LGE2024 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Singida achomwa Kisu na kijana wa CCM akiwa eneo la kupiga kura

LGE2024 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Singida achomwa Kisu na kijana wa CCM akiwa eneo la kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Singida Mjini, Hamis Nkua, amechomwa kisu katika mkono wa kushoto begani.

Akizungumza na Nipashe Digital katika Hospitali ya Rufaa ya Mandewa ya Mkoa wa Singida ,amesema amechomwa kisu leo Novemba 27, 2024 saa 8:00 mchana katika eneo la Unyankae kata ya Mandewa Manispaa ya Singida.

Nkua ambaye wakati akizungumza nguo zake zilikuwa zimetapakaa damu,amesema amechomwa kisu wakati alipokwenda na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya Singida mjini,Swahiba Mwanga eneo ka Unyankae baada ya kupigiwa simu na viongozi wa kata wa chama hicho kwamba wamevamiwa.
 
View attachment 3163345

Ukiona haya mambo kina Mwashambwa wanahofu na upinzani!
 
Huyu ni mtu wa ngapi anajeruhiwa au kuuawa kwa jina la CCM ?.
Yakipita 72 Masaa watakuwa wengi wameshapotezwa.
 
Duuh yaani ni hivyo hivyo vyeo vya mitaa mpaka damu zinamwagika au kuna mengine watu wanamalizana kwa visingizio vya uchaguzi............
 
Ccm sio watu.....ujumbe wa mtaa tu ni vita.

Kwanini hawakubali kushindwa.

Who is supporting them? Nani anawatuma?
Daaah nachoka kabisa.
Wanafanikisha haya kusafisha njia ya mwakani.
 
Haya mauaji yanayoendelea kwa wana chama, viongozi na wwgombea wa nafasi mbalimbali kwenye huu uchafuzi wa serikali za mitaa ni kielelezo tosha kabisa kwamba CCM imekwisha kabisa

Walianza kuteka, kutesa, kujeruhi, kupoteza na kuua wapinzani wao kisiasa hasa CHADEMA lakini sasa wanafanya waziwazi bila kificho
Ni hofu gani hii kubwa kabisa iliyowakumba mpaka wanafanya mauaji mengi kiasi hiki
Wataua wangapi!
Watajeruhi eangapi!
Watapoteza wangapi!
Kila wanachofanya kwasasa wanazidi kuharibu

Ogopa sana mateke ya mwisho ya ng'ombe aliyekata roho..hii ndio ccm ilipofikia kwasasa
 
nawapongeza polisi kwa kuimarisha amani kipindi hiki cha uchaguzi

pia nawapongeza wanachama wenzangu wa chama cha mapinduzi kwa ushindi wa kishindo maeneo mengi nchi hakika watanzania wameonyesha ukomavu kisiasa kwa kuchagua kilicho bora
 
Back
Top Bottom