PreGE2025 Katibu wa BAVICHA Mtaa wa Msasani, Tunduma 'No Reforms No Election' ina mpango wa kuipendelea team Lissu

PreGE2025 Katibu wa BAVICHA Mtaa wa Msasani, Tunduma 'No Reforms No Election' ina mpango wa kuipendelea team Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hoja zake zijibiwe tusisingizie kuwa atu katumwa.
Aseme ni wapi fomu zimeanza kutolewa, ni Tume huru ya Uchaguzi au ni CHADEMA?? Hapo atajibiwa hoja zake zinazofuata
 
Uchaguzi utafanyika na washindi kitangazwa. Leo eti Chadema izuie uchaguzi hiyo ni ndoto ya mchana. Bora mkashiriki kuna watu wengi tu watawapa kura kuliko hiki kituko mnachojaribu kukileta. Kama hamjanipanga kupiga kampeni sababu ya ukata bora mseme kuliko hiki kituko.
Mtu malafi wa madaraka pekee ndiyo atashiriki uchaguzi wa mwaka huu bila kubadilisha sheria.Mko madarakani tayari mnaweza mkabaki madarakani bila kuharibu pesa(kodi)zetu,unafanya uchaguzi afu kura za raia haziheshimiwi si ujinga huwo sitaki kuamini kama tz kunaongozwa na wajinga kiasi hichi mnashindwa kuelewa ishu ndogo tu kama hii.
 
Hoja zake zijibiwe tusisingizie kuwa atu katumwa.

1. No Reform No Election ni azimio lililopotishwa wakati Mbowe akiwa Mwenyekiti.

2. No Reform No Election lengo lake ni kutoa nafasi sawa kwa kila Mtanganyika na Mzanzibari kushiriki uchaguzi.

3. Reforms zikifanyika wagombea hawatakuwa watumwa wa vyama kwani watakuwa na fursa na haki sawa ktk chama chochote, au kama wagombea binafsi.
 
Yaaani Lissu aliyekuwa mzima asiye na ulemavu akapata ulemavu kabisa kutokana na kututetea watanzania leo hii ndo useme anatafuta faida zake?

Kweli CCM ni wajinga. Na hizi propaganda za kijinga mnazozidi kuzifanya ndo zinazihirisha hamstahili kabisa kuliongoza hili Taifa.
 
Huyo katibu Ana hoja wala sio siri

Lisu kigeugeu amejipanga na timu yake kuenda nchi nzima kutangaza no reform no election kupumbaza timu mbowe wakati timu yake inajiandaa kwa uchaguzi halafu ghafla atabadili gia hewani

Akisubiri kubadili gia hewani uchaguzi ukikaribia kuwapa nafasi timu yake kugombea kwa kisingizio kuwa Tume ya uchaguzi ikileta za kuleta kuchakachua matokeo Chadema iko tayari kumwaga damu wakati anaipa timu yake kugombea

Mliojipanga kugombea Chadema ubunge na udiwani timu Mbowe endeleeni na harakati zenu bila woga wala hofu

Mkidharau hiki nimeandika mtakuja kuniamkia shikamoo hata kama mumenizidi umri

Lisu tapeli mark my words
 
Katoa mawazo yake ila ataishia kuitwa majina ya hovyo na watu wa hovyo wanaojihisi wao ni wakamilifu na mawazo yao tu ndio sahihi!
Tatizo hayuko makini na nini kinaendelea ndani ya chama chake au anafahamu lakini anataka kuwachanganya tu watu. Yeye kama kijana na kiongozi wa chama alipaswa awe navdetails zote nakinachoendelea kwenye chama chake, ila jinsi anavyo ongea hafai hata kuwa kiongozi.
 
Na wewe ni mjinga kama uyo???
Sijui kati ya wewe,mimi na huyo aliyetoa maoni yake nani ni mjinga! Kaongea kitu kizuri tu kwamba inaonekana chama hakiongei lugha moja,wakati wengine wanasema bila marekebisho hawatashiriki uchaguzi,wengine wanachukua fomu hata kabla ya marekebisho yanayoshinikizwa.kijana anaona kama kuna mpasuko,anahimiza umoja wa dhati! Sasa kama wewe huioni mantiki yake,huwezi mjibu chochote cha maana zaidi ya kumuita majina ya ajabu kujifurahisha nafsi!
 
Elisha Asa Mwambene, Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mtaa wa Msasani, Tunduma, Mkoa wa Songwe, ameibua mjadala mzito kuhusu kampeni ya “No Reforms No Election” inayoendeshwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Lissu.

Kupitia mahojiano na wanahabari, Elisha amesema vijana wengi Tunduma wameshindwa kuelewa lengo hasa la kampeni hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho tayari wameshatangaza nia ya kugombea nafasi za ubunge katika uchaguzi ujao.

Kwa mujibu wa Elisha, kampeni ya Lissu inaonekana kuwa na ajenda ya siri ya kuingiza “Team Lissu” bungeni huku ikilenga kuiweka pembeni “Team Mbowe”, jambo ambalo linaweza kuligawa na kulidhoofisha chama.

Ameeleza kuwa badala ya kuhamasisha umoja, kampeni hiyo inazua migawanyiko isiyo ya lazima ndani ya CHADEMA.

Akiwasihi wanachama wa CHADEMA katika Tunduma, Elisha amewataka kupuuza siasa za upendeleo na kuzingatia maslahi ya chama kwa ujumla. Amesisitiza kuwa siasa safi ni zile zinazojenga mshikamano, sio zinazotengeneza makundi na misuguano isiyo na tija.

View attachment 3286829
Lissu,Heche na Lema ni sikio la kufa.Hawana maarifa ya sayansi ya siasa
 
Back
Top Bottom