TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Tatizo wabongo tu wabishi sana. Unakutana na mtu anakuambia Tanzania hamna Corona...
Alisema maji moto bhana...

Juzi kati hapa kitaa cha Bunju, mama mmoja kushuka kwa daladala na barakoa yake. Vijana wa bodaboda wanaanza kumzomea eti analeta udhuru, Tanzania hakuna Corona. Magu kaitokomeza... Hapo ni town vipi huko Mpitimbi?
 
Wengi wanaisikiliza serikali tu
Badala kuweka nguvu kwenye kuhamasishana tujijinge, tupo bize kupigia kelele wenye mamlaka...

Nadhani ingekuwa poa tungekuwa bize kuhamasishana kujikinga... Kuanzia kwa viongozi wa upinzani mpaka raia wa kawaida... Badala ya kila siku kuja na malalamiko kwa meko na wapambe wake, tungekuwa tunakuja na thread, post na tweet za namna bora ya kujikinga sisi kwa sisi...
 
Matusi ya nini ndg? Kitu gn kimeuma hapo? Kuna neno Corona umeitoa wp, mbona mm sikusema kuhusu Corona!
... ninyi hususan wewe si ndio mlikuwa mnabeza humu! Janga halibezwi ndugu; watu wanakufa halafu mnaleta maneno ya dharau humu? Eti kabla ya Corona watu walikuwa hawafi? Sasa imepiga penyewe; endeleeni na kebehi zenu!
 
ukweli ni kwamba tuliweka siasa na ujuaji kwenye vitu vinavyohitaji taaluma za watu, na baada ya hapo tukapata waziri wa afya mjinga akaacha kusimamia anachoona kinafaaa na kukiamini akaanza kujifanya mganga wa kienyeji, Pia watu wanaomzunguka na kumshauri rais wanamdanganya vitu vingi., Tanzania siyo wajanja kuzidi WHO tatzo ni ujuaji mwingi wa kipuuzi
 
Aonywae mara nyingi akishupaza shingo, huvunjika na wala hapati dawa...
... neno la uzima sana hili! Mungu ashukuriwe kwa neno hili la maonyo; ila mpumbavu atasikia maonyo? Na akisikia ataelewa? Maana yu katika kivuli cha upumbavu.
 
Hi mambo mingine sielewi bhana...

Kwani tunahitaji kutangaziwa ndo tujue ipo?!!
Wewe una uelewa huo. Trust me kuna mijinga mingi sana inawasikiliza wanasiasa kuliko madaktari na hata Mungu.

Juzi kati nimeshuhudia madogo wa boda wakimzodoa mama wa watu kashuka kwa daladala akiwa kavaa barakoa. Eti mama analeta uchuro bongo hakuna Corona, Magu kaifutilia mbali...

Trust me Magu akisema korona ipo tuchukue tahadhari, kesho maji tiririka kila mlango na kila mtu atavaa barakoa.

Kwakuwa tunajua kuna mjinga ya namna hiyo ndo maana tunamtaka kiongozi wa malaika mtarajiwa atangaze hilo ili hii vita tupigane kwa pamoja. Ni vigunu sana kuishinda hii vita peke yako.

Tujihadhari, hatuombei lockdown kama machizi mengi yamavyofikiria.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Korona inaondoka na mabosi tu
... maskani huku wanaondoka sio mchezo; hao mabosi unawasikia kwa sababu wana majina makubwa. Sasa hivi ni misiba kila kona ya nchi; sio mijini sio vijijini. Usiombe.
 
Wanyonge wanakufa kimyakimya na wala idadi yao haina umuhimu sana. Likiwakuta wao ndio utasikia kwamba wamefariki dunia na mlolongo wa salamu za rambirsmbi na matangazo kedekede. Kama tulivyokuwa tukisema na kubezwa, muda utatuambia "time will tell" na muda wenyewe ni huu. Masikio kama yalikuwa yameziba, sasa yanaanza kuzibuka. Na macho kama yalikuwa hayaoni sasa yanaanza kuona mwanga kwa mbali.
 
Sawa Acha WAFE.
... maskani huku wanaondoka sio mchezo; hao mabosi unawasikia kwa sababu wana majina makubwa. Sasa hivi ni misiba kila kona ya nchi; sio mijini sio vijijini. Usiombe.
 
Back
Top Bottom