Katibu Mkuu CCM Taifa, Daniel Chongolo apiga stop "Uchawa" ndani ya UVCCM

Kwa hiyo zile nyaraka za kumpongeza Hangaya toka vikao halali huwa nikutuhadaa wanachama ikiwa kuna
Chuki
Vita
Uchawa
Fitina
Makundi nk

Ukiwa Mtendaji mkuu wa chama chenye dola nani au chama kipi huwa kinasababisha hayo.Kumbe Mbatia alikuwa sahihi.
Msajili anadharaulika kwa kuegemea upande mmoja.Tangu lini baba unaita watoto halafu wanakugomea na wanakupa mashariti uachane na mama kwanza
 
KATIBU MKUU WA CCM NDG. CHONGOLO AITAKA UVCCM KUACHA KUWA WAPAMBE BINAFSI WA VIONGOZI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kutumia umoja wa vijana wa chama hicho kujenga miundombinu pamoja na miradi ya maendeleo wanayoanzisha kwenye maeneo yao.

Katibu Mkuu ametoa maagizo hayo leo tarehe 15 Novemba, 2021 baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa ambavyo vinajengwa kwa nguvu ya umoja wa vijana wa CCM katika shule ya Bukama, kata ya Kagoma wilayani Muleba, Mkoani Kagera.

Amesema malengo ya kuanzisha umoja wa vijana haikuwa na maana ya kuwatumia vijana hao kwenye mambo ya kutafuta kura za wagombea na kuhangaika na masuala binafsi ya viongozi, bali ni kujenga nchi kwa kujitolea na baadae kupata fursa ya kwenda kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi.

Amesema miaka ya nyuma kazi ya umoja wa vijana ilikuwa ni kujiitolea kujenga miundombinu na kufanya mambo mengine ya maendeleo na baadae kupata fursa ya kwenda jeshini kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi kwa ujumla.

“Miaka ya 2000 nyuma, asilimia tisini ya vijana ambao walikuwa wanachukuliwa kwenda jeshini walikuwa wanatokana na umoja wa vijana na ni kwa sababu walikuwa wanajitolea kulitumika taifa kwa kupitia umoja huo,” amesema.

Amesema kuwa kwa sasa vijana wengi wa umoja wa vijana wamekuwa wapambe namba moja ya wagombea na waangaikaji wa mambo binafsi ya viongozi huku wakiacha majukumu yao halisi.

Katika hatua nyingine Ndg. Chongolo amewapongeza umoja wa vijana Wilaya ya Muleba, kwa kujitolea kujenga vyumba vya madarasa huku akimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na viongozi wengine wa Muleba kuendelea kuwatumia vijana hao katika kujenga miundombinu mingine kwani tayari wameonesha utayari na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa moyo.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
KM pigakazi kaka,
 
Wewe utaacha Uchawa kweli?
Kwa hiyo ukiyasemea mazuri ya chama ni uchawa??!

Kuelezea itikadi njema ya CCM si uchawa.....kwani huko si kujikomba kwa MTU/WATU.....

Na Kama hata kuielezea CCM utaniita chawa basi endelea tu kwani sitoacha kukielezea kwa mazuri yake.......

Siempre CCM
 
KATIBU MKUU WA CCM NDG. CHONGOLO AITAKA UVCCM KUACHA KUWA WAPAMBE BINAFSI WA VIONGOZI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kutumia umoja wa vijana wa chama hicho kujenga miundombinu pamoja na miradi ya maendeleo wanayoanzisha kwenye maeneo yao.

Katibu Mkuu ametoa maagizo hayo leo tarehe 15 Novemba, 2021 baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa ambavyo vinajengwa kwa nguvu ya umoja wa vijana wa CCM katika shule ya Bukama, kata ya Kagoma wilayani Muleba, Mkoani Kagera.

Amesema malengo ya kuanzisha umoja wa vijana haikuwa na maana ya kuwatumia vijana hao kwenye mambo ya kutafuta kura za wagombea na kuhangaika na masuala binafsi ya viongozi, bali ni kujenga nchi kwa kujitolea na baadae kupata fursa ya kwenda kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi.

Amesema miaka ya nyuma kazi ya umoja wa vijana ilikuwa ni kujiitolea kujenga miundombinu na kufanya mambo mengine ya maendeleo na baadae kupata fursa ya kwenda jeshini kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi kwa ujumla.

“Miaka ya 2000 nyuma, asilimia tisini ya vijana ambao walikuwa wanachukuliwa kwenda jeshini walikuwa wanatokana na umoja wa vijana na ni kwa sababu walikuwa wanajitolea kulitumika taifa kwa kupitia umoja huo,” amesema.

Amesema kuwa kwa sasa vijana wengi wa umoja wa vijana wamekuwa wapambe namba moja ya wagombea na waangaikaji wa mambo binafsi ya viongozi huku wakiacha majukumu yao halisi.

Katika hatua nyingine Ndg. Chongolo amewapongeza umoja wa vijana Wilaya ya Muleba, kwa kujitolea kujenga vyumba vya madarasa huku akimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na viongozi wengine wa Muleba kuendelea kuwatumia vijana hao katika kujenga miundombinu mingine kwani tayari wameonesha utayari na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa moyo.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Kaziiendelee Team, We proud on you,
 
[emoji116]
IMG_20211116_114850.jpg
 
Kaziiendelee
 
Back
Top Bottom