Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa kiwanda hicho, kwani inasaidia kusafirisha malighafi kutoka mgodini yanakochimbwa makaa ya mawe hadi kiwandani ambako nishati safi ya makaa inatengenezwa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Seneda amesema, "Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa takribani shilingi bilioni 5.72 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, hususan katika maeneo korofi ambapo daraja kubwa limejengwa ili kuhakikisha barabara inapitika muda wote."
Awali, katika kipindi cha mvua, barabara hiyo ilikuwa haipitiki, hali iliyokuwa ikisimamisha uzalishaji kiwandani. Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa mradi huo, uzalishaji umeboreshwa na unafanyika bila kusimama kwa msimu, jambo ambalo limeongeza tija na ufanisi na kukuza uchumi wa Mkoa wa Songwe.