peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
- Thread starter
- #21
Katibu mkuu wa CCM Taifa fika Jimbo la Hai huko Kilimanjaro ukakutane na kituko cha mwaka 2022.
Siku ya Mwisho ya wajumbe walioomba kugombea nafasi za ccm kata ilikuwa Tare 20.6.2022 saa 10.
Cha kushangaza baada ya Jana, Leo tarehe 21.6.2022 katibu wa ccm wilaya ya Hai Mr Ballo , amechukua / amekusanya fomu zote Za wagombea walizojaza nakala tatu Tatu Kila mgombea kwa kata 17 na nafasi za wenyeviti, makatibu, wenezi na wajumbe wa kata na wilaya na kuzipeleka Ofisi ya CCM wilaya kabla fomu Za wagombea hazijapita kujadiliwa na vikao vya chama ngazi ya Kata ambavyo ni sekretariet ya chama ngazu ya kata na kamati Za siasa Za Kata Ili wagombea watakao jadiliwa na kupitishwa kwa mujibu wa katiba ya ccm majina yaweze kwenda Ofisi ya ccm wilaya Kuendelea kujadiliwa na vikao vya wilaya.
Sasa Kwa Hali ilivyo kama Katibu Mkuu wa CCM Taifa hataingilia kati kuna kila dalili uchaguzi wa ndani wa ccm jimbo la Hai kuvurugwa na upinzani kwani Makatibu wa ccm kata zote wameweka mgomo kutokupokea fomu Za wagombea kutoka wilayani kabla hazijajadiliwa na secretariat ya kata na kamati Za siasa Za Kata.
Makatibu wa ccm kaya 17 wana maswali wanajiuliza hawana majibu hadi sasa na si rahisi wapate majibu bali majibu ni kususia uchaguzi au kuziria uchaguzi.
1. Je fomu Za walioteuliwa na Majina yao Ndio yanayoletwa wilayani au ni kubeba mzingo wote waliochukua fomu na kumpelekea mwenyekiti wa ccm wa wilaya na Katibu wake?
2. Je Kanuni Za uchaguzi wa ccm kwenye ngazi ya matawi na kata unaelekeza mfumo alioutumia Katibu wa ccm wa wilaya kuchukua fomu zote Za wagombea ngazi ya kata na kukaa nazo hadi siku atapenda kuzirudisha?
3. Je mikoa mingine ngazi ya wilaya Makatibu wa ccm wa wilaya wamefanya uhuni alioufanya Katibu wa ccm Hai?
4. Je kwanini amechukua fomu walizojaza wagombea zaidi ya 500 kutoka kata 17 zinazounda wilaya ya Hai bila kuishirikisha sekretariet ya chama wilaya wala kamati ya siasa ya ccm wilaya na
Akamshirikisha mwenyekiti wa ccm wilaya tu?
5. Je Kwanini Katibu wa ccm na mwenyekiti wa ccm wilaya wameanza kuchukua fomu ,Majina na namba Za simu Za wagombea mapema kabla ya uteuzi wa wahombes na uchanguzi?
Kuna agenda gani kama Sio kuharibu na kuvuruga uchaguzi wa ccm?
6. Je mkoa wa Kilimanjaro una wilaya zaidi ya saba je wilaya zingine Makatibu wa ccm wa wilaya Wanafanya ujinga kama huu wa kuchukua fomu Za wagombea kabla ya vikao vya chama kwenye ngazi Za chini kujadili Majina na mapendekezo?
7. Je Katibu wa ccm wilaya anasimamia uchaguzi wa chama kwa kutumia kanuni zipi na miongozo ipi na ya mwaka gani ya uchaguzi wa ccm kwa wilaya ya Hai?.
8. Je Katibu wa ccm wilaya ya Hai anafahamu na kutambua madhara ya kuharibu uchaguzi wa Ndani wa ccm especially kwa jimbo la Hai lililokuwa ngome ya chadema kwa miaka mingi?
9. Katibu wa ccm anatambua kuwa fomu za wagombea wote wa chama ni mali ya chama na zinasitahili kujadiliwa na kupitiwa na vikao halali ili kupata bara za vikao na wagombea halali badala ya mtindo alioutumia yeye kuzinyakua kutoka kwenye kata?
10. Katibu wa ccm Hai, anatambua kazi ya sekretariet ya ccm wilaya na Kamati ya siasa ya wilaya kwenye shughuli zinazohusu uchaguzu wa ndani ya chama?
12. Kwa maswali yote yaliyotajwa hapo juu ni wazi kuwa uchaguzi Wilaya ya Hai ndani ya ccm ukifanyika utakuwa sio wa haki kwa wagombea wengine na ili haki ifanyike kuna kila sababu Katibu wa ccm Hai kupishwa au kusimamishwa kusimamia uchaguzi hadu hapo uchaguzi wa ccm Mkoa wa Kilimanjaro utakapomalizika. Kwa sababu ataharibu hata zoezi zima la kuchagua mwenyekiti wa ccm Mkoa pamoja na wajumbe wote kwani fomu alizozichukua za wajumbe wote wa Kata ni wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa isiupokuwa wajumbe wa wilaya na kata.
13. Mwisho tunasusitiza kwa nia ta kukinusuru chama kuwa Mr Bsllo Musa Katibu wa ccm Wilaya ya Hai ni kiongozi hatari na asiyestahili kuruhusiwa kusimamami, kuratibu na kutangaza matokeo ya uchaguzi ngazi ya wilaya ya Hai, hivyo kipindi hiki cha uchaguzi apangiwe majukumu mengine na apigwe marufuku kujihusisha na shughuli za uchaguzi wa ccm.( Wananchi wa Hai wanaipenda ccm na wapo tayari kuichagua ccm na kuwapata viongozi imara na shupavu bila kumtumia Jatibu wa ccm MrBallo).
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Swali haya Katibu wa ccm wa mkoa aliulizwa hakutaka kujibu wala kuelezea kanuni Za uchaguzi ndani ya chama.
Katibu wa ccm wa wilaya ya Hai anaendesha uchaguzi wa ccm kibabe na kihuni bila kufuata kanuni na miongozo ya ccm kama chama tawala.
Katibu Ajajifunza na kuelimishwa kuwa wilaya ya Hai ni wilaya ya kimkakati hivyo akicheza na uchaguzi huu, mwisho kutakosekana wagombea wanaotokana na ccm na uchaguzi kutokafanyika au ukifanyika wateule watakuwa zao la CDM na mwisho atakushababishia chama kuwa chama cha upinzani kwenye Jimbo kama kilipotokea.
Tume Wasiliana na Katibu wa ccm mkoa wa Kilimanjaro Mh Mabya simu yake ilikuwa inaita tu ila Tumetuma ujumbe kwa sms na ulipokelewa na haujajibiwa.
Tunashauri na kupendekeza Katibu wa ccm Hai ambayo upande wa pili unagawa mlungula ili ccm ipate wagombea weak asimamishwe kusimamia uchaguzi wa ccm mapema na haraka kukinusuri chama kipindi hiki cha uchsguzi utakao pelekea ccm Hai kushinda uchaguzi mkuu 2025 na serikali za mitaa 2024.
Chadema waweka msimamo kuelekea chaguzi hizi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025 kama Katiba Mpya haitapatikana.