Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo yupo mjini Ifakara. Nashangaa kuona ulinzi ni mkali

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo yupo mjini Ifakara. Nashangaa kuona ulinzi ni mkali

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Polisi ni wengi, kila kwenye junction ya kuingia barabara kuu ya Morogoro kuna polisi amesimama.

Vijana wa bodaboda wengi wameondoka kwenye vituo vyao kwa hofu ya kukamatwa.

Kifupi nimeshangaa Katibu Mkuu wa CCM kupewa ulinzi na mapokezi kama kiongozi wa serekali.

Tufike mahali viongozi wa juu wa CCM waache kujiona kama viongozi wa Serikali
 
CCM wakienda uchochoroni kama huko Ifakara wanainua mabega? Chongolo huyu akiwa mjini huwa anatembea kama muuza kuku tu.
Unamkuta ubungo pale kwenye appartment zake . Kavaa kibukta kakaa nje ya geti, anaangalia mafundi. Gari kubwa ila haendeshwi na halindwi. Kuna vituko sana bongo.
 
Polisi ni wengi, kila kwenye junction ya kuingia barabara kuu ya Morogoro kuna polisi amesimama.
Vijana wa bodaboda wengi wameondoka kwenye vituo vyao kwa hofu ya kukamatwa. Kifupi nimeshangaa katibu mkuu wa ccm kupewa ulinzi na mapokezi kama kiongozi wa serekali. Tufike mahali viongozi wa juu wa ccm waache kujiona kama viongozi wa serekali

Hii tabia ilishika sana kasi wakati wa Magufuli, eti hata mpaka msemaji wa CCM akipita na msafara wake magari yanasimamishwa ili kupisha msafara wake! Mchezo huo naona unaendelea hadi sasa.
 
Iko ni Chama tawala sio mbaya mtendaji mkuu wa Chama (katibu mkuu)kulindwa pia kwaiyo lazima awe na escort za nyoka(usalama)
 
Back
Top Bottom