PreGE2025 Katibu Mkuu TEC, Rev Dkt. Charles Kitima: Wasitupangie cha Kusema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa kanisa katoliki wanaojitahidi sana kuishi maisha ya dini bila siasa na ku.maintain integrity ni masista wa katoliki Hongera sana kwao.

Ila Mapadre katoliki wengi ni pasua kichwa huwezi linganisha na masista.
Masista wako serious sana na wito wao

Kama ingewezekana masista wapewe upadre na mapdre wavuliwe upadre warudi majumbani kwao na vijiweni
 
Sasa hapo kanisan utahubiri kondoo au nn,maana hao unawahubiria ndio wanaumizwa,wengine wamekufa,
Kuna elimu nyingine sio lazima ufundishwe,mnatupa wakati muhimu xna kuwaelimisha tuwaelimishe watoto wetu na ww pia nikuelimishe?😁😁😁😁
 
Unavuta bangi Wewe!!!
 
Wizi wa kura ni siasa? Utekaji na mauaji holela ni siasa? Ufisadi ni siasa? Kusema uwongo na kubatiza ile tume jina la Tume huru ni siasa?
Acha njaa na uchawa. Viongozi wa dini wana haki ya kukemea maovu yote katika jamii. Labda lile tawi la ccm liitwalo bakwata ndio hawawezi kukemea. Au yule kada wao Malasusa.
 
Sijui unapata wapi nguvu na muda wa kuandika takataka kama hii hapa, kutwa/kucha, na kila siku!

Sasa elewa tu kwamba hakuna litakalo wasalimisha safari hii. Mtazolewa tu na tsunami kama hamtaingiwa na akili vichwani kungali mapema.
Afadhali umenisaidia kujibu..kajamaa kutwa kuchwa kanajitutumua kuandika pumba.

Binafsi Mimi kwa Sasa watu wa aina yake nikuwatukana TU maana kama ni kuwa ELIMISHA SANA Ila hawaelewi
 
Huyu ni kampeni meneja wa Lissu katika uchaguzi wa 2020 ni mwanasiasa kamili nyuma ya pazia tofauti na baadhi ya maaskofu wanaoanza na kumaliza siasa zao juu ya mimbari siku za Jumapili.

Lazima awe na donge kwa kuzingatia ukweli kwamba DP World anafanya kazi pale bandarini tena kwa ufanisi uliotarajiwa tofauti na fitina aliyotusambazia makanisani kuupinga uwekezaji wake.
 
Hao wakenya na waganda ambao wanafananishwa na binadamu kwa akili zao wanaionea wivu Tanzania kwa kila kitu.

Ardhi nzuri yenye rutuba tumewazidi.

Ukubwa wa eneo lenye kufaa kuzalisha mali tumewazidi.

Siasa za kiungwana zisizo na chembe za ukabila na upuuzi wa kudharauliana, tumewaacha mbali.

Madini karibu kila kona ya nchi na kufunguka kwa kasi kwa nchi kwa ujumla, tumewaacha mbali.

Tatizo la mtanzania wa kawaida ni akili nyepesi ya kujiona yeye hafai kwa chochote lakini eti jirani yake ndiye anayefaa!, hizi ni akili za kitumwa zinazompa urahisi adui wa kuweza kututawala kadri anavyojisikia.
 

Amefanya vyema sana
 
Kutoa zaka na sadaka hakukufanyi kuwa mkatoliki kindaki ndaki bwana, wangapi wanatoa zaka na sadaka kubwa tu tena wahudhuruhaji wazuri jumuia, kila event za kanisa yet hawajiiti kindaki ndaki?

Kazi koja wapo ya kanisa la kristo ni kukumea mauvu kwenye jamii, Bwana wetu yesu kristu alifanya hivyo, mitume wake walifanya hivyo, na miaka kwa miaka, ww ni nani kushambulia established society kama catholic ?
 
Makanisani kuna ufisadi mkubwa tu. Kanisa linashindwa kumaliziwa kwa miaka mitano na zaidi na waumini kwa sababu ya kutoruhusiwa kuhoji wanasali wakiwa wamenuna.

Hizo kamati za ujenzi za makanisa zimejaa wezi wa kwenye mashirika ya umma na taasisi za kiserikali wanahamisha wizi ule ule kwenye nyumba za ibada.
 
huo ufisadi nani alichunguza? Unapoongelea kanisa ku dhehebu, kila dheheb lina waumini wake, na waumini ni uti wa mgongo wa kanisa husika

So far kwa experience yangu, hakuna taasis imenyooka kama catholic, ndio wenye miradi mingi kuliko hata taasis nyingine ya kidini, form shule, vyuo, hospitali. Kama wangekuwa na usimamizi mbovu sidhan kama wangekuwa hapo walipo

Kuna chombo chochote kilichowahi kuchunguza hizo tuhuma za ufisadi?
 
Vipindi vyote vya utawala wa wakatoliki wenzao hawajawahi kukemea lolote..
Wacha UONGO wewe chawa/kada wa sisiemu.

Magufuli ambaye alikuwa Mkristo mkatoliki alikosolewa sana hadi akajaribu kuwaonea kwa kuwavua uraia baadhi ya maaskofu, mfano Askofu Severin Niwemugizi, Askofu Kakobe, nk.

Askofu Gwajima akabambikiwa kesi ya uongo hadi akapelekwa kupimwa mkojo.

Askofu Mwingira akapigwa pini, nk.

Huyu Tundu Lissu ambaye pia ni mkatoliki alinusurika kuuawa kipindi cha utawala wa Magufuli, Mkatoliki mwenzake.

Mkileta udini kuweni wazi tu msitafute uhalali feki kwa kusingizia upande wa pili.

 
Nabii Nathani alimkemea Mfalme Daudi waziwazi, Samuel pia alimkea Mfalme Sauli, Yohane Mbatizaji alimkemea Herode. Hii ni sauti ya kinabii.

Maaskofu wanaendeleza kazi ileile ya kinabii kwasababu ndani mwao kunawaka moto wakinabii.

Ukweli unauma sana nikuuvumilia tu.
 
Mkuu fanyia kazi hoja wa Watumishi acha ubishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…