Katibu Mkuu Wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi kufanya ziara Mikoa ya kanda ya Kaskazini 29/05/2024

Katibu Mkuu Wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi kufanya ziara Mikoa ya kanda ya Kaskazini 29/05/2024

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda kuwapeni taarifa ya kuwa kuanzia Kesho Katibu Mkuu wa CCM Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi ataanza na kufanya ziara nzito sana katika mikoa mitano ya kanda ya kaskazini,kati na Pwani. Ambapo mikoa hiyo ni mkoa wa singida ambao ndio utakuwa wa kwanza kwa siku ya kesho na baada ya hapo yeye na msafara wake mzima utaelekea kanda ya kaskazini kwenye mikoa ya Manyara,Arusha , Kilimanjaro na kumalizia kwa kishindo kikuu katika Mkoa wa Tanga.

Ziara hiyo nzito itajumuisha pia uwepo wa katibu wa itikadi ,uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amossi makala. Ni katika ziara hiyo ambapo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu katika staili ya kipekee kabisa.

Ziara hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na maelfu ya watu wa kanda ya kaskazini ,imeonyesha kuteka hisia za watu wengi sana mitandaoni na maeneo mbalimbali,hasa ikizingatiwa ya kuwa pamoja na mambo mengine itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi na secretarieti nzima kufanya ziara ukanda huo wa kaskazini.

Ziara hiyo imevuta hisia za wengi hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa ni kanda ya kipekee kabisa kisiasa na ambayo kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni kama ni Ngome kuu ya upinzani hususani kwa chama kikuu cha upinzani hapa Nchini yaani CHADEMA ambacho kwa sasa kimepoteza ushawishi kiliokuwa nao kwa Wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
FISIEMU MAMBO YAO.... 🤒🤒🤒
Screenshot_20240528-214211.png
 
wazee wamezidiwa kete na vijana wawili, bashite na jerry. imagine ccm yote wangekuwa kama hawa wawili, mbona pangechimbika.
 
Ulaji kwa Chawa nyakati hizi za kampeni 😂😂
Embu niambie wewe unalipwa shilingi ngapi kuandika na kushinda humu jukwaani? Maana inaonyesha unalipwa na ndio maana pengine unafikiri kila mtu analipwa kama unavyolipwa wewe.
 
wazee wamezidiwa kete na vijana wawili, bashite na jerry. imagine ccm yote wangekuwa kama hawa wawili, mbona pangechimbika.
CCM Ni Chama cha mikakati na mipango na chenye kujuwa namna ya kukaa midomoni na vinywani mwao watu. Si unaona hata habari za CHADEMA na chaguzi zao wala hazijulikani na mtu wala kufuatiliwa na watu wala kujulikana nini kinaendelea huko.

Watu wapo Bize na CCM tu.ukigeuka huku unakutana na habari za Mwamba Makonda,ukiangalia kule unaona CHUMA David Kafulila yupo kwenye Tv akishusha NONDO za hatari zinazowachanganya wapinzani, watu hawajakaa sawa wanashangaa Ziara nzito chini ya unahodha wa Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi.

Yaani ni kazi juu ya kazi.
 
Katibu na mwenezi wake hawana mvuto.
Hawafanyi biashara wala maonyesho ya sura bali wanakagua utekelezaji wa ilani ya CCM,kusikiliza kero na kuzitatua kwa kuzipatia majibu.pamoja na kueleza nini serikali imefanya na inatarajia kufanya nini.
 
Kwahiyo wewe hulipwi na Tumbiri? 😂
Nikajuwaga ukiwa mzee unakuwa na akili kumbe hata ujinga nao huzeeka na kukomaa .kwa hiyo kijana mjinga hata akiwa mzee atakuwa ni mjinga hata kama ana mvi😃😃😃.

Wewe si ulisema ninalipwa na dkt Tulia? Si ni wewe ulisema nina lipwa na mheshimiwa Makonda? Si ni wewe ulisema nina lipwa kumpamba Rais Samia? Na sasa unasema nalipwa na Mhessimiwa CHUMA Mwenyewe Kafulila? Inakuwaje mimi nalipwa na watu wote hao? Kwanini na wewe usilipwe? Au wewe huna akili ndio maana hulipwi? Basi na wewe andika ili ulipwe kama yapo malipo.
 
Naona kama anaenda kutuliza upepo baada ya Bashite kuchafua hali ya hewa!
 
Nikajuwaga ukiwa mzee unakuwa na akili kumbe hata ujinga nao huzeeka na kukomaa .kwa hiyo kijana mjinga hata akiwa mzee atakuwa ni mjinga hata kama ana mvi😃😃😃.

Wewe si ulisema ninalipwa na dkt Tulia? Si ni wewe ulisema nina lipwa na mheshimiwa Makonda? Si ni wewe ulisema nina lipwa kumpamba Rais Samia? Na sasa unasema nalipwa na Mhessimiwa CHUMA Mwenyewe Kafulila? Inakuwaje mimi nalipwa na watu wote hao? Kwanini na wewe usilipwe? Au wewe huna akili ndio maana hulipwi? Basi na wewe andika ili ulipwe kama yapo malipo.
Unaweza kuweka ushahidi niliposema unalipwa na hao uliowataja?

Nimekuuliza swali wewe hulipwi na Tumbiri?

Mbona umepanic? 😂😂

Kwanini uliacha ghafla kuweka namba Yako ya mkeka hapa JF? 😂😂😂😂😄
 
Unaweza kuweka ushahidi niliposema unalipwa na hao uliowataja?

Nimekuuliza swali wewe hulipwi na Tumbiri?

Mbona umepanic? 😂😂

Kwanini uliacha ghafla kuweka namba Yako ya mkeka hapa JF? 😂😂😂😂😄
Nimekujibu kulingana na akili yako ilivyo kwa kukurejesha nyuma iliyotamkwa Mwenyewe,kwa hiyo kama kichwa chako kinapoteza kumbukumbu kwa mambo ya nyuma .hilo ni juu yako.
 
Back
Top Bottom