TANZIA Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari

TANZIA Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari

Taarifa za awali kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Tixon Nzunda pamoja na dereva wake wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea eneo la Mjohoroni mkoani humo.

Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa juu ya ajali hiyo.

View attachment 3020136View attachment 3020137
Picha kutoka eneo ilipotokea ajali

======

Dkt. Tixon Tuyangine Nzunda alikuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, nafasi aliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu na kuapishwa 19 Machi, 2023.

Nzunda alizaliwa January 29, 1968 na ameacha mke na watoto wanne. Aliajiriwa na Serikali mwaka 1992 kama afisa msaidizi wa elimu daraja la tatu na tangu hapo ameshika nafasi kadhaa ikiwemo katibu mkuu msaidizi utumishi, katibu tawala mkoa wa Rukwa na naibu katibu mkuu Serikali za mitaa.

Picha kutoka Maktaba.

Mijooloni kuna damu zimemwagika sana watu wa maombi wapite hapo kupaweka sawa,damu zilizomwagika zinadai nyingine zaidi
 
Kwahio unataka kufananisha safety features za usafiri wa mkonge 1HZ uliobuniwa 1976 dhidi ya gari yenye teknolojia ya 2024 kiusalama?

Kwa mbung'a iliyotokea ingekua ni cruiser mkonge hata paa la gari lisingeonekana 😂. Hio gari ni imara hakika na eneo ambalo viongozi wanatakiwa kukaa ni siti za nyuma tatizo wabongo wanapenda kuvunja vishoka. Angekaa siti ya nyuma with seatbelt fastened ni hakika angetoka salama tu.
Kwa hiyo mkuu unashauri hayo magari LC 300 series yaendelee kuagizwa kwa watu kama Katibu Tawala, Meya, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakurugenzi wa mashirika, RPC, OCD nk ...

Huoni kwa vyeo vyao wanahitaji gari za kawaida ? Na speed yote ya nini ?
Tena sehemu yenyewe ni karibu na KIA hakuna kona wala nini (open space)

Hauoni hizo gari ni gharama sana kulingana na uchumi wa nchi ?

Nina uhakika kuna gari za bei nafuu na nzuri kutoka Japan ( Land cruiser) na comfortable kuliko kushindana kununua latest car ambayo ukila mzinga m 450 imepotea
 
Gari za bei nafuu ni zipi? Kwa serikali ya kifisadi kama hii tuliyonayo hamna mtu atataka aendeshe gari inferior sababu pesa za kununulia zipo.

Imekuwa kama norm toka kwa serikali ya awamu ya nne kununua latest Japanese vehicles especially hizo Utalitarian kama LandCruisers kwa viongozi na waandamizi wao. Awamu zilizofuata zote wameiga tu.

Jakaya aliingiza 100 series. Magufuli akaingiza 200 series. Sahizi samia ameingiza 300 series Landcruisers alongside Prado counterparts kama J120 na J150 series na soon mtashuhudia uingizwaji wa Prado box new model za mwaka huu 2024 zinazotambulika kama J250.
 
Kwa hiyo mkuu unashauri hayo magari LC 300 series yaendelee kuagizwa kwa watu kama Katibu Tawala, Meya, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakurugenzi wa mashirika, RPC, OCD nk ...

Huoni kwa vyeo vyao wanahitaji gari za kawaida ? Na speed yote ya nini ?
Tena sehemu yenyewe ni karibu na KIA hakuna kona wala nini (open space)

Hauoni hizo gari ni gharama sana kulingana na uchumi wa nchi ?

Nina uhakika kuna gari za bei nafuu na nzuri kutoka Japan ( Land cruiser) na comfortable kuliko kushindana kununua latest car ambayo ukila mzinga m 450 imepotea
Yaagizwe tuu pesa ipo
 
Gari lililopata ajali ni la RC Kilimanjaro,ila lilikuwa limembeba RAS Kilimanjaro.

Kwanini RC Kilimanjaro hakuwa kwenye gari lake?

Maswalinni mengi kuliko majibu!
RC hakuwa vizuri kiafya ndio akamwagiza RAS amuwakilishe
 
Back
Top Bottom