Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Katibu Tawala Msaidizi wa zamani wa Mkoa wa Kilimanjaro, Renatus Msangira (45), amepanda kizimbani akidai kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani humo, Lengai Ole Sabaya, hakupewa kibali chochote cha maandishi kwenda kutekeleza majukumu nje ya kituo chake cha kazi.
Msangira, ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri, ametoa madai hayo leo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakati akitoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Filex Kwetukia.
Kwenye hii Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, Upande wa Serikali unatarajia kuwa na mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hii ni Enock Mnken, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Awali Wakili kwetukia aliwasomea maelezo ya awali ambapo alidai Januari 22,2021 Sabaya aliongoza genge la watuhumiwa wenzake sita na kwenda gereji inayomilikiwa na Francis Mrosso iliyopo eneo la Mbauda ambapo walikutana na mmiliki wa gereji hiyo na kumtuhumu anakwepa kodi, huku akifanya biashara hiyo ya gereji bila kutoa risiti za TRA.
Amedai kuwa Sabaya alimtisha Mrosso kuwa asipofanya kitu atampatia kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Wakili huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa Sabaya alimtaka Fransis Mroso kutoa shilingi Milioni 90 ili awe huru ambapo kutokana na vitisho Mrosso alikubali kutoa fedha hizo.
Alidai kuwa mhanga huyo alitoa kiasi hicho cha fedha ambapo walienda benki ya CRDB tawi la kwa Morombo akiwa katika usimamizi wa washtakiwa wenzake Sabaya na kuwa kwa wakati huo Sabaya alikuwa nje ya benki hiyo akiwasubiri na baada ya kutoa fedha hizo walienda eneo la Sombetini ambapo Sabaya alikabidhiwa fedha hizo.
Pia soma;
Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi