Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yuko Ikulu anapiga kazi!Nauliza kwa sababu kwa muda sasa nimekuwa nikimsikia Mh. Rais akimtambulisha Kaimu katibu Mkuu kiongozi ndugu Kusiruka! Je anaumwa au yupo wapi? kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa na mkuu wa utumishi wa umma nchini na katibu wa baraza la mawaziri na ndiye mkuu wa makatibu wakuu wote ningependa au tungependa kujua Je yupo wapi ndugu huyu?
Wapi?Yupo,
Yote unayosema ni sawa lakini kwa nini kila kwenye kuapishwa viongozi nafasi yake inakaimiwa na Bwana Kusiruka, toka anaapisha Wakuu wa mikoa hakuwepo na leo imepita zaidi ya wiki mbili hajaonekana tena, lazima Kuna shida sehemu si bureNafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi sio ya kisiasa . KMK anaweza akawa anatekeleza majukumu yake kimyakimya bila kulazimika kujitokeza hadharani
Hapo nyuma uliingizwa usanii kwenye utumishi wa uma. Waziri alikua anafanya kazi za katibu mkuu, katibu mkuu anafanya kazi za mkurugenzi wa idara. Mkuu wa idara atafanya kazi za maofisa wa kawaida kama makarani au hata wahudumu ili mradi kila mtu alikua anakwenda mbio kupata publicity ya kuonekana anafanya kazi na hivyo ajipendekeze kwa mamlaka ya uteuzi na utenguzi
Watu waliacha kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za majukumu yao wakawa wanapigana vikumbo kuuza sura kwenye runinga. Maranyingi wakifokea wasaidizi wao, wakitoa matamko hata ya kuwasimamisha kazi(huku kiuhalisia hawana uwezo huo) na pengine kuwananga na kuwafokea wananchi
Matokeo yake wananchi tumehaidaika na kuona mtumishi wa umma anayejitokeza hadharani kwenye vyombo habari ndio mchapa kazi.
Hata hivyo yawezekana mleta uzi kweli amemkumbuka katibu mkuu kiongozi. Nilikua najaribu kupanua mjadala tu
Mkuu pole kwa mafuaatakua ije ya ichi
Mkuu nimejaribu kukumbuka tu majibu ya wenye dhamana pindi wanapoulizwa maswali ya aina hiyo.Hata kuwepo kwenye kuapishwa viongozi ni sehemu ya kazi yake pia. Lazima Kuna tatizo si kawaida