Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Ametakiwa yeye arudi kituo chake cha kazi, hawezi kujitetea mbona mwenzake hajarudi, atekeleze alichotakiwa kufanya
Kwanini arudi kipindi hiki ambacho amekataa kuwa chaka na si wakati mwingine? Kwamj kuwa chawa lazima?
 
Akirudi ana kuta barua mezani ya uhamisho kwenda swekeni kama sio tukuyu Au huko nkasi basi mabamba mpakani na burundi [emoji23][emoji23][emoji23]
Atahamishiwa kwenye ile wilaya aliyokataa uteuzi wa kua mkuu wa wilaya. Sirikali ni lidude likubwa sana huwezi kua ndani yake halafu ukashindana nayo hautashinda
 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeanza mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu.

Maganga ambaye cheo chake ni Mwalimu Mwandamizi katika Manispaa ya Temeke, aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT Agosti 2017 hadi Septemba 30, 2020, akaomba tena Juni 1, 2020 na kumalizika Septemba 30, 2023, na baadaye aliomba kibali hicho kwa mara ya tatu lakini Katibu Mkuu UTUMISHI hakuridhia maombi hayo na kumtaka kurejea kwenye kituo chake cha kazi cha awali.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amesema Maganga ni mtumishi wa Temeke na alitakiwa kuripoti kazini kama alivyotakiwa katika tangazo la wito, lakini hadi sasa hajaripoti, hivyo kinachofanyika ni kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.

"Yule ni mtumishi wa Serikali hapaswi kuigomea Serikali, sisi tunachojua yeye ni mtumishi wetu, kule aliko kibali kimeisha sio tena sehemu yake ya kazi, amesema.

Maganga alichaguliwa Desemba 2022 na Mkutano Mkuu wa CWT kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Deus Seif
ambapo awali alikwa akitumikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.

Mnamo Januari 25, mwaka huu, Maganga, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Mathaman hawakufika kuapa.

Swahili Times.

Pia soma:
Status ya huyu Japhet Maganga ikoje? Je amekwisha ripoti TEMEKE kwenye shule aliyopangiwa?
 
Status ya huyu Japhet Maganga ikoje? Je amekwisha ripoti TEMEKE kwenye shule aliyopangiwa?
Alifunguliwa kesi ya utoro kazini baada ya kutoripoti kituoni kwake kwa zaidi ya siku 5 pasipo kutoa taarifa.
 
Kwamba nikiwa mwalimu siwezi kuacha kazi muda wowote ninaotaka Mimi????
 
Chezea Mshahara wake wa milioni 7 kwa mwezi, V8 VX aliyonunua katakana na makato ya Walimu kila Mwezi, anajilipa Honoraria hata milioni 10 akitakq, bado za safari za nje ya nchi kwa gharama za michango ya Walimu.

JE WEWE UNAWEZA KUACHA HAYO MAOKOTO WAKATI WALIMU WAMERITHIKA ATUMIE FEDHA ZAO KAMA ANAVYOTAKA ILI MRADI AWAPE T SHIRT MEI MOSI?
 
Chezea Mshahara wake wa milioni 7 kwa mwezi, V8 VX aliyonunua katakana na makato ya Walimu kila Mwezi, anajilipa Honoraria hata milioni 10 akitakq, bado za safari za nje ya nchi kwa gharama za michango ya Walimu.

JE WEWE UNAWEZA KUACHA HAYO MAOKOTO WAKATI WALIMU WAMERITHIKA ATUMIE FEDHA ZAO KAMA ANAVYOTAKA ILI MRADI AWAPE T SHIRT MEI MOSI?
Kwani hakuna Mamlaka iliyo juu yake?
 
Unamtoa mgodi wenye dhahabu unampeleka kwenye shamba la mate mbele, atawaelewa kweli

Ova
 
Back
Top Bottom