benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Taarifa za awali kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Tixon Nzunda pamoja na dereva wake wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea eneo la Mjohoroni mkoani humo.
Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa juu ya ajali hiyo.
Picha kutoka eneo ilipotokea ajali
======
Dkt. Tixon Tuyangine Nzunda alikuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, nafasi aliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu na kuapishwa 19 Machi, 2023.
Nzunda alizaliwa January 29, 1968 na ameacha mke na watoto wanne. Aliajiriwa na Serikali mwaka 1992 kama afisa msaidizi wa elimu daraja la tatu na tangu hapo ameshika nafasi kadhaa ikiwemo katibu mkuu msaidizi utumishi, katibu tawala mkoa wa Rukwa na naibu katibu mkuu Serikali za mitaa.
Picha kutoka Maktaba.