Katibu Mkuu CCM usimtishe Mbunge, tunaomba uishauri Serikali Wabunge wote na viongozi waanze kukatwa kodi

Katibu Mkuu CCM usimtishe Mbunge, tunaomba uishauri Serikali Wabunge wote na viongozi waanze kukatwa kodi

Hilo nalo muhimu, wote tulipe kodi kwa kadiri ya kipato chetu, kama kweli sote ni wazalendo.
Hili ndilo nataka sote tuseme tusipoteze muda kutaka mbunge ajiuzulu tukasahau kuwa hoja inatakiwa viongozi wote tulipe kodi
 
Nadhani na yeye kama mwananchi / mlipa kodi anahaki ya kuzungumza mawazo yake (hata kama unayaona ni pumba); Pia kama Kiongozi katika Chama husika nadhani pia ana haki ya kuongea..., kama wewe ulivyo na haki hapa ya kumkosoa
 
Hueleweki hoja yako ni nini! Unataka waongezewe mishahara halaf wakatwe kodi au wasiongezewe mishahara kabisa! Maana hoja ya katibu mkuu ni kuwa mishahara inatosha,asietaka aache..wewe unataka wakatwe kodi, katika mishahara ipi? Hii hii iliyopo au waongezewe ndo wakatwe kodi?
Soma kabisa vizuri ...... nimesema wazi tusijikite tuu kuwatataka watu wasiseme wanayo yahisi kwao na tukasahau kuwa hoja ya msingi hapa ni watu wote walipe kodi.
 
Hizi sarakasi hazisaidii kilichopo hawa watu waanze kulipa kodi,mishahara yao pamoja na posho zao hazikatwi kodi kwa nini? Baada ya miaka 5 wanapewa pension ya wizi
Hakika...
 
Kwa masikitiko makubwa hoja hii ya Mbunge aliileta wakati ambao sio mwafaka kwani kuna malalamiko mengi sana kwenye Sector ya Umma kutokulipwa mishahara stahiki na kupandishwa vyeo. Rais wa awamu ya tano alisema hatoongeza mishahara kutokana na kisingizio cha hali ngumu ilhali tukiona ujenzi kila mahali ujenzi unaoashiria kutokuweza kurejesha faida tarajiwa kwa wananchi.
 
Kwa masikitiko makubwa hoja hii ya Mbunge aliileta wakati ambao sio mwafaka kwani kuna malalamiko mengi sana kwenye Sector ya Umma kutokulipwa mishahara stahiki na kupandishwa vyeo. Rais wa awamu ya tano alisema hatoongeza mishahara kutokana na kisingizio cha hali ngumu ilhali tukiona ujenzi kila mahali ujenzi unaoashiria kutokuweza kurejesha faida tarajiwa kwa wananchi.
Chama cha mapinduzi kinaona hatari iliyopo kwenye hoja hii. Katibu Mkuu alichokisema ni sahihi ni katika kukiepusha chama toka kwenye hasira za wananchi.
 
Mbunge kimsingi anatakiwa kujitolea kuwawakilisha wananchi wake, ndo maana anatakiwa awe amejitosheleza kimapato na siyo kwenda kulialia njaa kwa serikali apewe pesa ya kula, hapo anakuwa sawa na mganga njaa. Tunahitaji wabunge na siyo waganga njaa kutoka huko majimboni.

Sio lazima mbunge awe tajiri, kikubwa awe amechaguliwa kwa kufuata utaratibu sahihi kuwawakilisha wananchi katika chombo cha kutunga sheria.
Kwanini wabunge wamejiwekea mishahara mikubwa, kujipangia wasilipe kodi ni kwa sababu wao wamekuwa wakinunua kura za wananchi, sasa ili undelee kuchagulia inabidi ulipe fadhila kwa kuonekana wewe unatoa misaada zaidi ya serikali.
Na ili kuhakikisha kuwa maslahi yao yanalindwa wamekuwa wakihongana na Viongozi Wakuu kama vile kutoa kinga ya kushtakiwa kwa viongozi kama Raisi, Spika, Naibu Spika etc...
Ili kuwalipa wabunge kwa kupitisha hizo sheria mbovu mbovu , nao wanatolewa kodi kwenye mafao yao, mishahara, na kuongezewa marupu rupu, safari etc..
Ni mfumo wa kula tu kwa kwenda mbele.
 
