Naomba tu kuelimishwa uhusiano wa ukuu kati ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na mbunge/waziri kupitia CCM.
Naingia ibadani Mungu awabariki sana.
Maendeleo hayana vyama!
Chama tawala ndio chenye serikali, chama ndio kinaandaa ilani ya uchaguzi, kisha chama ndio kinaenda kunadi ilani hiyo kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu
Wananchi wakielewa na kukubali ilani hiyo, wanachagua chama hicho kushika madaraka
Baada ya chama kushika madaraka, kinaunda serikali, na kisha chama kinakabidhi madaraka kwa serikali kwa lengo la serikali kutekeleza ilani ya uchaguzi iliyowapa dola( kuchaguliwa na Wananchi)
Kwa msingi huo,chama ndio chenye serikali
Sasa katibu wa NEC itikadi na uenezi wa CCM, kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977, kwa nafasi yake ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa( Central commitee), ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa ( National Executive Council) pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa
Sasa kwa katibu wa NEC itikadi na uenezi, kuwa mjumbe wa vikao vya juu kabisa vya maamuzi ndani ya chama cha mapinduzi, ambacho chama ndio chenye serikali
Hiyo inampa hadhi ya juu zaidi ya waziri, mkuu wa mkoa nahata mbunge
Ndio maana mwenyekiti wa CCM taifa ni mkubwa zaidi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania( Rais atakayetokana na chama cha mapinduzi)
Na hiyo ndio msingi wa CCM kuamua kuunganisha kofia ya Rais na mwenyekiti wa CCM taifa, kuepusha misuguano
Chama tawala ni kikubwa kuliko serikali