Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UVCCM TAIFA - Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndugu Victoria C. Mwanziva Anena Kuhusu Uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
“Tunampongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko aliyoyafanya katika Baraza la Mawaziri pamoja na watendaji wakuu wa Wizara mbalimbali”
“Katika nafasi mbalimbali tumeona uwepo wa Viongozi vijana; hii ni imani kubwa kwa vijana wa Taifa hili katika nafasi muhimu. Tunaamini watafanya kazi kwa bidii ili kuendelea kujenga imani kwa vijana katika kutumikia taifa letu la Tanzania.”
“Tunatumia nafasi hii kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi ushirikiano thabiti katika utendaji wao; Kila la Kheri katika kusimamia kwa weledi Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi”
Ndugu Victoria C. Mwanziva
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa