PreGE2025 Katibu Mkuu TEC, Rev Dkt. Charles Kitima: Wasitupangie cha Kusema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Duniani ni wapi? Ni nani anaye miliki watu wa Tanzania?
 
Mama Samia amefata nini hapo , nyie wahuni mnaajenda zenu binafsi mnataka kumchomekea Mama wa watu lengo ni kumchafua tu acheni uhuni una mwisho.
 
We mnafiki tu wale wale. Mkialikwa kwenye Ubwabwa wa Nchi si mnaenda kuwaombea? Sasa unasemaje hujiingizi? Hata hivyo ishajulikana uislam wa bongo una mashaka sana muulize Shekh Ponda
Ponda mimi namuona kama kichaa fulani hivi wala siamini kama ana elimu ya misingi ya uislamu .
Katika maneno yake sijawahi sikia akinukuu japo aya moja ya Quran wala hadithi ya mtume صلى الله عليه وسلم jambo linaloonyesha kuwa usheikh wake ni wa bandia kwakuwa hana elimu yoyote ya dini ya kiislamu.
Ponda ni mwanasiasa aliyejificha kwenye mwavuli wa dini ili kuuchafua uislamu.
 
Anachosema kiko kinyume na uislam? Au ndugu yangu wewe unaangalia tu ugali wako?
 
Mama Samia amefata nini hapo , nyie wahuni mnaajenda zenu binafsi mnataka kumchomekea Mama wa watu lengo ni kumchafua tu acheni uhuni una mwisho.
Mimi sina ugomvi na mama Samia.
Ninamuheshimu kwa 100% kama kiongozi wa nchi na kuwachukia wale wote wanaofanya uchochezi dhidi ya serikali yake kwakuwa matokeo ya uchochezi ni kuvuruga amani ya nchi yetu.
 
Anachosema kiko kinyume na uislam? Au ndugu yangu wewe unaangalia tu ugali wako?
Uislamu ni dini ya amani na haikubaliani na mambo ya uchochezi ambao ndio misimamo ya Isa Ponda tangu enzi za rais Kikwete.
Nabii Ibrahimu alipofika Makka alimuomba Allaah awape AMANI watu wa makka kabla hajawaombea chakula.
{ وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا بَلَدًا ءَامِنٗا وَٱرۡزُقۡ أَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُم بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ................... ... }
[Surah Al-Baqarah: 126]

Na ( kumbuka )
alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu ( mji wa Makka ) uwe mji wa AMANI , na uwaruzuku watu wake MATUNDA, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.............. .. "

Hapo unaona namna ambavyo Nabii Ibrahimu kaanza kuwaombea watu wa Makka AMANI kabla hajawaombea MATUNDA na hilo linamaamisha kuwa AMANI ni jambo la muhimu sana.
 
Mimi sina ugomvi na mama Samia.
Ninamuheshimu kwa 100% kama kiongozi wa nchi na kuwachukia wale wote wanaofanya uchochezi dhidi ya serikali yake kwakuwa matokeo ya uchochezi ni kuvuruga amani ya nchi yetu.
Mkuu unaamini kuna watu wmetekwa, kuuawa na wengine kupotea hadi leo kimyaa??

Mbona huzungumzii haki ambayo watanzania wote wanaidai?
 
Mkuu unaamini kuna watu wmetekwa, kuuawa na wengine kupotea hadi leo kimyaa??

Mbona huzungumzii haki ambayo watanzania wote wanaidai?
Mama Samia aliishawambia kwamba hayo mambo ya mauaji na utekaji ni changamoto ambazo zipo Dunia nzima!
Ukienda America zipo, ufaransa zipo, Africa kusini zipo, Nigeria zipo na hata India , Saudi Arabia, Sudani na Uganda changamoto hizo zipo!
Kinachotakiwa na kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola ambavyo vimefunzwa na vina weledi wa kutosha na tusitake kuvishinikiza wala kuvifundisha namna ya kutekeleza majukumu yake.
Ila kama ndugu,rafiki au jirani yako ameuawa au ametekwa na unao ushahidi wa akina nani waluomuua au kumteka ipo nafasi ya kuvisaidia vyombo vya dola kwahiyo peleka ushahidi na taarifa zako katika mamlaka zinazohusika ukiwa kama raia mwema ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
 
😃😃😃Basi mkuu ishia hapa hapa. Ushajulikana wewe ni nani.
 
