Katibu Mkuu CCM usimtishe Mbunge, tunaomba uishauri Serikali Wabunge wote na viongozi waanze kukatwa kodi

Hilo nalo muhimu, wote tulipe kodi kwa kadiri ya kipato chetu, kama kweli sote ni wazalendo.
Hili ndilo nataka sote tuseme tusipoteze muda kutaka mbunge ajiuzulu tukasahau kuwa hoja inatakiwa viongozi wote tulipe kodi
 
Nadhani na yeye kama mwananchi / mlipa kodi anahaki ya kuzungumza mawazo yake (hata kama unayaona ni pumba); Pia kama Kiongozi katika Chama husika nadhani pia ana haki ya kuongea..., kama wewe ulivyo na haki hapa ya kumkosoa
 
Soma kabisa vizuri ...... nimesema wazi tusijikite tuu kuwatataka watu wasiseme wanayo yahisi kwao na tukasahau kuwa hoja ya msingi hapa ni watu wote walipe kodi.
 
Hizi sarakasi hazisaidii kilichopo hawa watu waanze kulipa kodi,mishahara yao pamoja na posho zao hazikatwi kodi kwa nini? Baada ya miaka 5 wanapewa pension ya wizi
Hakika...
 
Kwa masikitiko makubwa hoja hii ya Mbunge aliileta wakati ambao sio mwafaka kwani kuna malalamiko mengi sana kwenye Sector ya Umma kutokulipwa mishahara stahiki na kupandishwa vyeo. Rais wa awamu ya tano alisema hatoongeza mishahara kutokana na kisingizio cha hali ngumu ilhali tukiona ujenzi kila mahali ujenzi unaoashiria kutokuweza kurejesha faida tarajiwa kwa wananchi.
 
Chama cha mapinduzi kinaona hatari iliyopo kwenye hoja hii. Katibu Mkuu alichokisema ni sahihi ni katika kukiepusha chama toka kwenye hasira za wananchi.
 

Sio lazima mbunge awe tajiri, kikubwa awe amechaguliwa kwa kufuata utaratibu sahihi kuwawakilisha wananchi katika chombo cha kutunga sheria.
Kwanini wabunge wamejiwekea mishahara mikubwa, kujipangia wasilipe kodi ni kwa sababu wao wamekuwa wakinunua kura za wananchi, sasa ili undelee kuchagulia inabidi ulipe fadhila kwa kuonekana wewe unatoa misaada zaidi ya serikali.
Na ili kuhakikisha kuwa maslahi yao yanalindwa wamekuwa wakihongana na Viongozi Wakuu kama vile kutoa kinga ya kushtakiwa kwa viongozi kama Raisi, Spika, Naibu Spika etc...
Ili kuwalipa wabunge kwa kupitisha hizo sheria mbovu mbovu , nao wanatolewa kodi kwenye mafao yao, mishahara, na kuongezewa marupu rupu, safari etc..
Ni mfumo wa kula tu kwa kwenda mbele.
 

Halafu hizo pesa za kuwahonga wananchi tutazi kagua vp. Tutajuaje kama katika million 2 tuliyompa kwa ajili yetu sisi wananchi, yote amewapa walengwa?
 
Hakuna haja ya kumtisha mbunge. Chongolo bado ana vimelea vya ubabe alivyorithi kwa mwendazake. Hayo ni maoni yake na siyo lazima asakamwe. Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya demokrasia na uhuru wa kujieleza na wa kutoa maoni. Kila swali lina jibu. Sasa kama Chongolo hana jibu kwa swali hilo basi anyamaze. Acha watu watoe maoni yao na waulize maswali, mwenye jibu atoe asiye na jibu anyamaze. Ubabe ubabe huu haufai hata kidogo.
 
Hili ndilo nataka sote tuseme tusipoteze muda kutaka mbunge ajiuzulu tukasahau kuwa hoja inatakiwa viongozi wote tulipe kodi
Kwani umeambiwa mshahara wa Mbunge haukatwi kodi? Mshahara wake unakatwa kodi kama kawaida visivyokatwa kodi ni posho kwa hiyo kama ni kulalamika Kutokatwa kodi tulalamikie posho zao na si mishahara yao
 
Kwa nini jibu la Chongolo na Zitto ulione sio la kidemokrasia ila swali la anaetaka nyongeza likawa ndio la kidemokrasia?
 
Kwanini tusiwe na suluhu la kudumu na la manufaa kwa taifa? kwanini hoja isiwe wabunge na viongozi wengine kulipa kodi?
Kwa hiyo wao kukatwa Kodi ndio uhalali wa kuongezewa Mishahara!? Mbona hizi Ni hoja 2 tofauti?
 
Kwa nini jibu la Chongolo na Zitto ulione sio la kidemokrasia ila swali la anaetaka nyongeza likawa ndio la kidemokrasia?
Wao wanajibu kwa kumkandia mtoa hoja na wanamwona kakosea kutoa hoja hiyo. Heshimu hoja ya mtoa hoja na kisha utoe maoni yako. kwani ubaya wa hoja ya mbunge ni upi? Je, wewe hupendi kipato chako kiongezeke? Mimi binafsi napenda kipato changu kiongezeke ila kuna vikwazo kufikia matamanio yangu hayo.

Kwangu ningekuwa ndio mjibu hoja ya mbunge ningesema hivi: Hoja ya mbunge ni nzuri maana kila mtu hupenda kuwa bora na kuwa na hali nzuri zaidi, ila inashindikana kwa sababu uchumi wetu hauturuhusu. pale hali ya uchumi ikiwa nzuri tutaboresha kipato na ustawi wa wafanyakazi wa makundi mbalimbali na sekta mbalimbali ikiwemo wabunge, wafanyakazi wa bunge na kwa watanzania wote kwa ujumla wao.
 
Sasa kama ni issue ya kulipa kodi itabidi mabalozi wa kuhamasisha kulipa kodi akina Hamisa Mabetto et al watinge bungeni wawahamasishe wabunge...
 
Afutiwe uanachama. Ili arudi uraiani, hatukumutuma kwenda kuomba mishahara yao ipande.

Kama aliona hakuna hela nani alimlazisha kugombea.

2025 huyu HAYUPO akae akijua

Kodi za laini ALIPIGA MAKOFI na kuunga mkono Hoja

Tunasemaaa 2025 Hayupooooo
 
Mnamshambulia mwenzenu kwa wivu tu.

Hakuna mtu ambae hataki kuongezewa mshahara popote anapofanya kazi hata kama analipwa zaidi ya mshahara wa mbunge.

Jibu sahihi aambiwe tu hakuna pesa basi.
 
Kweli huyu mbunge hamnazo yaani yeye anataka hela ya kuwahonga wananchi ili wamchague tena,kuna haja ya kuwa na katiba mpya
 
Hoja ya mshahara mdogo na kutokatwa kodi ni mada mbili tofauti. Yeye kutoa misaada kwa wapiga kura kama iko kwenye majukumu yake aendelee.
 
Kuna watu wapo tayari kulipwa ml. 1 kwa mwezi bila posho wafanye hyo kazi ya ubunge# wabunge walipe kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…