Kama unatambua kazi, majukumu ya mbunge huwezi kumuunga mkono Maganga. Kuwagawia wananchi hela, kutoa misaada kwa wananchi sio jukumu la Mbunge.

Mbunge anatakiwa kuhamasisha wananchi kujipatia maendeleo yao, na kuisimamia vizuri miradi ya maendeleo jimboni kwake ambayo ndio itapunguza shida kwa wananchi wake.

Kama kila mbunge atataka kulipwa hela ya kuhonga wananchi wake ili wamchague tena, ni mshahara kiasi gani utatosha?

Halafu hizo pesa za kuwahonga wananchi tutazi kagua vp. Tutajuaje kama katika million 2 tuliyompa kwa ajili yetu sisi wananchi, yote amewapa walengwa?
 
Hakuna haja ya kumtisha mbunge. Chongolo bado ana vimelea vya ubabe alivyorithi kwa mwendazake. Hayo ni maoni yake na siyo lazima asakamwe. Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya demokrasia na uhuru wa kujieleza na wa kutoa maoni. Kila swali lina jibu. Sasa kama Chongolo hana jibu kwa swali hilo basi anyamaze. Acha watu watoe maoni yao na waulize maswali, mwenye jibu atoe asiye na jibu anyamaze. Ubabe ubabe huu haufai hata kidogo.
 
Hili ndilo nataka sote tuseme tusipoteze muda kutaka mbunge ajiuzulu tukasahau kuwa hoja inatakiwa viongozi wote tulipe kodi
Kwani umeambiwa mshahara wa Mbunge haukatwi kodi? Mshahara wake unakatwa kodi kama kawaida visivyokatwa kodi ni posho kwa hiyo kama ni kulalamika Kutokatwa kodi tulalamikie posho zao na si mishahara yao
 
Hakuna haja ya kumtisha mbunge. Chongolo bado ana vimelea vya ubabe alivyorithi kwa mwendazake. Hayo ni maoni yake na siyo lazima asakamwe. Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya demokrasia na uhuru wa kujieleza na wa kutoa maoni. Kila swali lina jibu. Sasa kama Chongolo hana jibu kwa swali hilo basi anyamaze. Acha watu watoe maoni yao na waulize maswali, mwenye jibu atoe asiye na jibu anyamaze. Ubabe ubabe huu haufai hata kidogo.
Kwa nini jibu la Chongolo na Zitto ulione sio la kidemokrasia ila swali la anaetaka nyongeza likawa ndio la kidemokrasia?
 
Kwanini tusiwe na suluhu la kudumu na la manufaa kwa taifa? kwanini hoja isiwe wabunge na viongozi wengine kulipa kodi?
Kwa hiyo wao kukatwa Kodi ndio uhalali wa kuongezewa Mishahara!? Mbona hizi Ni hoja 2 tofauti?
 
Kwa nini jibu la Chongolo na Zitto ulione sio la kidemokrasia ila swali la anaetaka nyongeza likawa ndio la kidemokrasia?
Wao wanajibu kwa kumkandia mtoa hoja na wanamwona kakosea kutoa hoja hiyo. Heshimu hoja ya mtoa hoja na kisha utoe maoni yako. kwani ubaya wa hoja ya mbunge ni upi? Je, wewe hupendi kipato chako kiongezeke? Mimi binafsi napenda kipato changu kiongezeke ila kuna vikwazo kufikia matamanio yangu hayo.

Kwangu ningekuwa ndio mjibu hoja ya mbunge ningesema hivi: Hoja ya mbunge ni nzuri maana kila mtu hupenda kuwa bora na kuwa na hali nzuri zaidi, ila inashindikana kwa sababu uchumi wetu hauturuhusu. pale hali ya uchumi ikiwa nzuri tutaboresha kipato na ustawi wa wafanyakazi wa makundi mbalimbali na sekta mbalimbali ikiwemo wabunge, wafanyakazi wa bunge na kwa watanzania wote kwa ujumla wao.
 
