Katibu BAKWATA Kagera akatwa mkono, mkataji auawa kwa kipigo

Haki ya "self defence" inaanzia wapi na kuishia wapi?

Huyo kamanda wa polisi anayedai waliohusika na mauaji ya huyo marehemu wanatafutwa ili kufikishwa mahakamani, haoni kama walikuwa wanajilinda ili wasishambuliwe na marehemu?

Au kamanda wa polisi hajui kama kuna kitu kinaitwa "self defence" kwenye sheria zetu? kwa maelezo yake ni kama vile anawaona watuhumiwa tayari wana hatia, sawa na wale wanaopiga mwizi na kumuua.

Nina wasiwasi hao watuhumiwa wa mauaji wasije kuhukumiwa kwa kosa la mauaji bila kukusudia. Ikitokea hivyo, dhana nzima ya "self defence" itakuwa haina maana tena.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kwa sheria zetu hapa Bongo, hao wote wako na hatia mpaka itakapothibitika vinginevyo.
 
Daadeki Ukisikia maamuzi magumu ndio haya sasa, mtu unazuga kufa huku mtu kasimama na panga hapo humuoni? Akikushushia la shingo?

Hio courage sina, ila ya Mbio sina mashaka na miguu yangu hata kidogo kama ni mizima.
 
Hicho kiganja ingekuwa Afrika kusini wangekirudishia na kukiunga tena na mkono.
 
Hii dini ni ya ovyo sana, waumini wake hawana subira, wana munkari. Mioyo yao haina toba, mtu akiamua kufanya ukatili anafanya bila hofu. Kama aliondolewa kazini angeshukuru tu akaendelee na mishe zingine. Kwenye dini nyingine mtu anafukuzwa kwenye kitengo kizuri cha kupiga hela, mtu mpaka amejenga jumba kubwa la kisasa, mara paap anafukuzwa kazini lakini haanzishi ugomvi labda awe ana hitilafu ya akili. Kiujumla hawa waumini huwa hawana hofu ya mungu kujizuia na uovu
 
ilibidi nijifanye nimefariki kwa hiyo akakata mara ya mwisho akaona mimi sijitingishi ndiyo akaondoka
Aisee mara gafla jamaa angekata panga la shingo ingekuwaje?
Dah! Yahya kaishapewa mabikra 72 huko alipo
 
Mkazi wa Muleba mkoani Kagera, Abdulmalick Yahya (42) ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi, baada ya kuonekana akimshambulia kwa panga Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kagera, Hamza Zacharia (43).

Kutokana na tukio hilo, Zacharia anauguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Bukoba. Shambulio hilo limesababisha apoteze kiganja cha mkono wa kushoto.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Februari 6, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amethibitisha tukio hilo lililotokea Ijumaa Februari mosi, mwaka huu.

Chatanda amesema uchunguzi wa awali umebaini Abdulmalick kabla ya kutekeleza tukio hilo, alikuwa mtunza stoo ya vifaa katika mradi wa ujenzi wa jengo la Bakwata Complex linalojengwa katika Manispaa ya Bukoba.

“Februari mosi, 2024 alifukuzwa kazi ya kutunza ghala (stoo) la vifaa vya ujenzi wa Complex hiyo na kamati ya ujenzi, akamtuhumu Katibu wa Bakwata kwamba ndiye chanzo cha hayo yote. Kwa hiyo akaplan (akapanga) kulipa kisasi,” amesema Kamanda Chatanda.

Amesema, “Kitendo hicho kilisababisha mashuhuda waliokuwepo kujaribu kumzuia asiendelee kumjeruhi na walipoona anageuka na kutaka kuwadhuru, walimshambulia hadi pale alipookolewa na polisi na kuwahishwa hospitalini. Hata hivyo, alifariki dunia akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Bukoba.”

Kamanda Chatanda amesema uchunguzi kuwabaini waliohusika kumshambulia na kusababisha kifo cha mtuhumiwa huyo unaendelea.

Amesema watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani.

“Tunawaomba wananchi kumrudia muumba wao, hilo litawaongeza hofu na kuthamini maisha ya wenzao. Pia jamii iepuke kujichukulia sheria mkononi, ndiyo maana mtu akikosea tunatakiwa kumkamata au kutoa taarifa kwa mamlaka za Serikali, ili sheria ichukue mkondo wake,” amesema.

Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta alipotafutwa hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Amesema mamlaka zinazoshughulikia makosa ya jinai ndiyo zenye mamlaka ya kulizungumzia.

“Unajua hizo taarifa unazosema ni jinai ziko polisi na mimi sipo niko safarini nje ya mkoa. Nami nasoma habari kama wanavyozisoma wengine, pengine nikifika nitafahamu na kulizungumzia,” amesema Sheikh Kichwabuta.

Shuhuda wa tukio hilo, Said Fabian amesema; “Alimkatakata panga kidogo mgongoni yule bwana (Zacharia) akadondoka katika hali ya kujitetea akaweka mkono kichwani, ili asikatwe panga kichwani, kwa hiyo yule bwana (Abdulmalick) alichofanya alikata palepale mkono ulipokuwa mpaka akautoa."

Majeruhi afunguka

Majeruhi wa tukio hilo, Zacharia amesema alilazimika kuigiza kwamba amefariki ili asiendelee kushambuliwa maeneo mengine ya mwili.

“Wakati anakata mimi na-guard (najikinga) na mkono, kwa hiyo kila akitupa panga mimi naweka mkono, hali ilivyoendelea hivyo ilibidi nijifanye nimefariki kwa hiyo akakata mara ya mwisho akaona mimi sijitingishi ndiyo akaondoka," amesema.
Mmmmmmmh
Aisee., ni hasira au majini yalimvamia?
 
Inaauuma sana! Asante Mungu sheria ya Asili imesimama pale ilipotakiwa!!
 
Haki ya "self defence" inaanzia wapi na kuishia wapi?

Huyo kamanda wa polisi anayedai waliohusika na mauaji ya huyo marehemu wanatafutwa ili kufikishwa mahakamani, haoni kama walikuwa wanajilinda ili wasishambuliwe na marehemu?

Au kamanda wa polisi hajui kama kuna kitu kinaitwa "self defence" kwenye sheria zetu? kwa maelezo yake ni kama vile anawaona watuhumiwa tayari wana hatia, sawa na wale wanaopiga mwizi na kumuua.

Nina wasiwasi hao watuhumiwa wa mauaji wasije kuhukumiwa kwa kosa la mauaji bila kukusudia. Ikitokea hivyo, dhana nzima ya "self defence" itakuwa haina maana tena.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Uchunguzi wa kipolice bado ni muhimu sana,kuna watu wabaya wanaweza pita humo pia kutimiza yao!!
 
Back
Top Bottom