kenya. Wananchi walio wengi wana hali ngumu sana kimaisha kuliko sisi watanzania. Wakenya wanaoingia TZ kihalali na kinyemela ni wengi mno ili kutafuta maisha mazuri. Na hizo sera zao za kibepari zimechangia hali ya usalama Kenya kuwa ni ya kusuasua hasa kwenye mambo ya ugaidi. Kimsingi hakuna mwanausalama au mzalendo yeyote ndani ya Tanzania anayeweza kusikiliza huu ushuzi wa BAVICHA na CHADEMA kwa ujumla. Tanzania iko vizuri kuliko CHADEMA wanavyodhani
Wadanganye wajinga wenzako, sisi tunaoishi mipakani tunaijua Kenya kuliko wewe
 
Kuendesha Kesi Live mpaka Katiba iseme ?
 
Tuseme ukweli Kenya wana moja ya Katiba Bora kabisa kwa mazingira ya Afrika.

Yaani ukiangalia Mazingira ya Africa yalivyo basi hawa jamaa wana katiba nzuri sana aangalia Kesi ya BBI yao inaendeshwa live kabisa kila mtu anaweza fuatilia mjadala, huku hata kurecord tu hauruhusiwi kinacho uhusiwa ni kupigapiga picha tu.

Ni lini tutakuwa na hata Robo ya katiba ya hawajirani zetu?
Ukimuiga tembo kula boga................
 
Tuseme ukweli Kenya wana moja ya Katiba Bora kabisa kwa mazingira ya Afrika.

Yaani ukiangalia Mazingira ya Africa yalivyo basi hawa jamaa wana katiba nzuri sana aangalia Kesi ya BBI yao inaendeshwa live kabisa kila mtu anaweza fuatilia mjadala, huku hata kurecord tu hauruhusiwi kinacho uhusiwa ni kupigapiga picha tu.

Ni lini tutakuwa na hata Robo ya katiba ya hawajirani zetu?

Bila uchumi yote hayo n maigizo!!
Bado kenya n poor n its going no where with american democracy

Ilikua footprint ya USA SASA INAKUA YA CHINA!!
Huwezi chukua mbinu za adui yako utegemee kumshinda!!
I love china lol! They have their own system n now catching Us n toning the west
 
KUNA MPUUZI MMOJA ALIAMRISHA BUNGE LIONYESHWA USIKU TU KATIBA MPYA NI MUHIMU USSR
 
Mimi nina imani ya dhati katiba mpya itapatikana Tanzania, tena ile tuitakayo. Kama Jiwe alikata moto pasi watu kutarajia ikiwa yeye mwenyewe alishajipa hakika ya kutawala kwa muda mrefu sana basi hata katiba itapatikana.
Inawezekana isiwe kupitia kwa huyu mama (kwa mipango ya Mungu labda na yeye transitional president tu wa kutuliza uharibifu wa Jiwe) lakini katiba mpya itapatikana.
 
USA lini walianza kuonesha proceedings za mahakama live ,kuwa na akili japo kibaba tu.

USSR
Kesi ngapi tumeshazishuhudia zikiwa live?hiyo case ya yule askari aliyemuua yule mmarekani mweusi , ilikuwa ni DRC?
 
Samahani mkuu ila siasa za kenya ni za Inner Circles. Kila sehemu katika taaisi za uma kuna wakuu ambao wana weza hata kum challenge mkuu wa nchi. Hiyo ni demokrasia iliyopitiliza mipaka.

Kwa yanayoendelea kenya ni udhalilishaji wa raisi na serikali kwa ujumla. Natoa rai katiba tuliyo nayo ibaki hivo hivo.

Nchi kama kenya imejiingiza kwenye mtego wa public participation itafika mda nchi itashindwa kutawalika kwani kila mtu ana mamlaka.

The King Do No Wrong ndio msingi wa katiba ya Jamuhuri yetu kubali kataa na ni bora iwe hivo kuliko kuwa na katiba chama la wana kama kenya hakuna mtu mwenye mamlaka kamili.

Ni sawa na mtu utakuwa baba gani wakati kila ukiamua kitu mke anakupinga na watoto wanakupinga.
 
We naye unachekesha!!ina maana huo uhuru wa kuonyesha matukio ya mahakamani live ni kutokana na technology!??basi kama ni hivyo mbona hapa hata kurecord tu matukio mahakamani huku kesi ikiwa inaendelea hata kwa kutumia simu tu ni kosa?!kenya wana matatizo yao lakini kwenye uhuru wako mbali sana!!sisi kila kitu utaambiwa ni kutokana na sababu za kiusalama, ina maana kwenye level ya usalama tuko pabaya zaidi hata ya USA?!!
Tanzania ni Noth Korea ya Afrika .......!!
 
Back
Top Bottom