Katibu Tawala: Sabaya, hakupewa kibali chochote cha Maandishi kwenda kutekeleza majukumu nje ya kituo chake cha kazi

Katibu Tawala: Sabaya, hakupewa kibali chochote cha Maandishi kwenda kutekeleza majukumu nje ya kituo chake cha kazi

1. Suala hili la Lengai ole Sabaya siyo jambo la kushabikia hata kidogo. Hili ni jambo ambalo lina akisi namna ambavyo mfumo wetu wa utawala ulivyokuwa umeoza.

2. Pamoja na kuwashiria uozo huo watu wengi tuliushangilia tukiaminishwa kuwa tulikuwa tunajenga miundombinu ya "kufa mtu" na kusahau utu wa binadamu.

3. Tabia ya viongozi kama akina Ole Sabaya ilianza kuota mizizi miongoni mwa watendaji wa serikali hasa wateule mbali mbali. Wengi waliongoza kwa kutoa maagizo ambayo hayana tija kwa taifa na bila kufuata utaratibu. Ifahamike kuwa utumishi wa umma unayo miiko yake ambayo lazima isimamiwe na kuheshimiwa na kila Mtanzania.

4. Kwa kazi kubwa iliyoko mbele yetu na kazi kubwa inayomkabili Mh. Rais wa JMT SSH ni kurudisha miiko ya uongozi na ile utumishi wa umma kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu.

5. Bahati nzuri katika kipindi hiki cha awamu ya sita maagizo ya hovyo hovyo kutoka kwa watendaji wa serikali imepungua. Ahsante mama yetu kwa hili. Kila mtanzania mwenye akili timamu anaelewa kuwa "una kazi kubwa ya kurudisha misingi ya utumishi wa umma na miiko ya uongozi". Jambo ambalo nililo jifunza kipindi hiki cha mienzi sita ya awamu ya 6 mama unasikiliza na mumiini wa kufuata taratibu.

6. Hata jitihada za msajili wa vyama vya siasa kukutana na wadau kama jeshi la polisi na vyama vya siasa ni njia bora moja wapo wa kujaribu kujenga uhalali wa kurudisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ili kuondoa " tension" na "chuki" iliyopo baina ya vyama vya siasa na jeshi polisi. Kumbuka kubomoa nyumba ni rahisi lakini kuijenga nyumba hiyo ni sawa na kupanda mlima Kilimanjaro.

7. Watumishi wote wa umma wenye vinasaba vya Ole Sabaya waondolewe kama bado wako serikalini ili kujenga heshima ya uongozi na kuliponya taifa.

8. Taifa na maendeleo ni zaidi ya ujenzi wa miundombinu. Amani ya moyo kwa kila mtanzania ni faraja kubwa na ni sehemu ya maendeleo.

9. Kumbuka nafasi za kiutawala ndani ya serikali zitapita lakini Tanzania itabaki milele kama ilivyo kwa milima.

10. Mungu wape macho ya moyoni viongozi wetu ili waweze kuona tena kama alivyoona Mwalimu Nyerere. Nyerere aliona mbali sana ndiyo maana leo tumeendelea kusimama imara kama taifa.

11. Tusiwe na wakumlaumu kwa kuwa nyufa zipo kwenye nyumba yetu tujitahidi kuziba nyufa na kuijenga nyumba yetu upya. Tulipo poka haki za watu tuwarudishie haki zao. Tulipo kuwa na mateka kwa ajili ya kupaza sauti zao tuawaachie. Hili litasaidia kuturudisha kwenye misingi ya utu na utanzania wetu.

12. Uchumi haujengwi kwenye misingi ya manunguniko na "migomo baridi". Awamu ya 6 tunapumua japo siyo haba tunahitaji kupumua zaidi. Wakina Ole Sabaya wengi wakiwajibishwa tutapua zaidi. Na hii ni njia moja wapo yakurejea kwenye miiko ya uongozi.
 
Najiuliza Baadhi ya Maswali
Je SABAYA alikuwa anashirikiana na Nani kuwafungulia Watu Mashtaka ya MAKOSA Anayoyataka Yeye?
Sabaya alishasema kuwa alitumwa na Prof. Luoga, dk Mpango na baba lao Magufuli
 
Huyo Katibu tawala ushahidi wake ulipaswa kuishia kwenye ruhusa za Sabaya, sasa huko kote anakoelezea alikuwepo? Isije ikawa wameanza kuvuruga kesi
 
Waangaliepesa alizonazo banki au alizotoa toka akamatwe.wafunge akaunti zone katika banking zone zinazohusiana nasabaya na familia yake. Itasaidi kuonyesha kama kuna pesa chafu.hata kwa simu zake zote. Itasaidia kuona pesa zolipo .
 
Renatus Msangira (45), amepanda kizimbani akidai kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani humo, Lengai Ole Sabaya, hakupewa kibali chochote cha maandishi kwenda kutekeleza majukumu nje ya kituo chake cha kazi.
hii ndiyo huwa inaitwaga - kupigilia msumali wa mwisho kwenye geneza!!
 
Mitego ya Rais Samia ya Royal Tour yanasa TZS 158.4bl | Hoteli nne kubwa za kitali hadhi ya Kempinski kujengwa Serengeti, Ngorongoro,Manyara & Tarangire,

Wawekezaji toka Bulgaria matokeo ya Royal Tour kuwekeza US$ 72M karibu sawa na Tsha 158.4BL kwa kujenga Hotel nne kubwa za nyota tano ( Five Stars Hotel ) katika mbunga za Serengeti, Ngorongoro, Manyara & Tarangire.

Utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi kifupi cha miezi sita umeonesha matokea makubwa katika kila kona ya nchi, madhalani uwekezaji tayari umekua kwa 400% toka uwekezaji wa US$ 510M hadi US$ 2.98BL sawa na Tshs 7trilioni pesa ambayo itamfikila kila Mtanzania popote alipo katika njia moja au nyingine.

#Mliokuwa mnalalamikia gharama ya Royal Tour mnasemaje kuhusu hizi bilioni 158.4 za fasta?

Kazi iendelee

C&P
 
Hili dawa ilikuwa apelekwe uwanja wa wazi apigwe kwa mawe hadi afe kwa mateso makali sana.
 
Watajuana. Sabaya ni Mbuzi wa kafara. Inabidi Phillip Mpango , mkuu wa kikosi kazi za mapato aje kutoa ushahidi wake muda ukiwadia

Sio kweli ni mbuzi wa kafara. Analipia kukosa unyenyekevu na kuelewa madaraka na dhamana ya madaraka huwa ni vitu vya kupita
 
Sabaya hachomoki kwenye hii kesi, labda utokee muujiza mwingine wa jaji kuwafundisha mawakili wa CCM nini cha kufanya.
Kabisa Mkuu, Mawakili wa Serikali wamejigeuza kuwa MAWAKILI WA CCM. Inasikitisha sana tulikofikia kama Taifa.
 
Back
Top Bottom