Sasa kama ni issue ya kulipa kodi itabidi mabalozi wa kuhamasisha kulipa kodi akina Hamisa Mabetto et al watinge bungeni wawahamasishe wabunge...
 
Afutiwe uanachama. Ili arudi uraiani, hatukumutuma kwenda kuomba mishahara yao ipande.

Kama aliona hakuna hela nani alimlazisha kugombea.

2025 huyu HAYUPO akae akijua

Kodi za laini ALIPIGA MAKOFI na kuunga mkono Hoja

Tunasemaaa 2025 Hayupooooo
 
Mnamshambulia mwenzenu kwa wivu tu.

Hakuna mtu ambae hataki kuongezewa mshahara popote anapofanya kazi hata kama analipwa zaidi ya mshahara wa mbunge.

Jibu sahihi aambiwe tu hakuna pesa basi.
 
Kweli huyu mbunge hamnazo yaani yeye anataka hela ya kuwahonga wananchi ili wamchague tena,kuna haja ya kuwa na katiba mpya
 
MBUNGE AACHIE JIMBO!

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mbunge wa Mbongwe, Nicodemus Maganga kama anataka kuhudumia wananchi afuate utaratibu wa nchi na akitaka kulipwa kwa dola ahamie katika nchi zinazofanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aliopohijiwa na gazeti la Nipashe

Kwa upande wake kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala hilo alisema

Kama maslahi hayatoshi aache kazi ya Ubunge.

"Wabunge wasipoogopa wananchi hawatakuwa wabunge, Wakati Rais anawaambia wafanyakazi hawawezi kupandishia mishahara kwa sababu ya hali ya uchumi, Mbunge anataka malipo zaidi ni hujuma kwa Rais"

Maoni yangu:
Kwanza kabisa niseme wazi kabisa Mimi nilipata wasaha wa kumsikiliza vizuri mbunge aliyesema wazi kuwa mishahara yao wabunge haiwatoshi na alieleza vizuri kabisa kwanini aseme hayo, na mimi nilitarajia kabisa haya ni maoni yake binafsi na anao uhuru wa kutoa maoni yake akiwa bungeni na kama ni hukumu basi sisi wananchi ndio tunajua chakufanya.

Kwenye hili kumekuwa na unafiki mwingi sana na wengi watajidai kuwa hawaungi mkono hoja ya Maganga lakini ukweli ni kwamba wabunge wote kwenye mioyo yao wanaunga mkono hoja lakini wanaogopa wananchi kuusema ukweli. Ukimsikiliza Maganga akijieleza vyema utamuelewa kuwa wabunge wanao mzigo mkubwa sana pamoja na mshahara huo unaotajwa.


Nimeshangazwa na Katibu mkuu bwana Chongolo kumtishia mbunge anayetoa maoni yake na kusema kama hataki aachie ubunge hii ni kinyume kabisa na haki za bunge na mbunge na pia uhuru wa maoni.

Kama kweli tunajali wananchi na wewe ni katibu mkuu tunaomba ukishauri chama na serikali mishahara ya wabunge na viongozi wote ianze kukatwa kodi kama wafanya kazi wengine na wananchi wengine.

Ukweli ni kwamba wabunge na viongozi wakubwa mishahara yao haikatwi kodi kwa hiyo wanakula tuu mishahara kama ilivyo na hii hoja ya mbunge Maganga iwe chachu ya kubadilisha sheria zetu na kuishauri serikali kubadili sheria ili kila mtu alipe kodi sio kuwahamisha wananchi kulipa kodi huku wengine tena kundi kubwa lenye kipato kikubwa halilipi kodi.

Kwako katibu mkuu Chongolo.
Hoja ya mshahara mdogo na kutokatwa kodi ni mada mbili tofauti. Yeye kutoa misaada kwa wapiga kura kama iko kwenye majukumu yake aendelee.
 
Kuna watu wapo tayari kulipwa ml. 1 kwa mwezi bila posho wafanye hyo kazi ya ubunge# wabunge walipe kodi
 
Back
Top Bottom