Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Singida Mjini, Hamis Nkua, amechomwa kisu katika mkono wa kushoto begani.
Akizungumza na Nipashe Digital katika Hospitali ya Rufaa ya Mandewa ya Mkoa wa Singida ,amesema amechomwa kisu leo Novemba 27, 2024 saa 8:00 mchana katika eneo la Unyankae kata ya Mandewa Manispaa ya Singida.
Nkua ambaye wakati akizungumza nguo zake zilikuwa zimetapakaa damu,amesema amechomwa kisu wakati alipokwenda na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya Singida mjini,Swahiba Mwanga eneo ka Unyankae baada ya kupigiwa simu na viongozi wa kata wa chama hicho kwamba wamevamiwa.