Washughulikie madai yake ya msingi ammbayo ndio madai ya wananchi wote. Mbona mnaanza kufatilia mtu binafsi?
Kosa alishalifanya marehemu JPM ya kumuhangaikia mpaka akaingia kwenye uongozi wa juu wa TEC.

Anatuchonganisha sisi wakatoliki na watu wa madhehebu mengine kitu ambacho pia kinaichonganisha nchi na mataifa ya Ulaya. Huyu anatoka kijiji kimoja na TAL hivyo anaumia kuona CHADEMA inavyopata taabu katika muda huu.

Hakupenda bandari kuchukuliwa na DP World alichoshindwa kufahamu ni kwamba wafaidikaji wakubwa wa biashara za pale TPA ni wakatoliki wanaomheshimu yeye akiwa na hadhi ya mchunga kondoo.

Hata baadhi ya watendaji wa suala zima la bandari ni wakatoliki wenzake!, wanamstahi tu kwa sababu ukatoliki unafundisha siku zote kutunza heshima kati ya kiongozi na mlei wa kawaida.
 
Walutheri na waprotestanti kwa ujumla wanashangaa inakuwa vipi kanisa katoliki linakuwa na sauti ya kipekee kama vile wao hawapo na hawana umuhimu!.

Hakuna kanisa linalosikilizwa kama Katoliki, na hata marais wote wa kristo wanapiganiwa kwanza wajiweke sawa kwenye ukatoliki wao ili waweze kuongoza nchi vizuri ikiwa wao ni wakristo.

Marehemu Mkapa aliambiwa kwanza aweke sawa masuala yake ya ndoa ili aweze kuwa rais.

Marehemu JPM aliambiwa arudi kwenye ukatoliki na akae sawa na mke wake ili aongoze nchi vyema.

Ukatoliki unaheshimiwa na siasa zetu na umekuwepo uhusiano mwema wa muda mrefu kati ya kanisa na serikali kuu.

Lakini anavyofanya father Kitima muda huu ni kuiweka nchi kwenye wakati mgumu kwa ule ukweli kwamba anatumia mgongo wa ukatoliki ambao umekuwa na uhusiano mzuri na mfumo wa utawala tangu mwaka 1961.

Anawakwaza pia viongozi wakubwa kumzidi ndani ya uongozi wa kanisa kwa maana ya baraza la maaskofu. Kina Askofu Pengo wapo karibu sana na mfumo wa utawala hata maaskofu wengine wandamizi, pengine bila ya kujua akiwa amejawa na uanaharakati na kupenda kwake siasa.
 
Kuna kitu unakwepa kukisema.

Father Kitima anasema Haki za Kiuchaguzi na malalamiko ya Raia kupigwa na kuteswa wakati wa chaguzi ziangaliwe.

Mtu wa namna hii ana kosa gani?
Nyinyi mnataka mahusiano ya kina Pengo kama yale?

Hii itakuwa kanisa au takataka? Mtu anayepinga Madai ya Watanzania kuhusu haki na usalama wao huyo ndiye Mhaini namba moja
 
Umeongelea sehemu ndogo ya kikubwa anachokizungumzia. Hao CHADEMA waliitwa kwenye mkutano wa maadili na vyama vingine wakatanguliza ujeuri. Huko walipoalikwa haikuwa sehemu nzuri ya kuwakilisha vilio vyao kwa mapana na wakaweza kueleweka?.

Huyo wanamjua vizuri watu wa kitengo kuhusiana na mahaba yake ya kisiasa. Tatizo analivuta kanisa zima kana kwamba alishafanya kikao cha awali na wadau wanaosali katoliki halafu wakamwambia yote anayoyasema ndio msimamo wa kanisa zima.
 
Naona chawa unajitoa ufahamu
 
Hizo sheria ndogo za maadili ndio zitazuia wizi wa kura na kuzuia wagombea wa upinzani kutekwa na kuondolewa kuogombea pasipo sababu za msingi?
 
Ati Steven naye anatupangia vya kuema. Yani twende shule miaka yote wakati yeye anagema ULANZI halafu leo atupangie??
 
Hizo sheria ndogo za maadili ndio zitazuia wizi wa kura na kuzuia wagombea wa upinzani kutekwa na kuondolewa kuogombea pasipo sababu za msingi?
Una ushahidi gani utekaji kuwa haufanywi na maharamia wasio na uhusiano na serikali kuu?.

Tatizo mnapenda siasa za kihasimu zisizopenda makubaliano kufikiwa. Ujuaji unakuwa mwingi na mbeleni mnakutana na giza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…