TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Kujilinda ni jukumu la mtu binafsi. Ina maana huna sabuni? Huna uwezo wa kununua barakoa ya 500? Huwezi kuweka distance kati yako na mtu mwingine? Unataka Rais akushikie kiboko kufanya hayo? Embu tuwe serious kidogo jamani.
Kwani wewe serikali ikitangaza dharura utapungukiwa nini? We unajuaje kama alietoa wazo hajikingi? Mwisho wa yote we ndo serikali?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Kumekucha!!! Hatimae mdudu ametia timu kwenye ofisi ya Mh Rais rasmi!!!

Kocha Magu ajipange apangike kweli kweli, mpaka ikifikia mwezi wa 4 hivi, atakua ameshapoteza "BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI MPAKA SUB ZOTE" kutokana na ule ugonjwa wa kishetani aliosema haupo Tanzania.

Itakua yeye "ANAFANYA UTEUZI" na Sir God nae "ANAFUTA UTEUZI". Kasheshe, Tutaongea lugha moja mwaka huu walai!!!

Mtu unalala huku una mawazo kilo 7 kichwani, mawazo ya kesho sijui utaamshwa na taarifa gani. Ukisikia simu inaita asubuhi asubuhi "PRESHA INAPANDA" kabla hata ya kupokea (Usiombe ukawa na mgonjwa), roho ipo juu juu huna amani masaa yote unategemea taarifa ya vifo. Ukiingia JF unakuta thread tatu tatu za misiba hujui uanze kutoa pole thread ipi!!!
Hali ni mbaya kwa kweli.
 
Sichungi. Watanzania wanakufa kwa uzembe wa viongozi.tulishindwa nini kuchukua tahadhari tangu mapema? Nyie ccm mtabeba lawama za vifo vya watanzania.

Nakuonya kwa mara nyingine chunga sana kauli zako. Serikali Ina mkono mrefu.
 
Duuuuh bora vyuo na shule zifungwe tyuuh, aaaaah hii sasa ni hatari kwa kweli, na inaogopesha mno.
 
Instagram media - CLZ6T5Bh6jf ( 750 X 640 ).jpg
 
Mweh [emoji849] unatwanga maji kwenye kinu Kalaghabaho!! Yaani na mateso yote haya bado unawaza aongezewe tena mitano. Ulianza vizuri ila mwisho ni utopolo mtupu
Jifunze ku respect mawazo ya wenzako. Wewe sio binadama ambaye umekamilika peke yako. Kila mmoja ana desire yake na usifikiri kuwa wote tuna mawazo kama yako. Usichokipenda wewe haimaanishi kuwa na sisi pia hatukipendi.

Heshim mawazo ya wenzako na usipende kujaji kuwa ni utopolo. Wewe ni nani? Na nani kakipa mamlaka ya kujaji kuwa mawazonya wenzako ni utopolo?

Kama huna hoja ya kuchangia basi kaa kimya! Sidhani kama kuna mtu anahitaji your justification.
 
Back
Top Bottom