Nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi sio ya kisiasa . KMK anaweza akawa anatekeleza majukumu yake kimyakimya bila kulazimika kujitokeza hadharani
Hapo nyuma uliingizwa usanii kwenye utumishi wa uma. Waziri alikua anafanya kazi za katibu mkuu, katibu mkuu anafanya kazi za mkurugenzi wa idara. Mkuu wa idara atafanya kazi za maofisa wa kawaida kama makarani au hata wahudumu ili mradi kila mtu alikua anakwenda mbio kupata publicity ya kuonekana anafanya kazi na hivyo ajipendekeze kwa mamlaka ya uteuzi na utenguzi
Watu waliacha kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za majukumu yao wakawa wanapigana vikumbo kuuza sura kwenye runinga. Maranyingi wakifokea wasaidizi wao, wakitoa matamko hata ya kuwasimamisha kazi(huku kiuhalisia hawana uwezo huo) na pengine kuwananga na kuwafokea wananchi
Matokeo yake wananchi tumehaidaika na kuona mtumishi wa umma anayejitokeza hadharani kwenye vyombo habari ndio mchapa kazi.
Hata hivyo yawezekana mleta uzi kweli amemkumbuka katibu mkuu kiongozi. Nilikua najaribu kupanua mjadala tu