Katiba yetu ni ya kwanza kwa ubovu duniani

Katiba yetu ni ya kwanza kwa ubovu duniani

CCM inaipinga katiba mpya kwa nguvu zote. Kwa sasa hatuna katiba na ndio unamwona Magufuli anasema mahakama nyang'anya pesa watu wote washitakiwao, kisha anakuja Samia na kusema futa kesi zote na warudishie pesa zao. Magufuli anasema atakaekubali masharti ya ujenzi wa bandari ya bagamoyoni Mwendawazimu, anakuja Suluhu anasema ni anza ujenzi. Katiba haitapatikana kwa maombi, bali kwa gharama kubwa sana.

Hivi umepitia vizuri hoja yangu niliyomuuliza mtoa mada?
 
Kuna ajenda imejificha hapo na kuibiliwa hoja hiyo wakati huu ni mkakati ambao wapiga debe hawafahamu.Amini nakuambia Leo ikitolewa Ruhusa ya kuunda Katiba mpya wataibuka na jingine.
 
Umekwishajibiwa. Nenda library ya UDSM hapo. Kuna dissertations kibao. Hamu yako ya tafiti itakatwa.

Leta hapa hiyo dissertation, mbona mnapenda kubwabwaja bila kuwa na authority?

Halafu nimegundua, katika jukwaa ambalo lina watu ambao ni weupe sana. Anaweza kueleza senteso moja tu kutoka katika halmashauri ya kichwa chake, ikawa thread tayari. Hamna citing of authority wala nini. Ukiuliza tu, hilo umelotoa wapi. Utakoma na mvua ya matusi.
 
Amka, amka, usilale...Katiba mpya inakuja hiyo. Tafuta kazi nyingine kama kula yako kunategemea katiba mbovu ya sasa.
Matusi ndiyo jadi yenu. Wee lete huo utafiti kama utaniona nakunanga kiasi hiki.
 
Kwanza weka chanzo cha hiyo riwaya yako, pili hiyo ni hypothesis au thesis? tatu huwezi kutoa shutuma kwa katiba yetu bila kuwa na hoja dhahiri na kufanya upembuzi yakinifu kuthibitisha huo ubovu unaodai kwa kiwango hicho cha kimataifa. Wasiwasi wangu hujawahi isoma katiba na hujui sayansi na falsafa ya katiba. Ni kweli tunahitaji mabadiliko yatakayochochea demokrasia na ustawi wa taifa, lakini si lazima sana katiba mpya.
 
KATIBA yetu ni BORA MNOO....

Walioweka kipengele cha KUTOPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI walikuwa sahihi Sana....HAWAKUKOSEA...

Kivipi ?!!!

- Katiba ya 1977 ilitengenezwa kabla ya ujaji wa vyama vingi....

Kwa hiyo hapa hakuna SABABU ya kutengeneza mazingira ya kuibeba CCM!

-Hizi nchi zetu za KIAFRIKA ukiruhusu DEMOKRASIA ya kuyapinga matokeo mahakamani basi utaanza kutengeneza mazingira ya UBISHANI WA KISIASA usiokoma....wako watu watakaokuwa wanapinga kila uchao na huweza hata KUCHOCHEA HARAKATI ZA UASI WA KIMAPINDUZI na kuikosesha nchi utulivu(hapa ikumbukwe kuwa wanasiasa ndio wanaoongoza kuleta machafuko na Vita katika hizi nchi za kiafrika)....

Kwa hiyo KATIBA yetu ilitangulia mbele na kuwaepuka "watu aina hiyo".....

#NchiKwanza
#KaziIendelee
#UchumiKwanza
#KatibaYetuNiBora
#WananchiWalioWengiHawahitajiKatibaMpya
 
Amka, amka, usilale...Katiba mpya inakuja hiyo. Tafuta kazi nyingine kama kula yako kunategemea katiba mbovu ya sasa.
Katiba mpya si hitaji la watanzania walio wengi.....

Katiba mpya haiko ndani ya ilani ya UCHAGUZI ya CCM ...

CCM haikuiweka kipengele cha KATIBA MPYA na watanzania WAKAKICHAGUA kwa KISHINDO na kuwanyima kura CHADEMA WALIOKUWA na KIPENGELE hicho cha katiba mpya....

Katiba ina Mambo mengi....si tu UCHAGUZI NA TUME HURU.....

Mchakato wa katiba mpya hauwezi pekee kuhodhiwa na WANASIASA walio wachache kuliko makundi mengine......

#KatibaIliyopoNiNzuri
 
Kwanza weka chanzo cha hiyo riwaya yako, pili hiyo ni hypothesis au thesis? tatu huwezi kutoa shutuma kwa katiba yetu bila kuwa na hoja dhahiri na kufanya upembuzi yakinifu kuthibitisha huo ubovu unaodai kwa kiwango hicho cha kimataifa. Wasiwasi wangu hujawahi isoma katiba na hujui sayansi na falsafa ya katiba. Ni kweli tunahitaji mabadiliko yatakayochochea demokrasia na ustawi wa taifa, lakini si lazima sana katiba mpya.
Hakika 👍
 
Suala ninalohoji, umejuaje kama Tanzania ina katiba mbovu kuliko zote?
Leta Taarifa ya utafiti wako.
Aitoe wapi?!!

Kakariri huyo....

Huko anakosema Kuna katiba bora ni vyema akatubainishia tupajue.....
 
Mwana JF,

Hebu fikiria hili. Katiba yetu inasema Tume ya Uchaguzi ikishamtangaza mtu hakuna mtu anaruhusiwa kupinga matokeo mahakamani. Ulishafikiria siku mwenyekiti wa tume akimtangaza mtu yeyote kuwa Rais itakuwaje?..
Kwani Magu anasemaje huko motoni
 
Watz hata muongozwe na msafu na biblia bado ni tatizo

Utiì wa katiba au sheria hamna mnakalia kupiga kelele tuuuu kila kukicha

Mabadiliko ya katiba huanzia kwenye UTII wa KATIBA sito mdomoni

Kama viongozi na mahakama wanasigina HAKI waziwazi na Jaji Mkuu yupo unategemea nini?
 
Back
Top Bottom