Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Mwana JF,
Hebu fikiria hili. Katiba yetu inasema Tume ya Uchaguzi ikishamtangaza mtu hakuna mtu anaruhusiwa kupinga matokeo mahakamani. Ulishafikiria siku mwenyekiti wa tume akimtangaza mtu yeyote kuwa Rais itakuwaje? Yaani fikiria akitamka kuwa rafiki yake (mathalani Hashimu Rungwe) ndiye mshindi wa Urais, regardless ya kura zake, anakuwa Rais. Kwa katiba hii, hakuna mtu anaruhusiwa kupinga mahakamani.
Hii Katiba ni ya hovyo kabisa. Katika katiba za hovyo ni ya kwanza duniani. Watanzania tuikatae. Mtu mwenye nia njema hawezi kukataa katiba mpya yenye kutoa haki na usawa. Ni mafedhuli tu yanakataa haki. Yamezoea vya kunyonga km makaratasi ya kura ya kupigia majumbani kwao na mahotelini na kuyapeleka kwenye vituo vya kura kwa mabegi. Yanaogopa vya kuchinja. Yanataka yaendelee kufanya ufedhuli bila kuzuiwa.
Eti yanasema yanashughulikia maji, elimu na afya. Yalikuwa wapi kushughulikia hayo tangu 1961? Yaeleze ni nchi gani iliyoendelea ambayo siku moja ilifika hatua ya kuacha kushughulikia maji, elimu na afya? Haya ni mambo ambayo nchi zote zinaendelea kushughulikia mpaka mwisho wa dunia. Hata Marekani, UK, Japan... zinashughulikia haya mambo mpaka leo hii. Biden kasema bajeti yake kubwa inakwenda mwenye miundombinu. Hata Marekani bado inashughulika na miundombinu. Hakuna siku hii kazi itaisha. Mbona 1961, Nyerere hakusubiri kila kijiji kipate maji na umeme kwanza ndio nchi ipate katiba? Mbona 1977, Nyerere, Jumbe na akina Msekwa hawakusubiri mpaka tuingie uchumi wa kati ndio katiba ya 1977 iandikwe?
Halafu yanasema katiba siyo sera yao. Akina JK, Waryoba, Butiku... ni UKAWA? Yaleyale aliyopita kukusanya maoni (Polepole, Kabudi, etc.) leo yanasema katiba mpya haihitajiki!! Yaani Tanzania hii ina majitu ya ajabu sana sana. Tena yanaongoza nchi eti! What a shame and disgrace to the country!
Tuikatae hii katiba kwa nguvu zetu zote.