Katibu Mkuu wa CCM asikitishwa na wananchi Morogoro kutozwa Sh 7,000 bili ya maji yasiyotoka, aagiza TAKUKURU kuchunguza na kuwatia pingu wanaohusika

Katibu Mkuu wa CCM asikitishwa na wananchi Morogoro kutozwa Sh 7,000 bili ya maji yasiyotoka, aagiza TAKUKURU kuchunguza na kuwatia pingu wanaohusika

UTAPELI, Katibu Mkuu wa chama anatoa maagizo kwenye chombo cha serikali? Kwa mamlaka yapi? Katiba mpya ni muhimu kweli kweli
 
Serikali yote inatekeleza Ilani ya nnani?
kuna utaratibu wa kisheria wakati Serikali inapotekeleza Ilani, huyo jamaa yenu anatumia sheria ipi ama mamlaka yapi kutoa AGIZO kwa TAKUKURU kufanyia kazi maagizo yake? ingekuwa ombi kowa thats ok, ila anakwenda mbali na kuagiza watu wawekwe ndani - Je ana mamlaka hayo?
 
Kinana aliwahi zunguka nchi nzima na Kuja na madai kuwa Kuna mawaziri mizigo Saba yey na nape

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Viongozi wa vyama kutoa maoni kwa Serikali na kuwaomba wahusika wachunguze hatukatai, ila anayefika mbali na kutishia watu kuwaweka ndani hapo anabugi - kwa mamlaka yapi aliyonayo.
 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa bili na bei za maji kwa wananchi wilayani Malinyi mkoani Morogoro ili kupata ukweli iwapo wananchi hao wanabambikiwa bili au lah.

Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Mtimbila aliposimamishwa na wananchi akiwa katika msafara wake kuelekea Makao Makuu ya Wilaya ya Malinyi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM.

Mara baada ya kusimamishwa eneo hilo na wananchi walitoa kero yao kuwa bili ya maji ni sambamba na gharama za kununua maji ambapo pamoja na kwamba chanzo cha maji ni cha mserereko lakini bado wanatozwa shilingi 100 kwa ndoo ya lita 20.

Aidha,wamema bei ya maji wanayotozwa kwa mwezi kwa wale ambao hawajafungiwa mita za maji za ni shilingi 7,000 na bili hiyo inalipwa kila mwezi hata kama maji hayatoki.

Akijibu kero hiyo ambayo pia imetolewa na wananchi katika Wilaya ya Kilombero,Chongolo aliagiza Takukuru kufanya uchunguzi ili kuona uhalali wa bei hizo kwani mwongozo wa malipo ya maji ya chanzo hicho ni shilingi 20, kwa ndoo moja ya maji ya lita 20.

“Takukuru, hili lichukueni lichunguzeni kuona uhalali wake, maana nimepewa kero hii mara nyingi,sasa lifanyieni kazi,” amesema Chongolo.

Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu).
Morogoro Ina shida kubwa ya maji, kama suala la Mindu halitafanyiwa kazi haraka, sioni kama mbele Kuna mwanga.

Kwa kuwa Morogoro ni eneo ambalo mito ya maji inaanzia, nashauri tu NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais waanzishe hifadhi maalum za mito na ifanywe kama ilivyo Kanda maalum za kipolisi, inaangaliwa wakati wote, kama Kanda maalum, yenye bajeti maalum.

Nilitarajia apige Kambi pale bwawa la Mindu. Atoe maelekezo. Ashughulike na masuala mazito ya kisera katika Mkoa husika, aende na details za mipango ya chama na Serikali katika Mkoa, awe na data mkononi, na afike saiti kuona na kufanyia kazi.

Isiwe ziara ya kupiga maneno tu, maneno yawepo, na pia awe na mabuku yenye mambo ya maendeleo katika Mkoa husika na wapi yamefanikiwa, wapi yamekwama, na chama eneo husika wanasemaje, na Serikali inasemaje
 
Back
Top Bottom