Katibu Mkuu CECAFA - adai yanga si chochote kujitoa kwao hakutaathiri mashindano,hata wakishiriki wamezoea kubamizwa magoli mengi

Katibu Mkuu CECAFA - adai yanga si chochote kujitoa kwao hakutaathiri mashindano,hata wakishiriki wamezoea kubamizwa magoli mengi

Mzee anawakebehi wale waliokula khamsa kule Congo na Misri! Ila kama kweli kasema hivyo atakuwa hana adabu!
yanga.JPG
 
Ugomvi wa MUSONYE na Yanga ulianza Yanga ilipokataa kupeleka kombe Burundi baada ya Yanga kudhulumiwa dola 10,000 na CECAFA/FAT.

Nyingine Yanga ilipotolewa kwa hila na Police Uganda kwa kukataliwa goli la kusawazisha la Thomas Mourice Yanga wakaapa lazima na Simba watolewe ndipo Simba naye akapigwa 2-1 na Moro United
MUSONYE ilimuuma mno na kutamka yanga wanafitna sana .fainali ikawa Police Uganda na Moro United.

MUSONYE vs Yanga mechi ambayo yanga waligomea mshindi wa tatu ,hapa Povu lilikuwa halisomeki Yanga ikafungiwa.

Musonye vs Yanga siku pekee aliyochekelea ni pale Yanga ilipoipiga timu ya Uganda kwenye robo fainali 3-2 hapo Musonye alirukaruka maana Yanga na Simba zilikutana na fedha nyingi kupatikana.

Musonye vs Yanga ya Maximo yanga ilipeleka kikosi nusu mashindano yalifanyika Rwanda ,Yanga iliondolewa mashindanoni na kashfa kibao.

Musonye vs Yanga mashindano yaliyopita Yanga ilipojitoa povu lilimtoka pia Azam wakaingia fainali na Simba na kubeba ndoo.

Musonye hufurahia sana Yanga ikishiriki ,wasiposhiriki anakerekwa mno.
 
Mpuuzi sana, sasa kama alijua Yanga si lolote kwenye mashindano yake kwa mini aliipa mwaliko, INA maana kwao Kenya alikosa timu za kualika hadi aialike Yanga ambayo haina vigezo. Huyu siku akikanyaga ardhi ya Tz inabidi tumtie adabu kwa mikwenzi ndiyo atajuwa sisi si wa mchezo mchezo akawachezee Kariobangi na sofapaka kwao huko. Nina hasira naye huyu dictator was cecafa
Hahaha punguza hasira mkuu..
Huyu jamaa anajua hapa east africa derby kubwa ni simba na yanga. Ndo maana msimu wa juzi.kati aliwapanga kundi moja simba sijui wakashtukia! Wakasepa!
Musonye akiondoka cecafa anakufa maskini yule..

Naipongeza yanga,simba kwa kujitoa
 
Hahaha punguza hasira mkuu..
Huyu jamaa anajua hapa east africa derby kubwa ni simba na yanga. Ndo maana msimu wa juzi.kati aliwapanga kundi moja simba sijui wakashtukia! Wakasepa!
Musonye akiondoka cecafa anakufa maskini yule..

Naipongeza yanga,simba kwa kujitoa
Akafie mbele huko, anaboa sana mkuu. Haya mashindano zamani yalikuwa na hadhi sana, lakini tokea huyu mpuuzi aingie CECAFA yanazidiwa na ndondo cup. Bahati yake angekuwa hapa kwetu tungeisha mtia Lupango maana ni mlafi sana.
 
Back
Top Bottom