Katibu Tawala Mara asema Mikopo ya serikali sio zawadi rejesheni kwa wakati. Tusisahau mikopo waliopewa wasanii nao warejeshe harakaa

Katibu Tawala Mara asema Mikopo ya serikali sio zawadi rejesheni kwa wakati. Tusisahau mikopo waliopewa wasanii nao warejeshe harakaa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakuu

Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia mikopo inayotolewa na Serikali kwa manufaa na kuirejesha kwa wakati ili iweze kuwanufaisha wengine wenye uhitaji.

Akizungumza wakati alipokutana na timu ya wataalamu ya elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha ambayo imewasili mkoani hapo kwa ajili ya kutoa elimu katika baadhi ya vijiji vya wilaya za mkoa huo, amewataka wananchi kutambua kuwa mikopo inayotolewa na Serikali haitolewi kwa maana ya zawadi bali inatolewa kwa kusudi la kumwinua mwananchi kwa suala la kipato na inatakiwa irudishwe ili wengine waweze kunufaika pia.

Aidha, Kusaya ameeleza kushangazwa na tabia za wananchi kukopa kwenye taasisi za “mikononi” ambazo hazina ofisi, ambazo ni dhahiri kuwa ufuatiliaji wa marejesho hauwezi kuwa na ustaarabu.

Amesema taasisi ya ukopeshaji ni lazima iwe na ofisi, anuani na usajili na hivyo kuwataka wananchi kuchukua mikopo kwenye taasisi rasmi ili kuepukana na adha mbalimbali ikiwemo riba kubwa na kudaiwa bila ustaarabu.
1741774615034.png
 
Back
Top Bottom