Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
Habari ya asubuhi ndugu wanajamvi, natumaini bila shaka mu wazima wa afya na mmeianza vema siku ya leo. Kwa ambao ni wagonjwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa awajalie nafuu ya haraka ili muweze kurejea katika majukumu yenu ya kila siku.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo atafanya mkutano na waandishi wa habari siku ya kesho Alhamisi ya tarehe 20/05/2021 saaa sita kamili mchana (06:00 Mchana) katika ukumbi wa Halmashauri Kuu (NEC) Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma. Matangazo ya moja kwa moja (mbashara) ya mkutano huu yatarushwa kupitia akaunti na kurasa za mitandao ya kijamii ya Chama Cha Mapinduzi, chaneli ya Youtube ya Chama Cha Mapinduzi, Chaneli Ten na vyombo mbalimbali vya habari vya nchini Tanzania.
Mkutano huu na waandishi wa habari utakuwa wa kwanza kwa Ndg. Daniel Chongolo kuufanya tangu alipoteuliwa na kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho tawala mnamo tarehe 30/04/2021 kushika wadhifa huo katika Chama. Pia mkutano huu unafanyika wakati ambao Chama Cha Mapinduzi kimetoka kushinda kwa kishindo uchaguzi mdogo wa wabunge katika majimbo mawili ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi Iendelee. Nawatakia siku njema yenye mafanikio, tufanye kazi kwa maendeleo yetu na taifa.