Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema Rais Samia Suluhu Hassan alitumia njia ya maridhiano kuwapa upofu kwa muda wapinzani ili aweze kujipanga kukabiliana nao.
“Kumbe Mheshimwa Rais alikuwa anatuhadaa kwa hiyo Rais akataka kwanza awe na kipindi cha kutokusumbuliwa ili aweze kuishika nchi kwa hiyo wapinzani akatuhadaa ili tupunguze makashkash akaleta falsafa ya maridhiano kwamba anataka kuifungua nchi kumbe moyoni mwake anajua kwamba hapa alikuwa anatupotezea muda tu” amesema Ado
Soma, Pia: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini
Ado ameyasema hayo Februari 08, alipokuwa na ziara ya kichama wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani na kudai kuwa hivi sasa baadhi ya matukio kama ya kubambikiwa kesi kwa wanasiasa yamerejea akitolea mfano kesi ya utoaji wa taarifa za uongo inayomhusu aliyewahi kuwa Katibu katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa.