Mimi sina shida na katiba mpya. Shida yangu ni upotoshaji mnaoutoa, kana kwamba sisi hatuna uwezo wa kutumia akili zetu vizuri. Jengeni hoja za maana mnapotaka kuwaonesha watu kwa nini tunahitaji katiba mpya. Siyo ujinga huu wa kitoto mnaouandika humu. Eti katiba ya Tanzania ndiyo katiba mbovu zaidi duniani. Wee unafikiri sisi wote ni WAVIVU wa kufikiri?
Washauri wengi wa Rais wa marekani ni wapambe na wabeba mikoba tu.Sio wote ambao ni watumishi rasmi wa serikali, hao wawili walikuwa hawalipwi. Nafasi nyeti zote za utumishi US lazima zithibitishwe na Seneti.