Katibu Mkuu wa CCM asikitishwa na wananchi Morogoro kutozwa Sh 7,000 bili ya maji yasiyotoka, aagiza TAKUKURU kuchunguza na kuwatia pingu wanaohusika

UTAPELI, Katibu Mkuu wa chama anatoa maagizo kwenye chombo cha serikali? Kwa mamlaka yapi? Katiba mpya ni muhimu kweli kweli
 
Serikali yote inatekeleza Ilani ya nnani?
kuna utaratibu wa kisheria wakati Serikali inapotekeleza Ilani, huyo jamaa yenu anatumia sheria ipi ama mamlaka yapi kutoa AGIZO kwa TAKUKURU kufanyia kazi maagizo yake? ingekuwa ombi kowa thats ok, ila anakwenda mbali na kuagiza watu wawekwe ndani - Je ana mamlaka hayo?
 
Kinana aliwahi zunguka nchi nzima na Kuja na madai kuwa Kuna mawaziri mizigo Saba yey na nape

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Viongozi wa vyama kutoa maoni kwa Serikali na kuwaomba wahusika wachunguze hatukatai, ila anayefika mbali na kutishia watu kuwaweka ndani hapo anabugi - kwa mamlaka yapi aliyonayo.
 
Morogoro Ina shida kubwa ya maji, kama suala la Mindu halitafanyiwa kazi haraka, sioni kama mbele Kuna mwanga.

Kwa kuwa Morogoro ni eneo ambalo mito ya maji inaanzia, nashauri tu NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais waanzishe hifadhi maalum za mito na ifanywe kama ilivyo Kanda maalum za kipolisi, inaangaliwa wakati wote, kama Kanda maalum, yenye bajeti maalum.

Nilitarajia apige Kambi pale bwawa la Mindu. Atoe maelekezo. Ashughulike na masuala mazito ya kisera katika Mkoa husika, aende na details za mipango ya chama na Serikali katika Mkoa, awe na data mkononi, na afike saiti kuona na kufanyia kazi.

Isiwe ziara ya kupiga maneno tu, maneno yawepo, na pia awe na mabuku yenye mambo ya maendeleo katika Mkoa husika na wapi yamefanikiwa, wapi yamekwama, na chama eneo husika wanasemaje, na Serikali inasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…