Anatapata tapa Bashiru aka kiongozi wa kutumia dola kubaki kwenye dollar sasa anatumia kwacha na fatanga haha [emoji1] [emoji38] [emoji23] [emoji1787] 8
Katibu wa hovyo kuliko wote ccm
Dk Bashiru Kakurwa hakuwa na makando kando ya kuiba wala kuhujumu mali za chama! Alirejesha mali zote za chama zilizokuwa zimeibiwa chamani na mmoja wa watu waliokuwa wameiba "kujimilikisha" mali za chama ni Nape.
Alirudisha mali zote za chama,ikiwemo maduka,majengo, radio station na TV station, viwanja vya wazi n.k chama kiliongeza mapato kuliko wakati wowote toka chama kianzishwe, alisimamia uchaguzi ndani ya chama kwa utaratibu wa kueleweka!
Alilipa madeni na mishahala ya watumishi wote wa chama ambao walikuwa wanadai malimbikizo yao,aliwapa makatibu wa chama wa wilaya nchi nzima vitendea kazi vya ofisi kikamilifu pamoja na kuwapatia magari ya kisasa ili wafanye kazi zao kwa weredi!
Ndio wakati tuliona makatibu wa wilaya na mikoa wakiandaa na kuitisha mikutano ya adhara kunadi sera za chama.
Ndie aliefanya chama kutotegemea wafanyabiashara na mafisadi bali chama kilijitosheleza na kujiendesha kwa rasilimali zake zenyewe.
Sasa sijui tafsiri yako ya kusema ni katibu wa hovyo inatoka wapi? Au wewe ni muanga uliekuwa umejimilikisha mali za chama!!
Kama sio tueleze ni katibu gani wa chama cha mapinduzi aliewahi kufanya kazi ya angalau ya viwango vya DK Bashiru Kakurwa?