Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Napenda kuwapeni taarifa ya kuwa kuanzia Kesho Katibu Mkuu wa CCM Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi ataanza na kufanya ziara nzito sana katika mikoa mitano ya kanda ya kaskazini,kati na Pwani. Ambapo mikoa hiyo ni mkoa wa singida ambao ndio utakuwa wa kwanza kwa siku ya kesho na baada ya hapo yeye na msafara wake mzima utaelekea kanda ya kaskazini kwenye mikoa ya Manyara,Arusha , Kilimanjaro na kumalizia kwa kishindo kikuu katika Mkoa wa Tanga.
Ziara hiyo nzito itajumuisha pia uwepo wa katibu wa itikadi ,uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amossi makala. Ni katika ziara hiyo ambapo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu katika staili ya kipekee kabisa.
Ziara hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na maelfu ya watu wa kanda ya kaskazini ,imeonyesha kuteka hisia za watu wengi sana mitandaoni na maeneo mbalimbali,hasa ikizingatiwa ya kuwa pamoja na mambo mengine itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi na secretarieti nzima kufanya ziara ukanda huo wa kaskazini.
Ziara hiyo imevuta hisia za wengi hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa ni kanda ya kipekee kabisa kisiasa na ambayo kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni kama ni Ngome kuu ya upinzani hususani kwa chama kikuu cha upinzani hapa Nchini yaani CHADEMA ambacho kwa sasa kimepoteza ushawishi kiliokuwa nao kwa Wananchi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.