Mama Samia aliishawambia kwamba hayo mambo ya mauaji na utekaji ni changamoto ambazo zipo Dunia nzima!
Ukienda America zipo, ufaransa zipo, Africa kusini zipo, Nigeria zipo na hata India , Saudi Arabia, Sudani na Uganda changamoto hizo zipo!
Kinachotakiwa na kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola ambavyo vimefunzwa na vina weledi wa kutosha na tusitake kuvishinikiza wala kuvifundisha namna ya kutekeleza majukumu yake.
Ila kama ndugu,rafiki au jirani yako ameuawa au ametekwa na unao ushahidi wa akina nani waluomuua au kumteka ipo nafasi ya kuvisaidia vyombo vya dola kwahiyo peleka ushahidi na taarifa zako katika mamlaka zinazohusika ukiwa kama raia mwema ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.